Nataka kufungua biashara ya Mgahawa: Naomba kuelewesha kuhusu Mtaji, Vifaa mauzo na Changamoto zake | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nataka kufungua biashara ya Mgahawa: Naomba kuelewesha kuhusu Mtaji, Vifaa mauzo na Changamoto zake

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by Mark Francis, Jul 19, 2011.

 1. Mark Francis

  Mark Francis Verified User

  #1
  Jul 19, 2011
  Joined: Nov 19, 2010
  Messages: 605
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Nimefungua biashara ya Mgahawa sehemu flani hapa mjini DSM, nimeweka wafanya kazi 3; mmoja kwa ajili ya chips na wa2 kwa ajili ya chakula kwa sababu biashara yenyewe bado changa. Eneo ambalo nafanyia biashara lina population kubwa na halina competition kubwa sana. Mimi napitia mida ya jioni kucheki jinsi biashara inavyoendela na kuhakikisha hesabu zinaenda vizuri.

  Tatizo mpaka sa hizi ni zaidi ya mwezi na sioni faida yoyote zaid ya kuwalipa wafanyakazi wangu kwa kipato changu kidogo ambacho ninakipata kwenye kaajira kangu kwa mhindi. Naombeni mnisaidie yafuatayo;
  1. Nifanyaje ili niweke kuvutia wateja zaidi bila kutumia kiasi kikubwa cha fedha?
  2. Nifanyaje ili niweze kupata faida kubwa, yani kuwa na matumizi kidogo na mauzo mengi?
  3. Nifanyeje ili kuwabana wafanyakzi wngu waisimamie biashara vizuri na kupata faida?
  NAOMBENI USHAURI WENU.

  ====================================
  MAJIBU KUHUSU BIASHARA HII
  ==============================================
   
 2. CHASHA FARMING

  CHASHA FARMING Verified User

  #2
  Jul 19, 2011
  Joined: Jun 4, 2011
  Messages: 6,133
  Likes Received: 2,117
  Trophy Points: 280
  mkuu biashara ya mgahawa inaendana na vitu vifuatavyo.
  -
  location
  -usafi
  -chakula
  - wahudumu
  - bei
  - unicness/ je kwenye mgahawa wako kuna kitu cha ziada

  1. Lazima kuwe na chakula chaenye ubora na si bora chakula
  2. Location yake lazima iwenzuri na ya kuingilika na wateja.
  3. Wahudumu lazima wawe na kauri nzuri na lazima wawe wasafi mda wote
  4. Hotel lazima iwe safi time zote na muda ambao wateja unakuta wamepungua au kukata wanapitisha dekio ili kuweka mazingira ya usafi

  kuhusu kuto pata faida labda nikujibu ifuatavyo.
  1.
  inategemeana na bei ya msosi wako. Je umeweka bei ya kuvutia tu wateja bila kuajali kama kuna profiti?
  2 au umeweka bei ya juu kiasi kwamba wateja wanashindwa kuingia?
  angalia bei yako kama ina meet cost na kutengeneza profit kidogo
  3.
  hao wahudumu wako je niwaminifu kiasi gani? Je ni ndugu zako wa karibu sana? But kwenye pesa hakuna cha undugu hata mke wako anaweza kuchakachua tu.

  - jaribu kuspend siku nzima pale na ucheki wateja wanao ingia ni kiasi gani na pesa inayo patikana ni kiasi gani.
  - then hapo utaweza fanya analysisi ya kujua kama huwa wanakuibia au
  nb: Biashara ya hotel ni moja ya biashara ambazo kwa kweli huwa hazina hasara kubwa na ni moja ya business ambazo huwa zinatengeneza profit kwa haraka sana ukilinganisha na biashara za duka
   
 3. u

  ureni JF-Expert Member

  #3
  Jul 19, 2011
  Joined: Jun 14, 2011
  Messages: 1,272
  Likes Received: 230
  Trophy Points: 160
  Hongera mkuu biashara ya hoteli na chakula inalipa sana manake mtu yeyote lazima ale na ashibe kwa hiyo sio biashara ya kukuingiza hasara.Sasa ushauri fanya hivii chukua likizo huko kazini kwako siku 30,nenda kasimamie mwenyewe kwenye hizo siku hakikisha unaweka hesabu vizuri kama chips agalia guia la viazi umenunua kwa kiasi gani umeliuza kwa mda gani umepata faida ya kiasi gani na unapata faida ya kiasi gani hapo utaweza kuielewa vizuri biashara yako kuna viti vingi vya kujua,kama usafi,lugha wanayotumia watu wako huo,pia unasikiliza mawazo ya wateja kwa kweli wateja huaga wana bonge ya mawazo ambayo ni ya manufaa sana
   
 4. M

  Malila JF-Expert Member

  #4
  Jul 19, 2011
  Joined: Dec 22, 2007
  Messages: 4,410
  Likes Received: 733
  Trophy Points: 280
  Mimi si mfanyabiashara,lakini najua kitu kimoja kuwa biashara ni kununua na sio kuuza. Mchango wangu ni huu, je bidhaa za mgahawani kwako unanunua wapi na nani ananunua? Je bei za bidha hizo umejaribu kulinganisha na masoko mengine? Jaribu kufanya zoezi hili uone.
   
 5. Husninyo

  Husninyo JF-Expert Member

  #5
  Jul 20, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 23,814
  Likes Received: 583
  Trophy Points: 280
  Pamoja na yote waliyoongea wachangiaji waliotangulia, hakikisha chakula kinachopikwa ni kizuri kwa maana ya taste.
  Jaribu kuangalia aina ya wateja ulionao na upange bei kuzingatia vipato vyao.
  Unaweza kutenga sehemu mbili, moja ikawa na special foods ukaset price yake na sehemu nyingine ikawa na vyakula vya kawaida na bei yake.
  Pata muda ukusanye maoni ya wateja na wape trainning ya customer care hao wahudumu wako.
  NB: biashara nyingi mwanzo huwa ni ngumu na huna budi kukubali hasara.
   
 6. Dr wa ukweli

  Dr wa ukweli JF-Expert Member

  #6
  Jul 20, 2011
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 892
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 45
  1. usisahau kulips kodi TRA, na nyinginezo.
  2. BIASHARA KAULI hao wahudumu kama hawajui kuuza maneno walah mtume huuzi!
  3. knye biashara kuna ushirikina sana (i) utafute kimzizi pemba, bagamoyo, sumbawanga, nk kikusaidie kuvuta wateja
  AU( ii)MAOMBI OMBEA BIASHARA YAKO ITAFANIKIWA.

  NB: HAPA MJINI CHUMA ULETE NI NYINGI SANA ZINGATIA NO 3 (ii)
   
 7. Kingdom_man

  Kingdom_man JF-Expert Member

  #7
  Jul 21, 2011
  Joined: May 19, 2010
  Messages: 456
  Likes Received: 285
  Trophy Points: 80
  useful contribution. Excellent!!!
   
 8. kanyagio

  kanyagio JF-Expert Member

  #8
  Jul 21, 2011
  Joined: Dec 10, 2009
  Messages: 986
  Likes Received: 40
  Trophy Points: 45
  malila hebu eleza zaidi hapo kwenye RED
   
 9. r

  rakeyescarl JF-Expert Member

  #9
  Jul 21, 2011
  Joined: Dec 9, 2007
  Messages: 408
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Mkuu nimependa hapo kwenye blue-I salute you-JF ,KUNA VICHWA VYA MAANA KWELI HUMU!,sikulijua hili![QUOTE=Malila;2249518]Mimi si mfanyabiashara,lakini najua kitu kimoja kuwa biashara ni kununua na sio kuuza. Mchango wangu ni huu, je bidhaa za mgahawani kwako unanunua wapi na nani ananunua? Je bei za bidha hizo umejaribu kulinganisha na masoko mengine? Jaribu kufanya zoezi hili uone.[/QUOTE]
   
 10. jebs2002

  jebs2002 JF-Expert Member

  #10
  Jul 21, 2011
  Joined: Sep 3, 2008
  Messages: 4,328
  Likes Received: 2,387
  Trophy Points: 280
  Kama alivyoshauri jamaa mmoja hapo chiini au juu.
  Inabidi uchukue likizo kama yamiezi 2, hatakama sio ya malipo.
  Simamia mwenyewe kuanzia unaponunua sukari, chumvi mpaka vyakula na vyombo vya hapo mgahawani.
  Hapo utajua kuwa hio boashara inalipa au hailipi, na kama inalipa basi kwa siku ni kiasi gani, na ni chai ya namna gani wateja wanaipenda au chakula gani cha mchana au siku wateja ndio wanunua sana.
  Kuanzisha biashara ni bomba ila unatakiwa ujue hio business inaingiza roughly kiasi gani kwa siku, hapo itakua rahisi kuwabana wasimamizi kama kuna short.
   
 11. Ghost

  Ghost JF-Expert Member

  #11
  Jul 21, 2011
  Joined: Apr 20, 2010
  Messages: 429
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  very useful thread(s)
   
 12. Mark Francis

  Mark Francis Verified User

  #12
  Jul 22, 2011
  Joined: Nov 19, 2010
  Messages: 605
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Nashukuru sana kwa michango yenu ya mawazo, naahidi kuifanyia kazi na ntawapa feedback baada ya miezi kadhaa ndani ya jukwaa hili.
   
 13. Mbogela

  Mbogela JF-Expert Member

  #13
  Jul 23, 2011
  Joined: Jan 28, 2008
  Messages: 1,369
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 145
  [/QUOTE]hiyo cocept kailezea vizuri robert kiyosaki ktk poo dad, rich dad 2, the cashflow quadrant. Napendekeza ukisome
   
 14. abusaadalbusaid

  abusaadalbusaid Member

  #14
  Jul 23, 2011
  Joined: Mar 4, 2011
  Messages: 13
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Ndugu unatakiwa ugeuze baadhi ya vyakula na vinywaji au uongozee baadhi yake ili upate wateja zaidi na pia ni uzuri kutizama migahawa ilioko kabli yako wanatumia mbinu gani ili kupasi kuchukuwa ujuzi wao ila pia pengine sehemu wenyewe inawezekana kuwa si ya kuvutia kabisa kwa hivyo ndugu nakushauri ufanye mabadilisho ili uweze kuendelea na biashara yako
   
 15. Mshume Kiyate

  Mshume Kiyate JF-Expert Member

  #15
  Jul 23, 2011
  Joined: Feb 27, 2011
  Messages: 6,774
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Sema maeneo tuweze kukusaidia vizuri! Kuna maeneo mengine yanaitaji vyakula vizuri, maeneo mengine yanaitaji matangazo, maeneo mengine kuna aina ya vyakula wanavyopenda
   
 16. M

  Malila JF-Expert Member

  #16
  Jul 23, 2011
  Joined: Dec 22, 2007
  Messages: 4,410
  Likes Received: 733
  Trophy Points: 280
  Tunaposema biashara ni kununua sio kuuza,tuna maana kuwa bei ya soko inajulikana kwa hiyo ni lazima upate faida kabla hujauza bidhaa zako kwa kununua kwa bei nzuri/chini kiasi toka ktk chanzo(supplier mzuri).

  Mfano, Kilo moja ya mchele ni Tsh 1600/ soko la Kariakoo na mchele huo huo ni Tsh 1350/ pale Tandika na wewe mgahawa wako uko Buguruni, yaani nauli ya daladala ni sawa. Tayari huyu wa Tandika ameshaokoa Tsh 250/ kwa kila kilo atakayo nunua. Kwa hiyo mkija Buguruni ktk migahawa yenu,mnaanza kutafuta faida kwa kuuza wali ktk soko kwa bei moja,mwenzio ana Tsh 250/ aliyoiokoa ktk manunuzi na wewe una Tsh 0/. Kwa hiyo utaona huyu wa Kariakoo lazima apunguze kipimo cha sahani moja au aongeze ufundi ktk mapishi, sasa huyu wa pili anachofanya ni kuongeza ukubwa wa kipimo cha sahani kidogo na anaimarisha mapishi, ni lazima apate wateja wengi kila siku bila kulaza chakula, mwisho anapata muda wa kutosha kufanya maandalizi ya kesho na kupumzika, kufanya usafi wa eneo lake la biashara nk.

  Siku moja nenda Kitunda/Kivule/Majohe asubuhi sana uone vijana wa mjini wanachofanya?
   
 17. sajosojo

  sajosojo JF-Expert Member

  #17
  Oct 16, 2012
  Joined: Apr 14, 2010
  Messages: 815
  Likes Received: 113
  Trophy Points: 60
  Helo wadau naomba ushauri wenu niko hapa dar nina kama mil 1 nataka kufungua biashara ya mama lishe,nimwajili mtu wa kupika,je itanilipa?
   
 18. Mgombezi

  Mgombezi JF-Expert Member

  #18
  Oct 16, 2012
  Joined: Mar 23, 2009
  Messages: 630
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Nimekuwa nikiwashauri wajasiriamali wengi kwamba furaha yako katika biashara isiwe katika fedha/faida unazopata; lazima kuwe ni jambo la zaidi linalokusukuma kuanzisha biashara. Fursa yeyote ya biashara hutokana na uhitaji wa huduma/bidhaa katika eneo husika, hivyo basi biashara yako inapaswa kulenga au kufikia zaidi jamii inayokuzunguka kulinga na uhitaji wao. Kila biashara inalipa, bali hutegemeana na uhitaji uliopo katika eneo husika, ikiwa umeona uhitaji wa kuwepo kwa huduma hiyo katika eneo husika basi utapata faida tu; bali kama huduma hiyo inapatikana katika eneo husika na unahitaji kuongeza ushindani tu, inabidi ujipange vizuri.
   
 19. E

  ESAM JF-Expert Member

  #19
  Oct 16, 2012
  Joined: Mar 15, 2011
  Messages: 962
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 45
  Songa mbele na kazi maana biashara ya chakula lazima watu wale tu. Ila kama alivyoshauri Mgombezi angalia uhitaji wa huduma katika eneo husika au soko la bidhaa yako. Lakini pia kumbuka suala la chakula lazima liambatane na usafi wa hali ya juu, yaani mazingira pamoja na vifaa utakavyotumia. Pia usisahau kumwomba Mungu akusaidie na kuibariki biashara yako, ila fungu la KUMI umtolee usimwibie. Baada ya hapo mafanikio ni lazima tu.
   
 20. Autorun

  Autorun JF-Expert Member

  #20
  Oct 16, 2012
  Joined: Mar 21, 2008
  Messages: 556
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Biashara hyo nzuri mtaji ulionao usikupe hofu ili uweze kucompete vizur biashara hyo inahitaji mambo kadha yawe sawasawa.
  1. Usafi unahitajika wa hali ya juu( mazingira ya mgahawa,wahudumu, vyombo,na upishi)
  2. Kauli nzuri
  3. Ubunifu katika upishi
  4. Weka huduma za ziada
   
Loading...