Nataka kugombea ubunge ila si mwanachama wa chama chochote

MOSHIFST

Senior Member
Jun 4, 2014
136
247
Wakuu nataka kugombea ubunge lakini sijawahi kuwa mwanachama wa chama chochote kile na sina kadi ya chama chochote kile iwe chama cha kijamii au kisiasa.
Nina elimu ya Uzamili katika masuala ya kilimo
Nina miaka 30
Nina uzoefu wa zaidi ya miaka 5 katika sekta binafsi.
Nina kiu ya maendeleo jumuishi hasa kuwekeza katika elimu ya kilimo na kuongeza mazao thamani.
Mmbunge wetu kwa sasa ni darasa la saba ila chama sitakitaja.

Je nawezaje kugombea ubunge mwakani?
 
Aanza kumsifia bwana mkubwa utafikiriwa,hizo sifa kwa wenzako ni ziada ila pia uwe na pesa vinginevyo yatakushinda.

Ukitaka kupambana kwa haki kupata huo ubunge,basi gombea kupitia vyama vile vingine ambavyo haabudiwi mtu.
 
Wakuu nataka kugombea ubunge lakini sijawahi kuwa mwanachama wa chama chochote kile na sina kadi ya chama chochote kile iwe chama cha kijamii au kisiasa.
Nina elimu ya Uzamili katika masuala ya kilimo
Nina miaka 30
Nina uzoefu wa zaidi ya miaka 5 katika sekta binafsi.
Nina kiu ya maendeleo jumuishi hasa kuwekeza katika elimu ya kilimo na kuongeza mazao thamani.
Mmbunge wetu kwa sasa ni darasa la saba ila chama sitakitaja.

Je nawezaje kugombea ubunge mwakani?
Bila ubunge huwezi kutimiza hayo?!
 
Anza jifunza kuwa mnafiki, pia Fanya mazoezi ya kwenda kwa waganga kama bagamoyo Na sumbawanga.ukigombea kwa upinzani jiandae kuwekwa lockup za polis muda wowote.ukigombea kwa ccm uwe tayari kupambana kwa ushirikina Na rushwa za kuhonga wajumbe.
 
Kwani huwezi kufanya Maendeleo mpaka uwe mbunge?
Kwani wote walioiletea jamii yao Maendeleo ni Wabunge?
Kwenye huu ubunge unao lako jambo na katu sio Maendeleo kwa wananchi
 
yeah miaka kadhaa iliyopita kulikuwepo hukumu kuhusu wagombea binafsi(independent candidates)please fanya utafiti nini kilikuwemo kwenye hukumu hii.good luck
 
Kwa kutumia hiyo elimu yako, nenda mahakama kuu ili ukawaombe wakazie hukumu iliyoruhusu uwepo wa mgombea binafsi lakini mpaka leo utekelezaji wake umekuwa ukipigwa pigwa tu danadana na watawala.
 
Asante kwa maoni yako.Nadhani hii inaweza chukua mchakato mrefu sana japo ni njis rahisi sana.Ila nitalifikiria
 
Mkuu mimi ni MOSHIFST sio STEINAR

Huogopi kupigwa risasi kwa vile tu ni mpinzani?

I just think unaweza kusaidia nchi yetu bila kuwa in top position,

Fungua Charity mkuu inayohusiana na kilimo..

Unless una sababu maalumu ya kutaka kuwa Mbunge?
 
Hahha. Naomba uelekeze nia yako kwa lile jimbo la muheshimika wa mjengo pale idodomya. Ile kwenye kura za maoni hakikisha umevaa helmet
 
Wakuu nataka kugombea ubunge lakini sijawahi kuwa mwanachama wa chama chochote kile na sina kadi ya chama chochote kile iwe chama cha kijamii au kisiasa.
Nina elimu ya Uzamili katika masuala ya kilimo
Nina miaka 30
Nina uzoefu wa zaidi ya miaka 5 katika sekta binafsi.
Nina kiu ya maendeleo jumuishi hasa kuwekeza katika elimu ya kilimo na kuongeza mazao thamani.
Mmbunge wetu kwa sasa ni darasa la saba ila chama sitakitaja.

Je nawezaje kugombea ubunge mwakani?
sheria haikuruhusu ni lazima uwe mwanachama wa chama fulani ba sio ujiunge ghafla it 'll take time
 
Back
Top Bottom