Nataka kujenga chumba na sebule ya dharura

MBUZI MWENYE BUSARA

Senior Member
Nov 24, 2019
143
151
Wakuu habari za hapa jamvini?

Nitumbukie kwenye mada yenyewe.

Ni hivi nilijenga msingi wa nyumba ya vyumba vitatu moja master, sebule, dining, stoo na public toilet katika plot mbili tofauti na sehemu tofauti pia moja wilayani kwetu na nyingine katika kata yangu. Sasa kote nimeshindwa kuendeleza na nipo mjini nalipa Kodi nyumba. Sasa maisha yamenigonga kweli kweli.

Nimeamua sasa kuuza plot moja na msingi wake ile ya kwenye kata nije nijenge kwa dharura chumba kimoja na sebule tu bila mbwembwe nyingi. Nimempata mteja anataka kwa milioni tatu tu! Je kwa pesa hii nitamaliza hiyo project?

Wataalam msaada.

Nikishajenga hicho chumba na sebule familia itakaa humo wakati naendeleza jengo kubwa.
 
Suala la kuweza au kutokuweza kwa hiyo pesa inategemea unatarajia kujenga wapi? Gharama za ujenzi zinatofautiana kutoka eneo moja hadi lingine.

Kuna sehem tofali za kuchoma za nyumba nzima unazipata kwa 600,000/-

Mbao na mabati hali kadhalika inategemea unaezeka kwa mtindo upi? Slope, mgongo wa tembo au maparamanne?

Ila kwa Dar chumba kimoja na sebule kisicho na mbwembwe ukijibana inawezekana.
 
Kama unauza kiwanja na msingi kwa 3m huoni kuwa ushapata picha 3m itakufikisha wapi?
Ukiuza kiwanja Chenye msingi wanunuaji hua hawahangaiki na msingi ulioujenga(haupigwi kwny gharama za kiwanja) na Kuna mnunuzi mwingine anakwambia ukitaka ubomoe kabisa huo msingi uondoke nao Maana sina Mpango nao.
 

Similar Discussions

3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom