Nataka kuhamia Kijijini ni ndoto yangu

Eliud Bunju

JF-Expert Member
Nov 26, 2017
342
625
Mimi ni mzaliwa wa mjini Dar es Salaam lakini makuzi yangu yote ni kijijini badae nikarudi tena Dar baada ya kumaliza shule.

Nimeoa nina miezi 5 katika ndoa mke wangu ni mtu wa mkoa ninao toka mimi namaanisha Mbeya green city.

Mimi Nimuajiliwa serikalini kabla sijaoa nilikua nahamu sana ya kufanya kazi Mbeya haswa Tukuyu mjini ama Tunduma namaanisha wilaya yoyote sio Mbeya mjini ama Songwe mjini

Sasa hivi naishi Bagamoyo lakini kiukweli mji wa Bagamoyo unawatu wachache na umepoa sana pia heshima ya huyu mke wa mtu haipo hapa.

Pia suala la fedha biashara ni ngumu sana hapa maana watu wake ni wavivu kupita maelezo duka linafunguliwa saa 3 ni jambo la kawaida kwao.

Sababu za kuhamia Mbeya

- Kwanza napapenda sana
- Pili maisha yako chini sana
- Tatu hakuna kitu ambacho huwezi fanya kama bichi zipo Kyela
- Nne watu wake wapo active muda wote ni watu wa biashara na kupenda elimu sana
- Tano ninandoto ya kusoma mambo ya kilimo nadhan itakua vizuri nikisoma Mbeya chuo tayari nimekiona mfano wilaya ya Rungwe Tukuyu kipo.
- Mke wangu pia ananitia moyo hata kesho yupo tayari siwazi mengine maana nilimtoa bikira mwenyewe
- Ninahisi ni sehemu sahihi kwangu maana kilimo chake n chepesi sana na ninapenda sana kilimo
- Hali ya hewa ni tamu sana Tukuyu
- Ni mkoa ambao kuna neema ya chakula sana na watu wake ni wakarimu
- Napapenda Tukuyu kuliko sehemu yoyote Tanzania.
- Viwanja vinapatkana kwa bei nzuri tu

.Naomba ushauri wako.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mbeya japo jiji mzunguko wake wa fedha kwa wafanya biashara bado ni mdogo sana pia.

Ni mji mzuri sana kwa watumishi( waajiriwa) sababu unaweza save tokana maradhi kama chakula, nyumba zipo bei ya chini.

Ukiwa na elfu kumi ukienda sokoni unarudi na furushi la mazaga zaga.

Na sehemu nzuri sana kuishi ni wilaya ya rungwe.( hii wilaya imebarikiwa sana kwa vitu vingi ukiweza jiongeza utatoboa mapema) na wanyakyusa wa rungwe kiukweli ni wacheshi na wakarimu sana.
 
kama unakiri sehemu uliyopo watu ni wavivu na interest yako ni kilimo nadhani hapo panafaa zaidi kutoboa kimaisha kulilko tukuyu maana utalima utawauzia kwani hata ukiwa mvivu lazima ule.Utafuga utawauzia
Wavivu.
sasa ukienda Tukuyu kila mtu analima na kufuga utamuuzia nani?
Ni mtazamo wangu mkuu we ndo mwamuzi wa mwisho.

Sent using Jamii Forums mobile app
Kuna fursa ya kusoma pia chuo cha kilimo huko Mbeya

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mbeya japo jiji mzunguko wake wa fedha kwa wafanya biashara bado ni mdogo sana pia.

Ni mji mzuri sana kwa watumishi( waajiriwa) sababu unaweza save tokana maradhi kama chakula, nyumba zipo bei ya chini.

Ukiwa na elfu kumi ukienda sokoni unarudi na furushi la mazaga zaga.

Na sehemu nzuri sana kuishi ni wilaya ya rungwe.( hii wilaya imebarikiwa sana kwa vitu vingi ukiweza jiongeza utatoboa mapema) na wanyakyusa wa rungwe kiukweli ni wacheshi na wakarimu sana.
....maradhi....
 
Kama chuo cha kilimo, unaweza kwenda Pale MATI UYOLE kipo fresh.. Utapata mafunzo yako pale then unaingia kwenye kilimo chenye Tija..
Kama utalima mpunga me nitakuja kufanya biashara nawe, kozi Nina ndoto za kufanya biashara ya Mazao..
Nipo Mikoa ya Kusini Mashariki
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom