Nataka kufungua biashara ya kiwanda cha maji ya chupa, naomba ushauri wana JF | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nataka kufungua biashara ya kiwanda cha maji ya chupa, naomba ushauri wana JF

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by wanan, Aug 11, 2011.

 1. w

  wanan Senior Member

  #1
  Aug 11, 2011
  Joined: May 11, 2011
  Messages: 143
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 45
  Napenda kuwashirikisha ndg zangu juu ya mpango wangu wa kufungua kiwanda cha maji ya kunywa.nataka kufahamu juu mahitaji ya na vifaa muhimu kwa wale wote amabao wanafahamu najuu ya soko.kuhusu mtaji ninao wakutosha kabisa wadau ondoeni shaka.najuwa kwa njia moja au nyingine kutakuwa naajira kama nitafanikiwa kufungua na nafsi nitazitangaza hapa jf.Wadau mniambie mahitaji yote mhm na wapi naweza pata.Natanguliza shukuran za dhati kwa wot wanaJF.

  MFUNGO MWEMA NA MCHANA MWEMA KWA SIO FUNGU MUNGU WATIE NGUVU KWA KILA JAMBO
   
 2. M

  Malila JF-Expert Member

  #2
  Aug 11, 2011
  Joined: Dec 22, 2007
  Messages: 4,410
  Likes Received: 733
  Trophy Points: 280
  Inabidi ufanye utafiti mkubwa ktk mambo mawili, chanzo cha maji yako na soko la kuanzia. Juzi nilikuwa Iringa mjini,nikapewa maji ya Ndanda Lindi wakati kuna maji ya Africa na haya mapya ya pale Ilula, sasa ukiwa na chanzo cha maji kinachohitaji gharama kubwa ktk kuyasafisha(filtration process cost) maji lazima utapata taabu ktk soko.

  Pili inabidi uwe mjanja ktk survey ya soko,mwanzo ilikuwa rahisi,unakwenda ktk mji wo wote mikoani na unaanzisha plant na wenyeji wa mkoa huo wanakuwa ndio wateja wako wa mwanzo,mambo yamebadilika sana,kama nilivyo kuonyesha maji ya Ndanda yanauzwa Iringa mjini ambako kuna viwanda viwili vya maji.

  Usiogope wingi wa viwanda, panga mikakati kwa kuingia na bidhaa zenye ubora.
   
 3. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #3
  Aug 13, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Isiwe tu kupania kuanza mradi wa maji ya kunywa kwani biashara hiyo imeshamiri sana siku hizi. Angalia kwanza ubora wa bidhaa yako. Jaribu kufanya kwanza survey ya vijito vinavyotoa maji safi, bora na yenye ladha nzuri, ukifanikiwa hilo utawapiga kikumbo wale wanatumia gharama kubwa kuprocess maji hadi yapokeleke kwa matumizi ya kunywa.

  Pili jaribu kuwaona wengine wenye viwanda kama hivyo ili kupata ushauri mzuri na wa kufaa ili uwezeje kuboresha biashara yako. Si wafanya biashara wote wenye moyo mkunjufu, ila kuna wachache waso na kinyongo watakupa ushauri wa kufaa sana.

  Binafsi ningekushauri kitu kingine tofauti kidogo, kama kutengeneza juice na kuipake kwenye chupa na kuziuza, maana wengi wamechoshwa na vinywaji vya coca na pepsi ununuzi wa kubadilisha chupa. Siku hizi watu wanataka uhuru na mali anayonunua na hata kama unasafiri huhitaji kutembea na chupa za ziada kwa ajili ya kununulia soda au bia.
   
 4. serio

  serio JF-Expert Member

  #4
  Mar 15, 2015
  Joined: Apr 15, 2011
  Messages: 5,925
  Likes Received: 1,133
  Trophy Points: 280
  Kiongozi, tunaomba mrejesho...
   
 5. Mtanganyika

  Mtanganyika JF-Expert Member

  #5
  Mar 16, 2015
  Joined: Jul 18, 2007
  Messages: 1,613
  Likes Received: 280
  Trophy Points: 180
  Biashara hii ipo vizuri, kwanza kabisa usiogope swala la kwamba kuna maji mengi. Ni kweli maji yapo mengi lakini ukiangalia data bado watanzania wengi wanakunywa maji ya kuchemsha, mbili maji mengi faida ni 60% sababu maji is free commodity. Cha kwanza kabisa kabla ya kujua utatoa wapi maji, weka business plan yako chini kisha tafuta mtu mwenye uwezo wa kusoma na kuelewa business plan muombe aitoe makosa, afanyie smell test kuona kama ina pass.

  Kwenye proposal yako jambo kubwa sana ni sales literature na distribution plan. Ukiweza kutuliza kichwa na kutoa product yenye good quality na competitive price na ukatengeneza sales plan ya ukweli, nakupa less than 5 years lazima utakuwa na at least 5-10% market share kwa Tanzania. Kikubwa hapa ni jinsi utakavyo fanya branding ili uwe tofauti na wengine wote. Mfano, nimewaza kipindi fulani kutengeneza high end bottle water kama parrier au Voss ambapo lazima designing ya chupa iwe juu sana na quality ya maji yawe na PH ya world standard. Lakini hii lazima uwe na pesa ya kutosha kufanya advertisement sababu ya watu unao walenga. Au unaweza tengeneza maji ya nyumbani 20 liter, ukawa una supply majumbani na kugawa water dispenser free kwa mtu anasign mkataba wa kupata maji kutoka kwako for 2 years na ordering at least once a month. Believe me dispenser haina gharama yoyote compare na revenue guarantee.

  Tuje kwenye production yenyewe, kwanza inategemea vyanzo vya maji. Kama unataka kufanya reverse osmosis haijalishi maji unayatoa wapi. Vifaa vya kuanzia kuchonga chupa (mold) mpaka equipment za kuchuja maji, kujaza kemikali na kuyaweka kwenye chupa jumla yake ni USD 50,000. Hiyo ni china. Kama upo interest zaidi ni inbox nitakupa direct contacts za watu wanaouza. Na kama unataka niangalie proposal yako ukisha andika nicheki pia.
   
 6. Steven Sambali

  Steven Sambali Verified User

  #6
  Mar 16, 2015
  Joined: Jul 31, 2008
  Messages: 314
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 45
 7. serio

  serio JF-Expert Member

  #7
  Mar 16, 2015
  Joined: Apr 15, 2011
  Messages: 5,925
  Likes Received: 1,133
  Trophy Points: 280
  I have saved this...
  If all people were as direct as you have been, tungekuwa mbali sana. Ubarikiwe boss
   
 8. serio

  serio JF-Expert Member

  #8
  Jul 17, 2017
  Joined: Apr 15, 2011
  Messages: 5,925
  Likes Received: 1,133
  Trophy Points: 280
  Still no progress on this thread?
   
 9. Nichumu Nibebike

  Nichumu Nibebike JF-Expert Member

  #9
  Jul 17, 2017
  Joined: Aug 28, 2016
  Messages: 6,261
  Likes Received: 10,046
  Trophy Points: 280
  Una mtaji wa sh ngapi?
   
 10. Extrovert

  Extrovert JF-Expert Member

  #10
  Jul 17, 2017
  Joined: Feb 29, 2016
  Messages: 5,385
  Likes Received: 5,590
  Trophy Points: 280
  Maji yanahitaji mtaji mkubwa sana ila ni biashara isio na stress sana kutokana na kuwa maji ni convenient product. Utauza tu!!!
   
Loading...