Nataka kufanya biashara ya kuuza gesi

KiuyaJibu

JF-Expert Member
Aug 29, 2007
841
175
Nina rafiki yangu mmoja ambaye amebahatika kukutana na kuongea na bosi mmjo wa kampuni moja kubwa iliyojikita kwenye biashara ya mafuta na gesi; katika maongezi yao rafiki yangu alipendezwa na kufanya biashara ya kuuza gesi. Wakakubaliana kuwa anataka kufanya biashara ya kuuza gesi iliyoko kwenye mitungi kwaajili ya matumizi ya nyumbani nakadhalika.

Bosi huyo akamwambia tafuta mwenzio msajili kampuni mpate mahali pakuweka duka mimi nitawaleta mitungi ya gesi kwa bei ya jumla halafu baada ya kuuza mnanilipa fedha yangu inayobakia ni yenu; kwa maana hiyo, yule bosi anatoa mzigo depot mpaka duka lilipo bila kulipa hata shilingi moja.

Kabla sijakubali kuingia kwenye ubia wa biashara hiyo; naomba ushauri wenu kuhusu hii biashara kwasababu mimi ni mgeni.

Natanguliza shukrani zangu kwenu.
 
Ni biashara nzuri kama nyingine hasa unapopata eneo lenye uhitaji mkubwa lakini changamoto pia hazikosi mfano ukutane na competitors ambao ukiacha gas wanafanya biashara nyingine katika duka hilohilo hivyo nakushaur tafuta sehemu ambayo population ni kubwa na wauzaji wa hawapo au wapo wachache pia usitegemee biashara moja katika duka lako ni hivyo
 
Back
Top Bottom