Fahamu mambo mbalimbali kuhusu Kilimo cha Korosho

HABARI,
Pia kwa huo mpangilio wa upana kati ya mstari na mstari mti na mti Kule Dodoma wilaya ya mpwapwa gereza la pale wanashamba lenye mikorosho ya miaka kumi kwa mwaka mikorosho ile inatoa mpaka kilo 30 kwa mkorosho mmoja na ina miaka kumi tu ukiangalia mti hauna unapana hata wa mita 2.5 ila ikifikia zaidi ya mika 25 kama imeanza kubanana unaweza kupunguza mkorosho mmoja kati ya mitatu ila unakuwa tayari umeshapata mavuno zaidi ya mika 20 kwa mkorosho utakao utao ili kupata nafasi,Pia kwa kutumia mikorosho hiyo unaweza kuandaa mwenyewe miche mingine ya kubebesha kwa kutumia vikonyo kutoka kwenye mikorosho hiyohiyo ukaongeza idadi ya miti,

LUMUMBA
Point muhimu sana, nimekupata. Sisi tuliowekeza kwenye miti au misitu sasa tunataka kuwekeza kwenye korosho.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
HABARI,
"Mndengereko One,

Sawa hata kama ukitaka kupanda miche 25 kwa heka unaweza sawa waulize kwa vipimo gani na mbegu gani Au kama ni vipimo vya kuchanganya mazao,Mimi nilipost hapa kwamba unapopanda kwa ukaribu miche ya kubebesha huwa haiwi mipana sana kwa haraka inaweza kuchukua miaka 10-20 kuanza kubanana na inapoanza kubanana unaanza kupunguza hapo unakuwa umeshavuna zaidi ya miaka 10 huo mti kabla ya kuukata hata matumizi ya aridhi yanakuwa ni sahihi,Tusibweteke sana kwamba tunaaridhi kubwa ndio tukaitumia hovyo tumia aridhi chache kwa kutoa mazao mengi.
Ila pia kama wamekushauri ulime kwa miche 35 hiyo inawezekana kama unataka kuchanganya kulima mazao mengine kwenye eneo hilo(intercropping)Ila kama sio hiyo idadi ya miche ni midogo sana utatumia vibaya aridhi yako pia nakushauri utembelee mashamba ya mfano hasa ya mikorosho ya kubebeshwa ukapate somo wewe mwenye tusije tukakuchanganya kwa maana kila mtu anautaalamu na maamuzi yake.
USHAURI.

LUMUMBA
Lumumba, mimi nimekuelewa, kwa mtazamo wangu, miaka mitano au kumi ya kwanza naweza kupanda miche 120 kwa ekari moja ili kuongeza kiasi cha mazao miaka ya mwanzo kabla miti haijakua, na miti ikikua napunguza kwani itakuwa tayari ipo ktk kiwango kinachotakiwa.

Pia umesema ambayo ipo grafted ina umbo dogo hivyo naamini spacing ya miti 25 ni miti ya mbegu tofauti.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Bado mkuu sijapata, vp unalo?

Sent using Jamii Forums mobile app
Mimi ndo natafuta mwaka huu, huku Njombe nimeshapanda eka 500 za miti sasa ipo mwaka wa saba, mwaka huu nimeanza kupanda Macadamia nimepata eka mia, nina dada yangu yupo anafanya kazi kwenye maghala ya korosho Mtwara ndo nimempa kazi ya kutafuta ekari mia moja za korosho, pia huku Njombe napanda eka mia moja za chai, naamini nikiwekeza kwenye korosho pia my future definetelly will be great.

Hivyo mkuu tupambane kuhakikisha tunapata mashamba huko kusini maana hakuna kitu kizuri kupata fedha kila mwaka tena fedha za kutosha

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hapa

Sie wa mbali hautushauri kulima huko korosho? Najiona nimekuwa so interested lkn mamangu kanikatisha tamaa kuwa inahitaji close supervision, na wakati wa mavuno korosho hudondoka hivyo ni rahisi kuibiwa. Nimekatishwa tamaa lakini bado roho haitaki kuacha Jambo hili, nawe umesisitiza hapa.
Hata Mimi pia nishapanda toka December na korosho zimeanza kuota, ila kazi zinabana sana yaan hapa napiga hesabu za kwenda pasaka.

Kitu ambacho nakiona shamba linaweza lisikulipe awamu ya kwanza au ya pili ila siku likija kukulipa utashangaa sana, Shamba langu lipo masasi nami nipo Zanzibar/Dar es Salaam.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Habari wana JF. Naomba mwenye uzoefu au utaalamu wa zao la korosho anisaidie kujua mahitaji ya kuanzisha kilimo hiki. Nataka nitafute shamba(virgin land) kwa kilimo hiki, napenda nijue maeneo ambayo zao hili hustawi sana, mbegu bora ya muda mfupi, gharama za kuhudumia hadi kuanza kuvuna ikiwa ni pamoja na madawa, mbolea kama itahitajika na masuala mengineyo.
Noted sir

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa ardhi ya kagera naweza lima korosho?
HABARI,
"hazard Don,

Hongera kwa Swali zuri ambalo jibu lake litawasaidia wengi,Kwa kifupi Tanzania karibu 75%ya eneo lote mazao mengi ya biashara yanakubali mojawapo ikiwa korosho sasa kwa mkoa wa Kagera kuanzia Nsunga, Kyaka, Kyerwa, Nkwenda, Kayanga, Omurushaka, Kamachumu, ushwa, Kashasha, Nshamba, Muleba, Nyakasanza, Nyabugombe, Nyonga, Muzani, Bihararumo, Ruhuma Na maeneo mengi ya Nyanda za huko Korosho inakubali kama Singida na Dodoma mikoa yenye mvua chache korosho inakubali huko hakuna shida kabisa.

LUMUMBA
 
HABARI,
"hazard Don,

Hongera kwa Swali zuri ambalo jibu lake litawasaidia wengi,Kwa kifupi Tanzania karibu 75%ya eneo lote mazao mengi ya biashara yanakubali mojawapo ikiwa korosho sasa kwa mkoa wa Kagera kuanzia Nsunga, Kyaka, Kyerwa, Nkwenda, Kayanga, Omurushaka, Kamachumu, Rushwa, Kashasha, Nshamba, Muleba, Nyakasanza, Nyabugombe, Nyonga, Muzani, Bihararumo, Ruhuma na maeneo mengi ya Nyanda za huko Korosho inakubali kama Singida na Dodoma mikoa yenye mvua chache korosho inakubali huko hakuna shida kabisa.

LUMUMBA
Akhsante kwa majibu mazuri.
 
Wana jamvi! Nataka kuanzisha shamba la korosho la ukubwa wa 32 acres! Naomba wenye utaalaam na kilomo hiki wanijuze juu ya hatua muhimu za kuzingatia tukianzia na kusafisha shamba kwani kwa sasa ni msitu kabisa ambao haujawai limwa chochote!
Pili garama mbali mbali kwa kila hatua na any other information ambayo unadhani itanisaidia!
Natanguliza shukrani!
Habari,
Fungafunga; Unaendeleaje na mradi? Ulifanikiwa kupanda shamba lote?
nawiwa kufahamu hatua uliyopiga kwakuwa nipo mbioni kuchukua mkondo huu pia.

Ahsante

Sent from my SM-J330F using JamiiForums mobile app
 
Habari
Fungafunga; Unaendeleaje na mradi? ulifanikiwa kupanda shamba lote?
nawiwa kufahamu hatua uliyopiga kwakuwa nipo mbioni kuchukua mkondo huu pia... Ahsante

Sent from my SM-J330F using JamiiForums mobile app

Nilifanikiwa aise namshukuru MUNGU! Nilianza usafi kwa kufyeka msitu mwezi julai 2018 na kufikia novemba nikawa na 50 acres ambapo nilichoma moto kupiga mashimo na kupanda ekari zote 50 ilipofika january 2019. Nimepanda mikorosho kwa ushauri wa ndugu zetu wa chuo cha kilimo Naliendele na mpaka hivi sasa inaendelea vizuri sana!

Mwezi julai tena mwaka huu ntaendelea tena kumalizia kipande cha msitu kilichobaki ili 2020 januari nimalizie eneo lililobaki!

*KARIBU SHAMBANI BROTHER*
 
Mkuu umetumia kiasi gani kwa acre kusafisha pori?? Nataka kusafisha pia mwezi wa Saba, ila watu wa huku wavivu sijapata ona, Niko pwani.
 
Mkuu umetumia kiasi gani kwa acre kusafisha pori? Nataka kusafisha pia mwezi wa Saba, ila watu wa huku wavivu sijapata ona, Niko pwani.

Garama za usafi zinategemea mambo makubwa matatu

1. Aina ya msitu/miti iliyopo
2. Mkataba unaoingia na wasafishaji kwa maana ya garama zipi zitabebwa na mwenye shamba na zipi zitakuwa za wasafishaji. (Hapa kuna mambo meeeeengiiii yakujadili)
3. Aina ya wafanyakazi unaowatumia. Utatumia wenyeji au wageni wanao toka mbali na eneo husika (Hapa kuna vitu vingi tena vya kuviangalia na changamoto zake)

Ila kwa kifupi garama zilizopo sokoni kwa sasa ni kati ya Tshs 280,000 hadi 320,000 kwa ekari moja ukiondoa garama ya kununua mashine (chain saw), vifaa vya kazi ikiwamo mapanga, tupa,na buti, kupiga mashimo, miche na kupanda.

Ila usiogope bro karibu sana.
 
Garama za usafi zinategemea mambo makubwa matatu
1. Aina ya msitu/miti iliyopo.
2. Mkataba unaoingia na wasafishaji kwa maana ya garama zipi zitabebwa na mwenye shamba na zipi zitakuwa za wasafishaji. (Hapa kuna mambo meeeeengiiii yakujadili...)

Ila usiogope bro karibu sana..
Mimi sidhani kama nahitaji chainsaw, wachoma mkaa walishanisaidia kwa Hilo, vimebakia vichaka vichaka tu.

Asante though.
 
Mimi natumia elfu 70 kwa heka hapo miti mikubwa bado ambayo inahitaji chain saw so roughly kama laki 1 hivi nataka kukata hiyo miti ili July nisafishe na kuchoma moto,
November nawahi kupanda,
Shamba langu lipo Masasi
Garama za usafi zinategemea mambo makubwa matatu
1. Aina ya msitu/miti iliyopo.
2. Mkataba unaoingia na wasafishaji kwa maana ya garama zipi zitabebwa na mwenye shamba na zipi zitakuwa za wasafishaji. (Hapa kuna mambo meeeeengiiii yakujadili...)
3. Aina ya wafanyakazi unaowatumia. Utatumia wenyeji au wageni wanao toka mbali na eneo husika (Hapa kuna vitu vingi tena vya kuviangalia na changamoto zake)

Ila kwa kifupi garama zilizopo sokoni kwa sasa ni kati ya Tshs 280,000 hadi 320,000 kwa ekari moja ukiondoa garama ya kununua mashine (chain saw), vifaa vya kazi ikiwamo mapanga, tupa,na buti, kupiga mashimo, miche na kupanda.

Ila usiogope bro karibu sana..
 
Mimi natumia elfu 70 kwa heka hapo miti mikubwa bado ambayo inahitaji chain saw so roughly kama laki 1 hivi nataka kukata hiyo miti ili July nisafishe na kuchoma moto,
November nawahi kupanda,
Shamba langu lipo Masasi
Mkuu ninashamba masasi pia, lkn maafisa wa misitu wanakataza kutumia chainsaw kuangusha miti, hivyo tunalazimika kutumia moto na misumeno baridi kwako hali ipoje?
 
Back
Top Bottom