Nataka kuchangia fedha Jamii Forums

Nifanyeje ili kuwasilisha huo mchango?
Ofisi za Jamii Media (inayoratibu JamiiForums) zipo Dar es Salaam, unaweza kuwasiliana nasi kwa simu +255 222 843 510 (landline) au +255 713 444 649 (mobile) tukaufuata mchango popote ulipo ili kukupunguzia usumbufu. Lakini endapo utaona rahisi basi turahisishie nasi kwa kutumia njia hii iliyoelekezwa hapa:

JINSI YA KUICHANGIA JF

Mkuu wangu Sikonge,

Ukweli ni kuwa siku za nyuma tulijaribu sana kuwafahamisha members kuwa JF haiendeshwi kwa fedha za watu flani bali kwa kujitolea.

Tukatanabaisha wazi kuwa wanachama na wote wenye mapenzi mema inabidi watambue kuwa tuna mzigo mkubwa wa kubeba kwa niaba yao.

Nyakati hizo tulikuwa na wanachama waliojisajili karibia 2,000 hivi na tukasema endapo kila mwanachama (aliyejisajili) angechangia Tshs 10,000/= basi ilimaanisha kuwa tungepata Tshs 20,000,000/= ambayo kwa wakati huo ingetosheleza kuiendesha JF kwa karibia mwaka mzima bila wasiwasi.

Maisha yakabadilika, Server tuliyokuwa nayo ilikuwa ndogo sana kumbe kulinganisha na uhitaji wa watanzania, balaa lilionekana wazi Mwezi Februari pale Mhe. Lowassa alipokuwa akijieleza Bungeni... Server ikachemsha kubeba mzigo mkubwa.

Kwa wakati huo tukaona ni vema tukaangalia namna ya kuweza kuwashirikisha wanachama juu ya ugumu tunaokumbana nao... Tukalazimika kununua server kubwa zaidi mbili na zenye back up za kila baada ya masaa 6 kwa nyakati tofauti. Tukiwa na uwezo wa kufanya hosting hata BURE kwa website za watanzania.

Hilo likasaidia japo kwa gharama ambazo zilitoka mfukoni mwa mwanachama mmoja! Ndiyo, kulipia server hizo kila mwezi ni karibia $900 na ameendelea kufanya hivyo kwa imani kuwa kuna siku mambo yataenda sawa.

JF inahitaji SANA michango ya watanzania na wote wenye mapenzi mema.

Kuna wanachama ambao humu mnawaona wana usernames ambazo ni bolded, hawa ni Premium Members. Hawa walau wamechangia kwa kiwango cha kuanzia $5 na wawili walau $300 tangu JF inaanzishwa mwaka 2006 (ikijulikana kama JamboForums).

Tangu JF inaanza (2006) mpaka sasa Januari 9 2009, tumekwishapokea jumla ya US$ 1,450/= toka kwa wanachama waliojisajili na wasiojisajili.

Wengi wa waliohitaji kuchangia walikuwa wanatuma barua pepe nasi tunawapa maelekezo juu ya namna ya kutufikishia michango hiyo.

Ukweli ni kwamba kwa wasio wanachama wa JF wakiwa wanasoma hapa wanaona matangazo mengi ya Google kuliko wanachama waliojisajili.

Dhamira yetu si kuweka matangazo haya ya Google kwani hayaingizi kwa kiwango kikubwa hivyo, watu hawabonyezi matangazo hayo na hivyo income yake inategemea pale mtu atakapokosea akabonyeza tangazo ndipo tupate vijisenti kidogo kwa clicks hizo. Gharama za uendeshaji bado zinatoka mfukoni mwa mtu mmoja mpaka sasa na baadhi ya Premium Members ambao wameendelea kuona umuhimu wa kufanya hivyo.

Mpaka sasa JF ina wanachama waliojisajili karibia 8,000. Endapo waliojili hawa wangechangia walau Tshs 10,000/= kwa mwaka basi inamaanisha JF ingetengeneza Tshs 80,000,000/= kwa mwaka na hivyo tusingeweka matangazo KABISA na tungejitahidi kupata moderators ambao watakuwa wanalipwa kwa kazi yao na wangeifanya kwa umakini mkubwa zaidi.

Ukiangalia katika historia ya Forums nyingi, huwa zinashindwa kuhimili traffic inapokuwa kubwa kutokana na servers kuhitaji umakini zaidi na Forum owners hujikuta wanaona ni mzigo usio na faida hivyo forums hizo kufa.

Tumshukuru Maxence kwa kuendelea kulipia gharama hizi kila mwezi kwa kujitolea mpaka sasa huku akilipia na Chat Server (IRC Server).

Wapo wanachama kama Ogah, Nyambala, SteveD, FairPlayer, Mchukia Fisadi na Phillemon Mikael ambao huchangia walau kila wanapopata wasaa... Hawa nao wamesaidia kwa kiwango kikubwa katika jitihada za kuhakikisha JF inakuwa hewani. Bila kuwasahau wadau waliochangia walau $200 hivi initially kama Mtanzania, Field Marshal ES na Halisi.

Ninachoamini binafsi ni kitu kimoja, Tshs 5,000/= kwa mwaka inawezekana kabisa kwa watanzania tulio na uwezo wa kuingia mtandaoni. Na uzuri, benki zetu Tanzania zinaruhusu mtu ku-deposit Tshs 5,000/= kama kiwango cha chini.

Endapo kuna mwanachama anaguswa (kutoka moyoni) na angependa kuiwezesha JF kuendelea kusimama imara na kufanya vema zaidi bila mizengwe ya kifedha, basi anaweza kukubali kuchangia Tshs 5,000/= walau kwa mwaka.

Benki zetu (hapa naongelea NBC na CRDB kwa haraka) hazikulazimishi unayetuma hela kuandika jina lako la kweli bali lile ambalo ungependa mpokeaji alitambue.

Kwa walio Tanzania wanaweza kuichangia JF kwa kutuma katika akaunti za NBC au CRDB.

Akaunti ambazo tangu awali tulipendekeza zitumiwe ni za Maxence Melo (as the JF Founder) na tukawaomba wanaotuma waandike Nicks za kuweza kutanabaisha kuwa wao ndio walotuma.

Michango inaweza kutumwa kwa njia kuu nne:

Kwa walio nje wanaweza kutumia PayPal au Credit Cards au Debit Cards kwa kufuata link hii ( https://www.jamiiforums.com/payments.php) iliyo kwenye sahihi yangu (linapoonyesha dole gumba) na pindi mchangiaji anapoweka chochote tunakuwa notified nasi tunafanya kuwasiliana na mhusika ili aweze kupandishwa kwenda katika group la Premium Members.

Njia ya pili ni kutumia Western Union au Money Gram na kutuma kwenda kwa Maxence Melo wa Dar es Salaam.

Njia ya tatu ni kutumia Bank accounts za Maxence kama ifuatavyo:

NBC:

Acc #: 033201064359
Jina: Maxence Melo Mubyazi

CRDB:

Account Name: Maxence Melo Mubyazi
Bank: CRDB Pugu Road Branch
Swift Code: CORUTZTZ
Acc No: 01J2092391800

Njia ya nne ni kwa kutumia email ya macdemelo@gmail.com
kwenye hii link: https://www.payoneer.com/webapps/Load/LoadToPage.aspx

Ikumbukwe, SI LAZIMA kuandika jina lako la kweli na SI LAZIMA kwenda mwenyewe bank kutuma pesa hizo (kwani unaweza kumpa unayemwamini na kumpa account details na jina lako ambalo ungependa aandike).

Tunaweza kuandika mengi lakini ukweli unabakia pale kuwa JF inahitaji michango yenu kwa sana tu.

Kwa wenye maswali zaidi wanaweza kuwasiliana na Maxence kupitia namba yake ya simu +255713444649.
 
mmh preta leo kweli mapinduzi, baada ya pinduzi lako nashudia na ue tut nae kapindua lake!!!!!!!!!!!

naona leo ni pindu pindu kwa kwenda mbele ila afadhali maana lilikuwa refu
 
naona leo ni pindu pindu kwa kwenda mbele ila afadhali maana lilikuwa refu

sana kama reli ya chigoma enzi zile kabla ya wahindi!!!!!

ila lako chiboko, kila siku jioni mida ya mamushka ntakuwa nakukumbuka !!!

avatar na naniliu zote pindu leo.

indeed its a revolution day. ngoja nikupm kitu.
 
hio link ya kutumia paypal mbona haifanyi kazi? kuna mtu mwenye email account ya paypal ambayo tunaweza kutuma huo mchango?
 
hio link ya kutumia paypal mbona haifanyi kazi? kuna mtu mwenye email account ya paypal ambayo tunaweza kutuma huo mchango?

Mkuu ukifuata link ya https://www.jamiiforums.com/payments.php utakutana na maelekezo yatakayo kupeleka kwenye secured system of paymenyts na baadae utakutana na icons hizi:


btn_xpressCheckout.gif


OR

ContinueCheckoutButton_185x38_EN.gif


Hivyo wewe unayetaka kuchangia via PayPal itakuwa rahisi sana kwako, naamini utaweza mkuu wangu.

Kisha malizia transaction mkuu, kiulaini.
 
Mkuu ukifuata link ya https://www.jamiiforums.com/payments.php utakutana na maelekezo yatakayo kupeleka kwenye secured system of paymenyts na baadae utakutana na icons hizi:


btn_xpressCheckout.gif


OR

ContinueCheckoutButton_185x38_EN.gif


Hivyo wewe unayetaka kuchangia via PayPal itakuwa rahisi sana kwako, naamini utaweza mkuu wangu.

Kisha malizia transaction mkuu, kiulaini.
asante sana mkuu mwanzo haikunipa option ya paypal ilinipa 2c0 ndio maana nikarudi kuuliza nimeiona sasa hivi.asante sana.
 
Back
Top Bottom