Elections 2010 Nataka kugombea urais wa tz 2010

lazima uwe na slogan moja kali sana, kama vile "uwazi na ukweli", " kasi mpya, nguvu mpya na ari mpya",wewe yako iwe KIBOKO CHA MAFISADI, au UFISADI KWANGU MWIKO, au kali zaidi uahidi kufanya kazi bila mshahara.Chakula si nasikia bure ikulu? Hapo utashinda mara moja.
 
Lazima uwe mbea kama yule anayesema TZ nzima hajaona mahali palipojengwa vizuri kama University of Dodoma! Na pia alisema akiingia madarakani ataleta 'mapinduzi ya kilimo'!

Kaniki,
Hapo mimi sijui.
Kuna wa jinsi hiyo hapa TZ au ni Burundi labda?
 
lazima uwe na slogan moja kali sana, kama vile "uwazi na ukweli", " kasi mpya, nguvu mpya na ari mpya",wewe yako iwe KIBOKO CHA MAFISADI, au UFISADI KWANGU MWIKO, au kali zaidi uahidi kufanya kazi bila mshahara.Chakula si nasikia bure ikulu? Hapo utashinda mara moja.

Kwame,
Nikiwachokoza mafisadi nitafika kweli?
 
Na lazima upromise ajira milioni tano na maisha bora kwa kila mwanachuo maana wamegoma sana mwaka huu! Lazima uwe mbea tosha..
 
Na lazima upromise ajira milioni tano na maisha bora kwa kila mwanachuo maana wamegoma sana mwaka huu! Lazima uwe mbea tosha..

KANIKI,
Nitampromise nani na nimwache nani?
Vyuo viligoma, waalimu, reli, wastaafu, n.k
Mbona kazi mkuu.
 
Uchawi ni lazima pia, tena ukiweza kushambuliwa kwenye kampeni huko Mwanza na kuanguka chini Jangwani, jua ushindi wako utakuwa wa kishindo above 80%....ok?
 
Uchawi ni lazima pia, tena ukiweza kushambuliwa kwenye kampeni huko Mwanza na kuanguka chini Jangwani, jua ushindi wako utakuwa wa kishindo above 80%....ok?

Kaniki.
Ee e e e,
Mbona cheo hiki kinatisha?
Hivi ndivyo mambo yanavyotakiwa kwa 2010 au hata kabla?
 
Exaud,

Kwa nini unataka kwenda ikulu? Nini kinakuvutia (motivation)?

Kwa nini Tanzania Bara na si Tanzania?(au ulimi/vidole vimeteleza:)?). Kama ni Tanzania Bara nadhani katiba tuliyonayo kwa sasa haitoi hiyo nafasi.

Kama ni Tanzania kwa ujumla, basi ni wazo zuri lakini naona umechelewa kuanza. Kugombea Urais,kwa maoni yangu, unahitaji maandalizi ya si chini ya miaka mitano! 2010 ni 'kesho' tu!. Kutokana na muda, ili umshinde JK, utahitaji nzuvu za ziada. Pamoja na mabo mengine;

-Ni lazima ufahamike vizuri kwa watanzania (hili linahitaji muda na rasilimali)
-Ni lazima uifahamu vizuri Tanzania na watanzania (SWOT analysis inaweza kukusaidia!).

Umesha-recruit campaign manager?

SMU,
Unashauri nisubiri mpaka 2015?
Watu wameshauri masuala ya uchawi,kujifunza kudanganya,kutoa ahadi kibao, nk.Wewe hayo unaona ni sawa?
 
Unataka kugombea urais wa Tanzania Bara?

Sasa mbona unaleta mambo Palin mkuu, mambo ya kuona Africa ni nchi na ukikaa alsaka unaona Russia.
Unataka kugombea urais wakati hata hujui kama hii nchi unayoizungumzia kikatiba ipo au haipo.
Weka sawa hapa Mkuu.
 
Unataka kugombea urais wa Tanzania Bara?

Weka sawa hapa Mkuu.

PUNDAMILIA,,
Kimsingi na kivitendo, huyo rais mnayemwita wa Tanzania, ni rais wa Tanzania bara.
Kinadharia, hapo hapaelezeki.Nisije nikazua mjadala kama Zanzibar ni nchi au laa.
Basi niseme Rais wa Tanzania ili iwe rahisi kama mazoea yalivyo.
 
SMU,
Unashauri nisubiri mpaka 2015?
Watu wameshauri masuala ya uchawi,kujifunza kudanganya,kutoa ahadi kibao, nk.Wewe hayo unaona ni sawa?

2015 nadhani ni realistic zaidi kuliko 2010. Watanzania wanataka mabadiliko, lakini kwa sehemu kubwa chama dola kimekuwa kikiviza hamu hii ya watanzania.

Siamini uchawi. Kuna njia nyingi za uhakika za kujenga kujiamini (confidence) na kuaminiwa (credibility)zaidi ya waganga wa kienyeji.

Sio lazima kudanganya katika siasa. Unatakiwa kuwa visionary. Ahadi ni lazima zitokane na uelewa wa mambo na uwajibikaji. Ni lazima uwe tayari kusupport ahadi zako kwa kuandaa mikakati madhubuti na yenye kuaminika.

Kama unataka kugombea urais 2015, basi ingekuwa vema kama ungegombea ubunge 2010. Kwani wewe ni mwanachama wa chama gani?
 
Mawazo yako yamekaa vizuri sana, ila unashauri nini kuhusu kuwa mgombea kwa kupitia vyama vya upinzani?
 
............................................................................................
Lazima pia uwe na fedha nyingi. Kama unafahamiana na Gavana wa Benki Kuu,hiyo itasaidia.

Ganesh,
Kufahamiana na Gavana wa benki kuu?
Mbona hata sura yake siijui?
 
Wazo lako zuri, inaelekea unapenda siasa. Kwanza kabisa mwache JK amalizie ngwee yake ya 2010-2015. Huo mwaka 2010 unaotaka kugombea uraisi hakikisha unapata ubunge kwanza halafu uingie dodoma pale bungeni maana utapata exposure na network ya kutosha.
Au tayari una kikundi cha kampeni? Chama cha upinzani mmh! sijui kama utapita japo sina uhakika sana. CCM na mambo yote mabaya na mazuri ndo kipo madarakani, ila itapendeza na kuweka historia siku tukipata raisi toka chama cha upinzani tuweze kupata changamoto mbalimbali za utendaji.
Best of luck katika maandalizi yako.
 
PUNDAMILIA,,
Kimsingi na kivitendo, huyo rais mnayemwita wa Tanzania, ni rais wa Tanzania bara.
Kinadharia, hapo hapaelezeki.Nisije nikazua mjadala kama Zanzibar ni nchi au laa.
Basi niseme Rais wa Tanzania ili iwe rahisi kama mazoea yalivyo.

Mkuu Makyao,

Don't start your race with a wrong foot. Kama wewe umeamua kutaka kugombea urais basi hakikisha kila unalolifanya na kulisema liko sahihi kwani kinyume chake ni sawasawa na kujifunga mabomu mwenyewe.

Tunategemea Rais ndiye mlinzi Mkuu wa Katiba (Haijalishi kama katiba ni nzuri au mbaya) sasa endapo hapa katika kuulizauliza tu unaonesha hauko tayari kuiheshimu katiba iliyoko, je ukipata urais hutajiongezea vipindi vingine kadhaa vya uongozi kama Rais?
 
Kama unataka kuwa Rais 2010,you have to talk,talk,talk,on every conceivable subject,from now on until you declare your candidacy,ili watu wakufahamu,ama sivyo you will declare that you want to be President,halafu watu watuliza,"Exaud Who?"
You must talk.A politician must exercise his vocal chords.
 
Back
Top Bottom