Nataka kugombea nafasi ya Udiwani

Wernery G Kapinga

JF-Expert Member
Feb 2, 2012
372
119
Wan jamvi heshima kwenu

Mimi sio mzoefu wa siasa ila kwa kadri Mambo yanavyoenda hapa katani ni hovyo kabisa. Kuna mzee wangu mmoja hivi kaniambia ili uweze kugombania kiti hicho lazima ukae KISIASASIASA. Hapa ndo panaponishinda.

Sasa naomba mnisaidie mawazo, kukaa KISIASA SIASA ni kuwa mwongo sana au mzungumzaji sana?

Gharama ya kuchukua fomu ya kugombea Udiwani gharama gani?

Huku kijijini hakuna chama pinzani. Tunachokijua sisi ni chama Cha NYERERE. Ukianza kuleta upinzani jamii karibu yote itakutenga.

Changamoto ya kata yetu ni nyingi mno. Diwani aliyekuwepo anakaa zake mjini tu huko yaani Dah

Hakuna mkutano wowote aliowahi kuja kufanya na wananchi wala kumshawishi hata Mbunge aje. Siku hizi namuona anapiga sana ruti za kuja katani na wananchi wameshamgundua kwamba kumekucha na anadhani hatujamuelewa.

Safari hii labda nikose hela za fomu.
 
Kama utajua kupepeta mdomo unaweza kuwa mwenyekiti wa halmashauri na ndio mwanzo wa kuibuka rasmi kisiasa. Ila siasa ni mchezo mchafu! Utaweza!!
 
Back
Top Bottom