MLIPAKODI
JF-Expert Member
- Dec 11, 2012
- 234
- 88
Wadau,
Nahitaji kulima maparachichi. Kwa mwenye ufahamu zaidi naomba kujua changamoto na nini nifanyeje ili nieweze kufanikiwa.
MASWALI YA WADAU WENGINE KUHUSU ZAO HILI
Kama kuna mtaalamu wa kilimo naomba msaada kwa maeneo ya huku Katavi - Inyonga. Nimepanda miche ya parachichi nataka kuwekeza. Je, kwa eneo letu huku ninaweza kupata matokeo chanya?
Wakuu kilimo cha parachichi aina ya hass kwa sasa kinachukua umaarufu hasa kwa mikoa ya Mbeya, Njombe, Iringa, Arusha, Songea na kwingineko.
Mwenye kujua masoko yake hasa nje ya nchi na makampuni yanayonunua tujuzane please.
Kilimo cha maparachichi ni moja ya miradi bora wilaya ya Rungwe na sehemu zingine, wadau naomba kujua umbali unaofaa kati ya mche na mche.
Sent using Jamii Forums mobile app
MICHANGO/ UZOEFU WA WADAU KUHUSU ZAO HILI
Agronomy ya Parachichi
Hali ya hewa
-Ni tunda linalopenda sana sehemu za baridi, maeneo kama ya Rungwe-Mbeya, Njombe, Makete, linastawi vizuri sana, na huwa na Fatty Contenty kubwa
Joto
Nyuzi 15-25 Sentigrade
Muinuko
Mita 1200-1800 kutoka usawa wa baridi
Udongo
-Uwe kichanga tifutifu (Sandy loam), usiotuamisha maji
Aina za Parachichi
1. Zipo aina za kiasili. Kila sehemu kuna iana za parachichi ambazo ni za asili ya eneo husika, parchichi hizi, huwa ndefu sana, na mavuno machache
2. Zipo aina za kisasa (Chotara)
Ziko aina nyingi sana za Parachichi chotara, na hizi hapa chini ni baadhi ya zile maarufu hapa tanzania
i. Hass
-Hii ni aina maarufu sana katika aina za parachichi
View attachment 332265
- Ni tunda linalokuwa na vipere vipere
-Limechongoka juu na chini
-Linahifadhika kwa urahisi
ii. Aina ya pili ni Fuerte
View attachment 332266
-Hili ni aina ya parachichi lenye ngozi laini saini, ngozi yake inateleza kama imepakwa mafuta
-liko na mafuta mengi ila linawahi kuoza
-Ni zuri kwa matumizi ya kawaida , si kwa kusafirisha umbali mrefu
-Aina hii ikilimwa sehemu za miinuko na baridi sana, inafaa sana kutoa mafuta mengi yanayoweza kutumika kutengeza lotion na baadhi ya vyakula vya mifugo
iii. Aina ya tatu maarufu hapa tanzania -inaitwa X-ikulu
-Ana hii ni maarufu sana kwa mikoa ya nyanda za juu kusini (Mikoa ya Njombe, Iringa, Mbeya na Ruvuma)
-Mti wa aina hii huwa na majani mapana kama mti wa embe
-Mti huu huchukua muda mrefu sana kustawi
-Tunda lake huwa ni kubwa, na lina gharama sana
Upandaji wa Parachichi
Nafasi kati ya shimo na shimo
-Umbali wa kutoka shimo hadi shimo ni MITA 7
-UMbali wa kutoka mstari hadi mstari ni MITA 7
Lakini kipimo hicho hapo juu kitategemea sana na aina ya udongo wa shamba lako , kwa udongo wenye Phosphorus kwa wingi (P), kipimo hicho hakifai, maana baada ya mika 3-5 miche ya mistari miwili inayofuatana itakuwa imekuatana katikati
-Hivyo nafasi yaweza kuwa
8M X 8M-KWA NAFASI HII UTAKUWA NA MICHE 63 KWA EKA 1
AU 9M X 9M-KWA NAFASI HII UTAKUWA NA MICHE 49 KWA EKA 1
AU 10M X 10M- KWA NAFASI HII UTAKUWA NA MICHE 40 KWA EKA 1
Ukubwa wa shimo-Shimo laweza kuwa futi 2.5 x futi2.5 x futi 2.5 = (sm 75 x sm 75 x sm 75) (Kimo x upana x urefu)
-Au kipimo cha futi 3 x futi 3 x futi 3= sm 90 x sm 90 x sm 90
Mbolea
-Mbolea za kupandia zitakazohitajika , ni moja wapo kati ya hizi
-Samadi, Mboji, DAP, au TSP-Lakini ni muhimu kupandia mbolea asilia kama samadi ukachanganya kidogo na TSP au DAP
Kipimo cha mbolea,
-Kama ni mbolea za asili (Samadi au Mboji)-Kiasi cha kilo 16 hadi 20 kinapaswa kiwekwe katika shimo miezi 3 kabla ya kupanda mche
-Kama utapandia mbolea za viwandani (TSP, DAP, Minjingu, NPK etc)
kiasi cha gramu 100 hadi 200 kiwekwe kwa kila shimo, ichanganywe vizuri na udongo, kisha mmea uwekwe na kumwagiliwa
KUKOMAA NA KUTOA MAVUNO
-Parachichi hasa hizi za kisasa, hukomaa baada ya miezi 18 hadi 24
MAVUNO
-Kwa mara ya kwanza mti mmoja wa parachichi unaweza kukupa kati ya matunda 50 hadi 100 kwa mche mmoja.
-Mavuno hueongezeka kadri umri unavyoongezeka
-Mti wa parachichi ukifikia umri wa miaka 4 hadi 5, unakuwa full maturity, na hivyo mti mmoja unaweza kukupa hadi matunda 1200 kwa mwaka mzima '
FAIDA
kwa kipimo cha mita 10 x mita 10, katika eka mmoja utakuwa na mita 40
-Kila mti baada ya mika 5 unaweza kukupa wastani wa matunda 1000
-Hivyo kwa miti 40, utakuw na jumla ya matunda 40 x 1000= 40,000
-Kila tunda kwa bei ya shambani uuze tsh 250, na unamatunda 40,000
-Hivyo utapata jumla ya tsh 250 x matunda 40,000= 10,000,000tsh (MILIONI 10)
Magonjwa ya parachichi
Parcahichi kama mimea mingine inashambuliwa sana hasa upande wa majani pamoja na matunda.
1. Yapo magonjwa ya majani, yanayosababishwa na fangasi/Ukungu, Algae, pamoja na wadudu, pamoja na lishe duni.
View attachment 332289
Jani lililoshambuliwa na Alga
View attachment 332290
Mite-Utitiri mweupe Avocado lililoshambuliwa na Utitiri
2.Magonjwa ya matunda
View attachment 332291 View attachment 332291
View attachment 332292
-Tatizo la Scab, husababishwa na Ukungu/Fangasi hasa wakati wa baridi/unyevu mwingi
View attachment 332293
Thrips wa avocado Matunda yaliyoathiriwa na Thrips
DAWA
-Dawa za kutibu wadudu kama Karate, Matchi, Actellic 50 EC, za faa sana kumaliza wadudu katika mmea wa parachichi
-Dawa za Ukungu kama Ridomil Gold, Ebony 72 WP (Mancozeb na Metalaxyn), Ivory, na Nordox zaweza kutumika kumaliza matatizo ya ukungu
-Lishe ya mmea
Mbolea za kukuzia kama CAN, UREA NA SA (hasa kwenye maeneo yenye magadi kwa wingi, na chumvi nyingi) yaweza kutumika kubalane PH YA Udongo.
-Booster=Mbolea za majani, maua na matunda kama vile Polyfeed Starter, Polyfeed finisher, Wauxal macro mix, Potphos, au Multi K , Ni muhimu sana zikatumika wakati wa maua, na matunda ili kuzuia matunda ya parachichi kuabort (Fruit abortion) yakiwa machanga, pamoja na kuzuia matunda kudondoka yakiwa machanga.
Hitimisho
Parachichi-Kama matunda mengine, ukililima kitaalamu, na ukaweka juhudi na maarifa linakutoa katika umaskini
Hass na X-Kulu ndizo zinakubalika kwa ubora na wingi wa mazao
Parachichi hupendelea sehemu zenye barid na unyevunyevu. Bila shaka Iringa nzima ina hali hyo. Ila ni vizuri ukipima udongo wako ili kujihakikishia kiwango cha rutuba katika shamba lako.
Idadi ya miche ni kuanzia miche 60 mpaka 100 kwa ekari moja.
Kuhusu mbegu nzuri inategemea na target ya soko lako. Ila kwa ujumla parachichi za kisasa kama Hass na X-Kulu ndizo zinakubalika kwa ubora na uwingi wa mazao.
Hass ndo parachichi tamu zaidi lenye soko la nje
Panda mbegu moja inaitwa Hass. Kwanza ndo parachichi tamu zaidi likiiva na yanapelekwa hadi masoko ya nje, kama unafanyia Moshi nenda Usa River Arusha, kuna chama kinaitwa TAHA. Ukiweza waGoogle watakupatia mbegu idadi yeyote utakayo; hata miche na unapewa bure yakiiva wanakutafutia na soko wao wanakukata asilimia 10% ya malipo yako, hawana wizi wala konakona wateja wanao tayari.
Parachichi zinalipa sana ila kabla hujafanya chochote jifunze mengi ndio uamue kama uwekeze au la
Mbegu bora ni HASS ni nzuri kwa maana kiwango cha mafuta, palatability na shlev life yake ni kubwa sana
Kama unalima Moshi Hakikisha hali ya hewa ya mahalia haizidi 30 nyuzi joto hali ya udongo usiotuamisha maji.
Mbegu zinapatikana hapo SIHA kwenye shamba la Africado, bei maelewano.
Uzalishaji: Kulingana na utaalamu ekari moja ni miche kat ya 40 - 106. hii inategemea unataka kuleaji miti yako, kama utaicha iwe bush 40 ni sahihi. kama unauwezo wa kulea vizuri bila kuiacha iwe miti mikubwa 72 - 106. ukienda siha utaona mashamba ni aina mbalimbali za upandaji.
Kuhusu mavuno: Mti mmoja unaweza kutoa hadi 200kg (export quality fruit) kama umelenga masoko mengine unaweza kupata hadi 400kg kwa mti wenye miaka 6 na kuendelea. mavuno yanaanza mwaka wa nne.
Bei ya maparachichi kwa msimu huu imesimama 1450/kg kwa yale yanayosarishwa nje. Kumbuka kuna size 12,14,16, 18, 20, 24, 26 kwa lugha nyepesi hiyo idadi intakiwa ifike 4kg
Parachichi zinalipa sana ila kabla hujafanya chochote nenda kawatembelee Africado na wakulima, ama nenda Njombe kawatembelee wakulima na Mnununuzi Korongo 3 au nenda Rungwe uonane na wakulima kupitia umoja wao UWAMARU, ongea nao kisha wanuunuzi KUZA Africa, Rungwe Avocado, Korongo 3, Biofarm/Biofresh usikie na upate mengi ndio uamue kama uwekeze au la.
Mikoa ya Nyanda za Juu Kusini wanaita parachichi Green Gold (Dhahabu ya Kijani)
Kusini hili zao huitwa green gold, wengi wametoka.
So far kuna mpaka viwanda vya usindikaji MBozi na NJombe vimeanza kujengwa. Ukipanda hass which mature at the age of 2.5 to 3 years, mti mmoja hutoa matunda 300 kwa mwaka mpaka 500. UKiwa na miti 70 kwa eka manake una matunda 21,000 sawa na 7000kg. Assume kilo moja ni 1500tshs (bei ya leo Njombe iyo) kwa eka unapata 10.5mil ukiwa na eka kumi sawa na 105mil kwa mwaka ambayo kwa mwezi ni sawa na mapato ya 8.7mil (mshahara wa mkurugenzi huo tena gross nadhani ikija take home lazima alambe 5mil)
Just assume mwaka mbaya ukapata just nusu ya iyo 105mil maisha yanasonga huna haja ya kuajiliwa ni kutafuta mtaji panda parachichi.
Mambo iko uku wahi mashamba Moshi Mbeya na NJombe kuwa na better future yako na ya wanao
Wananunuzi wanakuja nyumbani kwako kununua hata kama una mti mmoja
Mbeya, Njombe wananunuzi wanakuja nyumbani kwako kununua hata kama una mti mmoja. Kampuni ya Rungwe wao ndio kidogo wanamasharti hasa ya usafi, mti usiwe karibu na jalala au choo. Hata hivyo soko la ndani ni kubwa sana maana hatuna mahekta ya parachichi panda tu parachichi isitoshe wakenya ndio huja nyanda za juu kununua hivyo Arusha ni karibu kabisa na wakenya unaweza tafuta connection.
Wakenya wenzetu wana export to UK. Jambo lingine ni kwamba Parachichi za Tanzania zinaenda msimu tofauti na ulaya hata tulime ardhi ya mikoa yote inayostawi parachichi hatutoshelezi soko la dunia. Mikoa inayastawi parachichi ni Mbeya, Njombe, Arusha Kilimanjaro, Kgera na Kigoma. Kila sehemu inayostawi kahawa na chai parachichi itakubali.
Parachichi inayofanya vyema ni Hass sokoni na inayofanya vyema zaidi ni inayokomaa mwezi November hadi March. Kipindi hiki wazalishaji wakubwa wanakuwa hawana mzigo. Mzalishaji anaechelewa ni Israel yeye anaishiwa mzigo mwezi January.
Hivy ukiwa ukanda wa Busokelo na lupembe maeneo ya Mfriga, Madeke, Mfriga, Iduli , ikondo una uhakika wa kukutana na soko la ukahakika.
Uzoefu unaonyesha parachichi mwaka wa tatu utakupatia matunda 40 had 60 ambapo utapata kilo 10 hadi 15.
Kingine cha kuzingatia mbegu bora ya parachichi inatakiwa itokane na kikonyo cha mti ambao ni kizazi kisichozidi cha nne, hapa utapata size na shape nzuri ya Hass. Kununua mche ambao kikonyo kimetoka kizazi cha mbali ni hasara kwako matunda yataanza kutoa yasio na shape halis ya hass.
China wanahitaji mamilioni ya tani za parachichi kwa mwaka
China wanahitaji mamilioni ya tani za parachichi kwa mwaka (umesikia avocado deal waliyosaini Kenya na China)
Hapa ndio utaona uzuri wa kilimo cha matunda ya muda mrefu. Mti wa parachichi unadumu na kuvuna miaka 40+ kwahiyo hata uchumi ukiyumba miaka 7 mfululizo utavuna nakuuza kwa bei nzuri miaka ijayo. Tofauti sana na mazao ya muda mfupi kama mahindi, maharage, spices like ginger etc.
Uchumi hata ukiyumba upande wa chakula hii ni basic human need, research nyingi zina-favor avocado kutokana na health benefits zake nakufanya iwe kilimo salama zaidi.
Watu kila kukicha wanazidi kutambua umuhimu wa matunda kwa afya zao.
Idadi ya watu inazidi kuongezeka na hivyo watumiaji wa agriproducts wanazidi kuongezeka.
Dalili njema ipo hata hapa Tanzania ambapo kila mkoa, wilaya mpaka kijijini bei ya parachichi vibandani/mezani kila mwaka ni 500 iwe masika, kiangazi tofauti na embe, chungwa, pear.
Iwapo utafuata masharti ya soko la nje na kufanya organic farming, utapeta hata uchumi uyumbe vipi.