Fahamu mambo mbalimbali kuhusu Kilimo cha Korosho

Usipige mahesabu hayo piga hivi mwaka jana kilo ilifika 3900 na korosho wauza kwa kilo, gunia moja ni sawa na kilo mia sasa itategemea kwenye hiyo miti 25 au 30 utapata kilo ngapi, mfano miti yote ya korosho hiyo 30 au 35 umepata kilo elfu tano mia tano
1kilo=3900tsh
5500kilo=×?
21,450000tsh hiyo kwa bei ya mwaka jana so mwaka huu hatujui if itapanda au laa kama itapanda itazidi kua neema kwa wakulima wa korosho. Na huo ni mfano tu kama utapata hizo kilo au kwa magunia itakua hv
1gunia=390000tsh
20gunia=?
7, 80000tsh
Ni hivyo tu nadhani kaka lumumba akija atatoa ufafanunuzi vzr. Shukran sn
Ahsante mkuu, na mimi mwakani nitapanda. Tatizo la kilimo cha Tz unaweza kuta baada ya miaka 5 bei ikaporomoka sana.
 
Ndio hvy kaka ila tusikate tamaa na kushuka kwa bei na kwa zao la korosho kama utapata kupeleka mwenywe nje ya nchi basi utakua mwenywe kufaidika sana
Ila kupeleka nje ya nchi inatakiwa uwe na mzigo mkubwa sana ili uone faida. Uzuri wa Korosho ni zao la biashara pia chakula, tofauti na kitu kama Pamba ambayo mabadiliko ya teknologia yanaweza kuwapoteza kabisa.
 
Mkuu Ardhi ilikuwa inatolewa na Halmashauri ya Lindi. Sijuhi kwa sasa hivi kama bado wanatoa maana mvua ndo zinaishia labda mpk mwakani tena.

Nimefika Lindi last week na taarifa nilizopewa ni kwamba ardhi waliyoitenga kwa kilimo imeshakwisha!
 
Dah sawa kaka. ni msitu mkubwa sn wa kulimia au pori la kawaida tu kwa ajili ya kufanya usafi
 
Dah sawa kaka. ni msitu mkubwa sn wa kulimia au pori la kawaida tu kwa ajili ya kufanya usafi
Poli la kawaida sana
IMG_20180404_113828.jpg
IMG_20180404_113832.jpg
 
Nna Eka 50 Ikwiriri, Rufiji aliyeko interested aje tuzungumze nimpe Eneo alime kwa makubaliano tukayobaliana.

Ova
 
Please naomba angalia sera ya kilimo kwanza na kipaumbele chake for the next five years. Na kama tuna road map yoyote

Hakuna sera ya kilimo kwanza Tanzania na haijawahi kuwepo. Labda kama unamaanisha sera ya kilimo!! Hata hivyo kwenye sera kuna issues tu na statements ambazo kwake sidhani kama zina msaada kwa sasa..labda ungemwambia asome 5 years plan ya nchi kuangalia vipaumbele hadi ifikapo 2020/21 ningekuelewa. Aidha pia unatakiwa ujue tofauti ya sera mkakati na master plan! Aidha kuna kauli mbiu na long term plans za nchi.
 
Katika pitapita zangu kwenye kata mbalimbali zilizopo Lindi, aise nimejifunza kuwa watu wengi waliochukua miche ya korosho msimu huu hakika wamekwenda kuipanda katika mashamba niseme machafu au ambayo hayakuandaliwa vizuri!

Nadhani kuna haja ya elimu ya kutosha itolewe kwa wakulima juu ya maandalizi ya shamba hatua kwa hatua mpaka mche wa mkorosho unapopandwa!

Mengi ya mashamba hayo yanamilikiwa na watu waliopo mijini ambao wameweka vijana au mwanakijiji msimamizi ambae anatoa taarifa ya maendeleo ya shamba kupitia simu au picha za watsup!

Ndugu zangu ambao mna interest ya kuwekeza katika kilimo hiki napenda niwakumbushe kuwa kazi ya kilimo hata siku moja haijawai kufanywa au kusimamiwa kwa simu.

Wengi wetu tumeweka mategemeo makubwa sana tukiwa na calculator zetu mezani tuki reffer ile bei ya 3970 kwa kilo times namba ya kilo kwa mkorosho mmoja times idadi ya ekari ulizoambiwa na “mfanyakazi/msimamizi” wako kule Lindi kuwa zimepandwa msimu huu.

Changamoto ni kubwa na kinachoendelea Lindi na maeneo mengine katu hayataweza kututoa hapa tulipo kama juhudi binafsi katika kusimamia uwekezaji huu hazitachukiwa!

Naomba magwiji wa kilimo hiki ambao wamejaa tele katika jukwaa hili watufundishe hatua mbali mbali za maandalizi ili kuokoa jahazi ambalo kwa mtazamo wangu tayari limeshageuzwa lilikotoka na linakaribia kuzama!!

“”NIISHIE HAPO KWA SASA””
 
HABARI,
"mahavanga,
Hujakosea kwa kipimo chako hicho nakubaliana na wewe kabisa hata ukitaka miti 20 kwa heka inawezekana ,Kama umefatilia post zangu zote nilieleza vema,Kama mkulima anafanya kilimo cha mchanganyiko na mazao mengine kama mahindi,mtama,ufuta alizeti n.k ni sawa ila kama ni zao la korosho tu ni matumizi mabaya sana ya aridhi sana mita 12 duh.Ndugu mikorosho ya kubebeshwa na ya kisasa huwa haitanuki sana nitatuna picha moja kutoka mahali mkorosho wa miaka 10 haujazidi mita 3 upana kwa kila upande na kila mwaka wanavuna zaidi ya kilo 20 kwa mti mmoja hapo ndani ya mita 12 zako umeacha mikorosho miwili inayoweza kupandwa Hapo kati na bado ungeweza kupanda mazao mafupi kama maharage N.K.Unaweza kupanda idadi kubwa ya miti kwenye heka moja baada ya mika 10 na kuendelea inapozidi kubanana ndipo unapunguza mmoja mmoja ila tayari mti unakuwa umeshakupa mavuno kwa zaidi ya miaka 10 haingii akilini uwache eneo wazi kusubiri miaka 20 ibanane Duh Tusipende kukariri lazima tujiongeze tufate maelekezo ya pembejeo ila kuna mambo mengine lazima kujiongeza,India kati ya nchi zinazoongoza kwenye kilimo hicho kwa heka moja wanapanda mpaka miti 150-200 sasa wewe ndugu ukisema miti 30 Tusibweteke na aridhi tuliyokuwanayo tuangalie kuwekeza sehemu ndogo unavuna kikubwa.TEKNOLOGIA.TECHNOLOGY

LUMUMBA
Nimeupenda ushauri wako huu and it is so technical.

Nimejifunza jambo muhimu ntakaloli apply mahali, literature zinasema hiyo 12M kwa 12M hadi 15M ila ushauri wako umeweka vizuri zaidi.
 
Asante Lumumba, kila mtu niliekuwa namconsult alinipa hesabu ya miche 28 hadi 30 kwa ekari, hadi nikapata shamba la ekari 4 hapo mtwara nikapiga hesabu zangu nikaona ni dogo sana kwani nitavuna kiasi kidogo cha korosho. Ningekuwa nimepata majibu kama haya na maelezo yaliyoshiba i would have decided otherwise.. Nimeshangaa kuona inaweza kufika miche zaidi ya 3000 kwenye hizo ekari kumbe kwa maelezo niliyokuwa nayo mwanzo hapo hata miche 1000 haingeingia shambani.
Asante sana
Based on the reference ulipewa maelezo sahihi tu ila LUMUMBA Kanyumbulika na kuinyumbulisha vizuri zaidi.
 
Back
Top Bottom