Nataka kufanya biashara ya vinywaji, naomba msaada wa mawazo

BOFREE

JF-Expert Member
Mar 1, 2012
523
1,000
Wakuu nataka kufanya biashara ya vinywaji na kuuza jumla nina mtaji mdogo siwezi kuwa distributor kwa kufuata bidhaa kiwandani hivyo natafuta muuzaji wa kuniuzia jumla na mimi niweze kuuza jumla kwa mkoa wa Dar es salaam.

Au kama kuna mtu anafahamu sehemu au namna ya kununua kwa jumla kreti ishirini za vinywaji vya Cocacola na ishirini za vinywaji vya Pepsi.

Duka litakua na vinywaji vingine kama maji na nk
1622554641439.png

 

BOFREE

JF-Expert Member
Mar 1, 2012
523
1,000
Wakuu hawataki kutoa mchango kabisa namna ya kununua maji kwa jumla, soda kwa jumla, juice kwa jumla.
 

Lihove2

JF-Expert Member
Mar 23, 2018
2,422
2,000
Kuuza kwa jumla faida unajua ni shiling ngapi kwa carton /creti?

Ili uuze jumla upate faida ya kiwezesha kulipa pango ni vizuri uwe na mtaji mkubwa unaokuwezesha kununua kwenye yale magari yao siyo kwa mtu mwingine
 

Ugobha

JF-Expert Member
Jul 18, 2020
872
1,000
Usinunue kwa mtu bali ongea na wale wanaotembeza na magari utajua kiwango wanachoanza kuuza.

Au jaribu tafuta jirani anayechukua mzigo mkubwa kama itawezekana akuunganishie oda japo.

Chunguza vzri kuhusu bei huwa kuna upigaji
 

white wizard

JF-Expert Member
May 18, 2011
6,147
2,000
Wakuu nataka kufanya biashara ya vinywaji na kuuza jumla nina mtaji mdogo siwezi kuwa distributor kwa kufuata bidhaa kiwandani hivyo natafuta muuzaji wa kuniuzia jumla na mimi niweze kuuza jumla kwa mkoa wa Dar es salaam

Au kama kuna mtu anafahamu sehemu au namna ya kununua kwa jumla kreti ishirini za vinywaji vya Cocacola na ishirini za vinywaji vya Pepsi.

Duka litakua na vinywaji vingine kama maji na nk
Sasa mkuu hiyo biashara utaiweza kweli?, kwani creti moja ya soda faida yake ni kama tsh.500, nadhani kwenye gari unauziwa 9500, na wewe unatakiwa kuiuza 10, 000!!kuifanya biashara hii ni rahisi sana hasa ukiwa Dar, wewe watafute wale wenye magari ya pepsi/coca watakupa utaratibu wa kuwa wana kushushia kwani huwa wanasambaza mitaani.yaani carton moja ya maji faida ni kati ya 300-400!!
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom