Nataka kuingia kinyang'anyiro cha Ubunge jimbo la Kwela, nipeni data! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nataka kuingia kinyang'anyiro cha Ubunge jimbo la Kwela, nipeni data!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Malinga, Nov 30, 2009.

 1. M

  Malinga Member

  #1
  Nov 30, 2009
  Joined: Nov 9, 2009
  Messages: 6
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ndg zangu wana JF, ninaishi Mwanza, na ni mzaliwa wa mkoa wa Rukwa. Nimesoma thread inayohusu Mrema na Kimaro kule Vunjo; malumbano yao yameibua kitu ndani mwangu, kile nilichokuwa nikikitamani miaka mingi, yaani ukombozi wa jimbo la Kwela. Nimeguswa na kuelewa kwamba siyo tu vunjo inayokaliwa kimabavu na wanasiasa wasio na msaada kwa wananchi, hata Jimbo la Kwela, Sumbawanga (mh Mzindakaya). Nataka nikatoe changamoto na hatimaye kungo'oa kisiki hicho cha mpingo katika kinyang'anyiro cha Ubunge kupitia CCM, kuanzia kura za Maoni.

  Sina uzoefu mkuubwa sana katika siasa, lakini elimu yangu ni ya chuo kikuu na uzoefu wa kutosha katika shughuli nyingine za kijamii, siyo siasa.

  Ningependa kupata taarifa zifuatazo:

  a) Fukuto la uchaguzi la mwakani katika jimbo hilo!

  b) Kura za maoni zitafanyika mwezi upi

  c) Ni nani na nani ambao wamejitokeza hadi sasa ktk kuonyesha nia ya kuingia katika kinyang'anyiro. Ukimfahamu mshindani wako ni rahisi kumng'oa.

  d) Sifa za mtu anayetakiwa kugombea ubunge, kupitia CCM!

  Naombeni taarifa za kina zitakazo nisaidia kujipanga vyema.

  Nitafurahi kama mtanishirikisha kwa PM (private message) ili msianike mchele kwa kuku wengi.
   
 2. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #2
  Nov 30, 2009
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Utapitia chama gani kwenye kugombea? Tuanzie hapo kwanza!
   
 3. bht

  bht JF-Expert Member

  #3
  Nov 30, 2009
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 10,341
  Likes Received: 209
  Trophy Points: 160
  Masa hope u will note the bolded and underlined
   
 4. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #4
  Nov 30, 2009
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 541
  Trophy Points: 280
  kwenye thread yake kasema atapitia chama cha ccm
   
 5. Kituko

  Kituko JF-Expert Member

  #5
  Nov 30, 2009
  Joined: Jan 12, 2009
  Messages: 9,366
  Likes Received: 7,007
  Trophy Points: 280
  Naona siku zako za kuishi duniani zinakaribia kuisha, yaani majimbo yote huyayaona mpaka kwa XCANT MAJIYATANGA MZINDAKAYA, JARIBU TUONE
   
 6. E

  Ex-Fisadi Member

  #6
  Nov 30, 2009
  Joined: Aug 19, 2009
  Messages: 79
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mzee, kwa taarifa ulizomwaga hapa JF, mi naona hufai kuwa hata mwenyekiti wa mtaa. Nakushauri usubiri na kujifunza siasa kwanza kwa kwenda ukajiandikishe kupiga kura hukohuko jimboni halafu utajua cha kufanya baadaye.
   
 7. nguvumali

  nguvumali JF Bronze Member

  #7
  Nov 30, 2009
  Joined: Sep 3, 2009
  Messages: 4,864
  Likes Received: 143
  Trophy Points: 160
  Kituko please, usimvunje moyo, kwanini afe, huyu simuamiaji kule , ni mwenyeji, mzawa......
  kaka nenda kamng'oe Mzindakaya Maji ya Tanga.
   
 8. ELNIN0

  ELNIN0 JF-Expert Member

  #8
  Nov 30, 2009
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 3,771
  Likes Received: 221
  Trophy Points: 160
  Si Kwela tu MKuu, Majimbo yapo mengi tu ya kubeba, kuna jimbo la kwetu kule Sikonge pia halina mtu, huyu jamaa aliachiwa na babake, wakati mi niko darasa la pili miaka ya 80 babake alikuwa mwenyekiti wa ccm tabora vijijini - kamwachia mwanae, sasa hakuna maendelea yoyote kule. nilienda xmas ya mwaka jana nikaombwa nigombee na watu kibao ulizingalia nimekuwa nikienda kwetu mara kwa mara na nimekuwa nikisaidia miradi midogo midogo ya kilimo.

  tatizo sijawahi kuwa mwanachama wa chama chochote kwa sababu sipendi kusema uongo na kudanganya watu, ila elimu ni chuo kikuu - uhandisi.

  kwa wale wenyeji wa sikonge watanikubalia kwamba huko tuna jimbo ila halina mbunge, na hilo tulichukue
   
 9. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #9
  Nov 30, 2009
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Mhhhh haya bwana kila laheri
   
 10. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #10
  Nov 30, 2009
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  teh teh huyu anatafuta kutolewa mshipa ....we muache ajishauwe tu ..anathubutu kutaka kuchukua fomu kwenye jimbo la Mzindakaya???hahaaaa
   
 11. Liz Senior

  Liz Senior JF-Expert Member

  #11
  Nov 30, 2009
  Joined: Apr 19, 2007
  Messages: 485
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Mimi nina wasiwasi kama utaweza kufanya lile aliloacha kulifanya Mzindakaya, maana hata taarifa muhimu luhusu jimbo unalolifikiria huna! Pengine una nia njema sana ila tu kwa sasa bado hujawa tayari. Na hata mchakato wa kufikia kuwa mgombea ndani ya chama chako hicho taarifa zake huna, pengine unahitaji kufanya kazi ya ziada kwa ajili ya 2015. Vinginevyo itabidi ukapige kambi kule kuanzia sasa.
   
 12. ELNIN0

  ELNIN0 JF-Expert Member

  #12
  Nov 30, 2009
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 3,771
  Likes Received: 221
  Trophy Points: 160
  Mzee kama ni kwela, tena kwa ticket ya si si emu, mi sipo .... aga kabisa familia kaka kabla hujaanza mchakato.
   
 13. F

  Fungu la kukosa Member

  #13
  Nov 30, 2009
  Joined: Jun 16, 2009
  Messages: 64
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Dear Msanilo, I am happy to learn that your currently planning to contst for MP at Kwale constituency which for the last 30 years has been under the control of Chrisant Mzindakaya.I will very gratfyl if you can provide me with any an appropriate means of communication through which the information you required can be provided easily.For security reason I think is not good to pour out millet over thousands of peagions as once pro-mzindakaya know what you intend to do against him, they will also find a better deffensive mechanism against you.You have to know that Mzindakaya is not an easy man.He is primarilly wizard man in all atitudes.He killed MP for Kigoma Urban constituency when he was a regional Commission for kigoma and he used that post to benefit himself by running illgeal business of gold and diamond under government name.When Kigoma MPs united against him under leadership of Mbano, he victimised him.He also used his authority as Regional Commisioner to utilize prisoners'manpower contrary to the law.Prisoners had to work on his firms of more than 1000 hectors free of charge just because he was RC.THESE ARE JUST A HINT ONLY OF INFORMATION YOU NEED BUT I WILL BE ABLE TO TELL YOU MUCH FURTHER THAT THAT IF ONLY YOU PROVIDE WITH ME JUST A FORGILED E-MAIL ADDRESS FOR CONTACT BETWEEN YOU AND I.fOR THE TIME BEING IAM IN THE UK FOR PhD STUDIES.
   
 14. Sisimizi

  Sisimizi JF-Expert Member

  #14
  Nov 30, 2009
  Joined: Nov 10, 2009
  Messages: 490
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 35
  Mhhhhh! Kama haya ndiyo maoni tunayompatia mshikaji sooo! Tunalalaika juu ya viongozi wasiofaa halafu, Ex-Fisadi.

  malinga
  Usihofu, tutakupatia data kwa PM.

  Big up kwa moyo wa ushujaa. Lazima Goliathi aangushwe kwa kamkono na kombeo la ka Daudi.

  Keep it up!
   
 15. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #15
  Nov 30, 2009
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Fungu la Kukosa

  Got it wrong, I have no ambitions to become a politician at all, am happy with what have been doing for my country. Its Mr/Miss Malinga who is vying to uproot Hon Dr Mzindakaya in Kyela constituent! for records keep it clear
   
 16. RayB

  RayB JF-Expert Member

  #16
  Nov 30, 2009
  Joined: Nov 27, 2009
  Messages: 2,754
  Likes Received: 88
  Trophy Points: 145
  Kwako Mh Mbunge mtarajiwa,
  Kwanza naomba uelewe kuwa ubunge wa kiukweli sio huo wa kuulizia data kutoka nje ya eneo, unatakiwa ulijue jimbo lako kwa undani na pengine kuishi na ile jamii kwa muda wa miaka kadhaa ya karibuni kabla ya 'kugombania' hilo lijicheo. You have to know your community in and out.
  Pili kuijua jamii yako si kwa mtindo huo unaotaka kufanya kama research ya eneo husika kwa kuandaa questionnaire uliyotupa hapo juu unless otherwise kama unataka kuwa Mbunge kama Hussein Mwinyi manake nasikia ni Mbunge huko Zenji lakini watu hawamjui na alifanya kazi ya ziada kushinda (ya ziada kweli kweli hadi usanii ndani) manake Mohammed Dewji 'Mo' anafahamika Singida kuliko Mwinyi Zenji. Ni mtazamo wananchi
   
 17. RayB

  RayB JF-Expert Member

  #17
  Nov 30, 2009
  Joined: Nov 27, 2009
  Messages: 2,754
  Likes Received: 88
  Trophy Points: 145
  Hey Masanilo

  You know may be you have those qualities in you as unseen and unrecognizable traits as I think this message wouldn't have fallen to you with no purpose so might need to start thinking of it now be it Kwela or somewhere alike
   
 18. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #18
  Nov 30, 2009
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 541
  Trophy Points: 280
  Malinga nimeona watu hapa wanasema kama huogopi kutolewa maini ,figo,sijui filigisi ,
  kwanza usiamini mambo ya kishirikina ingawa yapo kama uko na plan nzuri na wananchi pls go for it ..kwanza anza kwenda huko mala kwa mala ongea na wananchi na uwaonyeshe nia yako na uwezo wako kiuongozi ..toa sera na msimamo wako wa kueleweka kama 2010 hutapata angalau utakuwa kiasi umetambulika na raia wa huko ..then 2015 unaingia kwa upya
   
 19. E

  Ex-Fisadi Member

  #19
  Nov 30, 2009
  Joined: Aug 19, 2009
  Messages: 79
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mzee Malinga,
  Kwanza naomba uniwie radhi kwa kukuambia ukweli kuwa hufai kuwa hata Mwenyekiti wa Kitongoji. Kwa unyenyekevu na kusumwa na dhamira ya kweli nimekwambia usigombee kwa sababu yaelekea wewe hujui chochote kwenye siasa na wala haielekei kama ni mwanachama wa CCM, chama unachotaka kupitia kugombea ubunge huo.

  Nimeona watu wote wanakushauri uende jimboni ujifunze mazingira ya huko ndipo ugombee. Maana yake ni nini hiyo? Wanakuambia kuwa huwezi ukawa mwakilishi wa watu usio wajua, kwa hiyo hufai kabisa kuwa mjumbe wa watu wa Kwela.

  Kwenye thread yako unauliza kuhusu kura ya maoni!! La haula, haionyeshi kama wewe uko serious na unachotaka kufanya. pia yaelekea haujui utamaduni wa CCM na nguvu zao ziko wapi. CCM hushinda chaguzi mbali mbali kwa kutumia ujinga au kutokufahamu kwa wananchi. Wewe hauwezi kushinda au kupitishwa kwenye kura za maoni kupitia JF! Ni lazima uijue CCM, umjue Mzindakaya na mapungufu yake. Nina wasiwasi kama wewe ni mwanachama wa CCM, mtu usiyejua strength yenu iko wapi.

  For your information ni lazima ujifunze kuwa Fisadi (mimi niliisha acha), ujifunze kunyenyekea kwa wajumbe wa mkutano mkuu wa Jimbo, uwe na Fedha za kutosha za kukata kidogo kidogo kama takrima kwa wajumbe, ujue beii ya Mwenyekiti na Katibu wa CCM wa Wilaya na Mkoa, vile vile uanze kujisogeza sogeza kwa Pinda ili aje kukulinda kwenye CC hata kama utakuwa umepita kwenye kura za Maoni!

  Vinginevyo ninacho kiona kwako ni giza tupu. hufai kuwa Mbunge wa Kwela na wala sidhani kama hata unastahili kuwa mgombea kupitia sisiem labda jaribu DIPI ya Mtikila
   
 20. bht

  bht JF-Expert Member

  #20
  Nov 30, 2009
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 10,341
  Likes Received: 209
  Trophy Points: 160
  Mi nadhani haitakua busara kwa Malinga kufanya hivyo sasa kwa kuwa anaonekana kama hafahamu hata hali halisi ya Kwela...better kama kweli ana nia thabiti ayasome mahitaji ya wananchi pale kabla ya kuingia kichwa kichwa kwa kuwa itakua same story....longlongo tu!!!

  utawasaidiaje watu ilhali hata hujui matatizo au mahitaji yao??? (hulifahamu jimbo) nashawishika kusema msisiemu wewe unakurupuka na naogopa usije ukawa huna jipya....
   
Loading...