Fahamu mambo mbalimbali kuhusu Kilimo cha Korosho

Katika pitapita zangu kwenye kata mbalimbali zilizopo Lindi, aise nimejifunza kuwa watu wengi waliochukua miche ya korosho msimu huu hakika wamekwenda kuipanda katika mashamba niseme machafu au ambayo hayakuandaliwa vizuri!

Nadhani kuna haja ya elimu ya kutosha itolewe kwa wakulima juu ya maandalizi ya shamba hatua kwa hatua mpaka mche wa mkorosho unapopandwa!

Mengi ya mashamba hayo yanamilikiwa na watu waliopo mijini ambao wameweka vijana au mwanakijiji msimamizi ambae anatoa taarifa ya maendeleo ya shamba kupitia simu au picha za watsup!

Ndugu zangu ambao mna interest ya kuwekeza katika kilimo hiki napenda niwakumbushe kuwa kazi ya kilimo hata siku moja haijawai kufanywa au kusimamiwa kwa simu.

Wengi wetu tumeweka mategemeo makubwa sana tukiwa na calculator zetu mezani tuki reffer ile bei ya 3970 kwa kilo times namba ya kilo kwa mkorosho mmoja times idadi ya ekari ulizoambiwa na “mfanyakazi/msimamizi” wako kule Lindi kuwa zimepandwa msimu huu.

Changamoto ni kubwa na kinachoendelea Lindi na maeneo mengine katu hayataweza kututoa hapa tulipo kama juhudi binafsi katika kusimamia uwekezaji huu hazitachukiwa!

Naomba magwiji wa kilimo hiki ambao wamejaa tele katika jukwaa hili watufundishe hatua mbali mbali za maandalizi ili kuokoa jahazi ambalo kwa mtazamo wangu tayari limeshageuzwa lilikotoka na linakaribia kuzama!!

“”NIISHIE HAPO KWA SASA””
Changamoto nyingine kubwa kwa shamba jipya ni nyani! Hawa wanyama wanaweza kukutia hasara hadi ukashangaa maana huwa wanafukua miche ya mikorosho na kuing'oa. Labda Kama kuna utaalam wa kuwathibiti tofauti na kuweka mtu wa kulinda tusaidiane ujuzi tafadhali
 
Changamoto nyingine kubwa kwa shamba jipya ni nyani! Hawa wanyama wanaweza kukutia hasara hadi ukashangaa maana huwa wanafukua miche ya mikorosho na kuing'oa. Labda Kama kuna utaalam wa kuwathibiti tofauti na kuweka mtu wa kulinda tusaidiane ujuzi tafadhali

Mkuu, Mimi Nyani wameniharibia shamba la korosho ekari 30 Ikwiriri, mpaka leo tunahangaika nao
 
Mkuu, Mimi Nyani wameniharibia shamba la korosho ekari 30 Ikwiriri, mpaka leo tunahangaika nao
Akuna mdudu mwenye akili za ki pumbavu Kama nyani anafukua iyo Miche wala Hali Ila to anadhan umeficha kitu chin me walini sumbua sana Lindi.
 
Akuna mdudu mwenye akili za ki pumbavu Kama nyani anafukua iyo Miche Wala Hali Ila to anadhan umeficha kitu chin me walini sumbua Sana lindi
Nimekutana na hiyo changamoto Liwale. Wamefukua eka 12 nikarushia, wakafukua Tena kama 8
 
Nimekutana na hiyo changamoto Liwale. Wamefukua eka 12 nikarushia, wakafukua Tena kama 8
Hahaha yan awa wadudu shida Sana ASA umuone anavyofukua utacheka maana anato mche alafu anaanza kufukua shimo. Utasema anatafuta madin baadea anaanza kuuchambua mche mizizi yote then anahamia mche mwingine.
 
Hahaha Yan awa wadudu shida Sana ASA umuone anavyofukua utacheka maana anato mche alafu anaanza kufukua shimo. Utasema anatafuta madin baadea anaanza kuuchambua mche mizizi yote then anahamia mche mwingine
Washenzi sana Hawa. Inabidi kumtega mmoja halafu unamwamba mtini na kumtundika ili wenzie wamuone
 
HABARI,
"fungafunga,

Ndugu Hongera Tena kwa kuwa na kiasi hicho cha shamba kwani kama ukifanikiwa kupanda shamba lote unauhakika wa kuwa na miti sio chini ya elfu 3 ambacho ni kiasi kikubwa sana kwa kuanzia.
Nakushauri upande mikorosho iliyo bebeshwa kwani unaweza kupanda idadi kubwa kwenye shamba dogo pia inauvumilivu mkubwa wa magonjwa na inatoa mazao mapema.

Kwa kuandaa shamba ukisha safisha nivema kama mengi ni majani itakuwa vema kama ukiyachoma moto huwa inasaidia kuangamiza magojwa mbalimbali yaliyokuwa kwenye mimea hiyo ya mwanzo.

Umbali kati ya shimo na shimo unaweza kuweka kati ya mita 5-6 na umbali kati ya mstari unaweza kuweka mita 6-7,
kwa vipimo hivyo unaweza kuwa na mashimo 100-120 kwa heka moja.

Na uchimbaji wa mashimo unaweza kuchimba sentimeta 50 kwenda chini na upana wa sentimeta 50,Ni vema udongo wa juu nusu ya shimo yani sentimeta 25 ukautenga na ule wa chini wa sentimeta 25,Huu udongo wa juu utautumia kuchanganya na mbolea ya samadi wakati wa kupanda mmea.

Inashauriwa kupanda mmea wakati wa mvua na kabla ya kupanda changanya ule udongo na mbolea na kuacha kwa wiki mbili ili kuwezesha samadi kuchanganyika vizuri na udongo ndipo upande mmea.

Wakati wa kupanda unashauriwa kuweka ule udongo uliochanganya na samadi ujae robo ya shimo ndipo upande mmea wako na na wakati wa kufukia fukia nusu ya shimo kwa utaratibu huo utakuwa umefukia shimo lako na mmea kwa robotatu hiyo itasaidia kuacha eneo la maji kutuama wakati wa mvua au wakati wa kumwagilia na pia mmea kupumua vizuri,

Hii nimekupa picha kidogo juu ya maandalizi hayo ila nakushauri nenda Kituo cha naliendele Nimeweka post zake kadhaa hapa na anuani zake pale utapata maelekezo mengi juu ya magojwa na tiba zake kwakuwa mradi wako unaonekana ni mkubwa huna budi kufika pale.

Contact
Zonal Director (South),
Naliendele Agricultural Research Institute (NARI),
10 Newala Road, P. O. Box 509, Mtwara.
Tel.: +255 732 934 035
Fax.: +255 732 934 103
e-mail: utafiti@iwayafrica.com


LUMUMBA
Mkuu kwa nini majarida mengine wanasema miche ipandwe mita 12 kwa 12 kwa mstari kwa mstari na mche kwa mche

Kipi ni kipimo sahihi kwenye upandaji wa mikorosho?
 
Nilifanikiwa aise namshukuru MUNGU! Nilianza usafi kwa kufyeka msitu mwezi julai 2018 na kufikia novemba nikawa na 50 acres ambapo nilichoma moto kupiga mashimo na kupanda ekari zote 50 ilipofika january 2019. Nimepanda mikorosho kwa ushauri wa ndugu zetu wa chuo cha kilimo Naliendele na mpaka hivi sasa inaendelea vizuri sana!

Mwezi julai tena mwaka huu ntaendelea tena kumalizia kipande cha msitu kilichobaki ili 2020 januari nimalizie eneo lililobaki!

*KARIBU SHAMBANI BROTHER*
Mkuu ulipanda kwa umbali kutoka mche mpaka mche na mstari kwa mstari, msaada tafadhali.
 
Habari ya leo mkuu!
Hongera sana kwa kuwa na ardhi ya ukubwa huo.

napenda kukuongezea ujuzi wa faida kidogo juu ya matumizi bora ya ardhi kuhusu kilimo mseto, iko hivi kipindi unasubiri mikorosho yako ya kisasa(hybride) ianze kutoa matunda ili upate faida takribani miaka 3-5 jaribu kupanda mahindi kwa kipindi cha misimu miwili ya mwanzo kwa hilo eneo lako ili lisipotee bure na hii itapelekea kupata faida ya zao moja under zero cost of production.

(a)gharama za uzalishaji
-kulima ni bure kumbuka umelima kwa ajili ya korosho.
-mbegu ni mifuko 128 kila ekari ni mifuko 4 na kila mfuko ni 12,000/=(1,536,000/=)
-kupanda ekari moja maeneo mengi ni 30,000/=(960,000/=)
-palizi hapa ni ile itakayotumika kupalilia mikorosho(bure)
-sijaweka mbolea kwa sababu shamba kama ulivosema ni virgin.
Jumla ya gharama za uzalishaji/matumizi upande wa mahindi itakuwa ni Tshs 2,496,000/=

(b) mapato
Ekari moja inatoa wastani wa gunia 8-10 chini ya uangalizi mzuri kwa mtu aliezamilia kama wewe,
Hivyo basi utapata magunia 256 kwa ekari 32.

Mapato/mauzo kwa sasa ni 60,000/= kwa gunia (15,360,000/=)

utakuwa na faida ya 12,864,000/= kumbuka hii umelima msimu mmoja tu na nimesema ulime misimu miwili ya wawli maana mikorosho inakuwa bado ni michanga na itakuwa ni sehemu ya ulinzi wa shamba kwa mifugo na watu wanaokuzunguka hivyo. 12,864,000/=x misimu 2 (25,728,000/=).

Nakutakia kazi njema mkuu kwa haya maamuzi yako mazuri.
Ila mkuu hiyo bei ya mahindi ni kwa sababu msimu uliopita mvua hazikuwa nzuri hivyo watu hawakuvuna vizuri.
 
Ila mkuu hiyo bei ya mahindi ni kwa sababu msimu uliopita mvua hazikuwa nzuri hivyo watu hawakuvuna vizuri.
Uko sahihi, lakini ulichokisoma leo kiliandikwa mwaka jana so bei ilikua hiyo. pia sina imani bei itabaki hiyo hiyo unayoisema.
 
Kangomba
Yeah wananunua kwa mkulima kwa bei ya chini mfano elf2 kwa kilo.

Afu anapeleka kuuza ghalani ambako kule utaratibu wa mauzo ni wa mkopo,maana mpaka mnada upigwe bei ifahamike ndo ela inatoka baada ya siku kadhaa.

Huu utaratibu wa kuuza ghalani kwa mkopo ndo unasababisha mkulima auze kwa mnunuzi mdogo kwa bei ya ulanguzi ili tu apate ela ya kujikimu maana akipeleka ghalani ela inachelewa.

Ghalani ela inatoka baada ya mnada kupigwa kwa hiyo mkuu ni fursa kwa watu kwenye ela zao
Ukinunua elf2
Ukauza kwa 3940
Nafikiri hisabati ulisoma darasa la pili
Jibu ngapi hapo?
Mfanyabiashara hapo ndipo anapopunia pesa
Maana akitoa makato kidogo ata 600 tu
Bado inamlipa
3940-600=??
Kila mbuzi anakula kulingana na urefu wa kamba yake
Ila ni biashara haramu mkuu
serikali ikikufuma mnagawana umasikini,maana wanakataza ulanguzi huu
Tehtehteh
Nadhani umeelewa mkuu
 
Asante kwa ushauri LUMUMBA.Kama hutojali naomba namba yako. Yangu ni 0715217124 na ni mdau wa kilimo hichi baada ya kuhamaaishwa na member mmoja wa JF ambaye kwa sasa ni jirani yangu huko shambani Liwale
HABARI,
Pia kwa huo mpangilio wa upana kati ya mstari na mstari mti na mti Kule Dodoma wilaya ya mpwapwa gereza la pale wanashamba lenye mikorosho ya miaka kumi kwa mwaka mikorosho ile inatoa mpaka kilo 30 kwa mkorosho mmoja na ina miaka kumi tu ukiangalia mti hauna unapana hata wa mita 2.5 ila ikifikia zaidi ya mika 25 kama imeanza kubanana unaweza kupunguza mkorosho mmoja kati ya mitatu ila unakuwa tayari umeshapata mavuno zaidi ya mika 20 kwa mkorosho utakao utao ili kupata nafasi,Pia kwa kutumia mikorosho hiyo unaweza kuandaa mwenyewe miche mingine ya kubebesha kwa kutumia vikonyo kutoka kwenye mikorosho hiyohiyo ukaongeza idadi ya miti,

LUMUMBA
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom