Biashara ya Usafirishaji kwa Bajaji: Ueandeshaji, Changamoto, Faida na Ushauri

Asante sanaaaa!
7,000,000/= bei ya kununua
20,000= kipato kwa siku × siku 5 za wiki × mwaka
5,200,000/=
Ingiza mambo mengine kama services, vibali, bima nk.
Mwisho ndani ya miaka miwili ndo unarudisha hela uliyonunulia
Iuze ili ununue nyingine utaiuza kwa sh. zisizoidi
2.5 M.
 
Miradi ya vyombo vya moto ina changamoto sana. Fanya kama pesa ni ya kwako. Ila kama umekopa, ipo siku unaweza ukatembea na chupi kichwani!

Bado sijasahau nimelala, saa kumi alfajiri napigiwa simu niende kituoni, Hiace yangu niliyoinunua hata mwezi haujaisha imepata ajali.

Nilienda kimy kimya kituoni nikaichekii, nikapotea kama mwezi kwanza mambo yapoe poe. Nakwambia nilitoka nyumbani na ndala. Kituo cha dala dala nilikiona kiko mbali utadhani Dar na Chalinze.

Nikiangalia hata rejesho moja sijarudisha na chombo ndio kishakula mzinga!
Pole sana mkuu, hadi ukaona ujiite hivyo kwenye ID yako.
 
Used nzuri kuanzia million 4, utazipata mbeya na Dar.

Bajaji nzuri ni TVS king, hasa ukiipata ile toleo la zamani.

Kuhusu dereva tafuta kijana mwenye familia au nenda kwenye makanisa katangaze ajira au mskitini, hata kama wana mapungufu huwa yanakua machache.

Ukitaka upate faida kubwa kwa haraka endesha wewe mwenyewe.

Ukimpa kijana unamuwekea mafuta ya elfu 15,kwa siku anakuletea malengo 20000 kwa siku6.jumapili service sanasana ni kumwaga oil,kama kuna bulb zimeungua n.k.

Ukiitunza vizuri inaweza kukaa miaka mi4 hadi mi5.

Kama nyumba yako inafance mwambie dereva awe anailaza nyumbani kwako.

Ukitaka upate faida ya hii biashara uwe nazo kuanzia tatu.
 
Kama kweli una milion7 badaya ya kununua bajaji uingize 100k kwa wiki afu kwa mwezi 400 hadi 480 bado hujatoa services na emergency zingine ni bora utafute noah ata kana imechoka ya 6m-7m mradi injin nzima uweke njia za vijijin kwa siku 30-50 Inategemea na njia yenyewe kwa mwez una kuwa na uhakika wa 900 au 1.2m kabisa ukitoa service na mengineyo 800 700 hukosi hela unarudi chap chap sana ndan ya miez6 cha muhim ni kukomaa nayo tu ata kama itakuwa gari inaleta tatzo inajitibu yenyewe kwa hela ya faida
 
Umempa wazo
 
Asante sanaaaa!
Bajaji ya miaka miwili uuze 2.5M basi huyo dereva ni mharibifu sana anastahili tuzo lakini kwa dereva wa kawaida tu mwenye utunzaji kiasi bajaji ya miaka miwili bado mpya kabisa unauza hata 4M nakuendelea.
 
Mkuu nashukuru kwa ushauri, sasa nawezaje kutofautisha kati ya toleo la zaman na lasasa la TVs king?
Used nzuri kuanzia million 4,utazipata mbeya na dar..

Bajaji nzuri ni tvs king,hasa ukiipata ile toleo la zamani..

Kuhusu dereva tafuta kijana mwenye familia au nenda kwenye makanisa katangaze ajira au mskitini..jhata kama wana mapungufu huwa yanakua machache..

Ukitaka upate faida kubwa kwa haraka endesha wewe mwenyewe.

Ukimpa kijana unamuwekea mafuta ya elfu 15,kwa siku anakuletea malengo 20000 kwa siku6.jumapili service sanasana ni kumwaga oil,kama kuna bulb zimeungua n.k.

Ukiitunza vizuri inaweza kukaa miaka mi4 hadi mi5.

Kama nyumba yako inafance mwambie dereva awe anailaza nyumbani kwako.

Ukitaka upate faida ya hii biashara uwe nazo kuanzia tatu.,
 
Ka wengi walivyotangulia kusema bajaji ni nzuri ukiwa nayo na ukaijali mpya kwa upande wa TVS inagonga 7 200 000milion kwasasa, bajaji inaweza kukaa kati ya miaka 5-7 endapo itakuwa na matunzo mazuri na ikiwa kwenye njia nzuri,
mazingira ya vilima inamudu vizuri hesabu yake ni 20,000 per day ka ukimpa mtu, ila ka sehemu inabiashara nzuri hesabu inaweza badilika maana si sheria service unaweza piga baada ya week mbili na kubwa ni kumwaga oil na kubadilisha baadhi ya vifaa baadhi tu na ni vidogo, service inaweza isizidi 25,000 per two week, likijitokeza tatizo kubwa ka la injini ndo unatoboka ila service common ni kumwaga oil na kubadili raba ambavyo kwa vyote haviziti hiyo hela.

Kikubwa ni kuzingatia oil kumwaga na jitahidi kuweka oil nzuri si zile za kupima ukifanya hivyo itakuwa nzuri wakati mrefu zaidi.

Kila la heri katika biashara hiyo
 
Miradi ya vyombo vya moto ina changamoto sana. Fanya kama pesa ni ya kwako. Ila kama umekopa, ipo siku unaweza ukatembea na chupi kichwani!

Bado sijasahau nimelala, saa kumi alfajiri napigiwa simu niende kituoni, Hiace yangu niliyoinunua hata mwezi haujaisha imepata ajali.

Nilienda kimy kimya kituoni nikaichekii, nikapotea kama mwezi kwanza mambo yapoe poe. Nakwambia nilitoka nyumbani na ndala. Kituo cha dala dala nilikiona kiko mbali utadhani Dar na Chalinze.

Nikiangalia hata rejesho moja sijarudisha na chombo ndio kishakula mzinga!
Pole. Hukua umekatia bima comprehensive?
 
Back
Top Bottom