Fahamu mambo mbalimbali kuhusu Kilimo cha Korosho

Wana jamvi,

Nataka kuanzisha shamba la korosho la ukubwa wa 32 acres! Naomba wenye utaalaam na kilomo hiki wanijuze juu ya hatua muhimu za kuzingatia tukianzia na kusafisha shamba kwani kwa sasa ni msitu kabisa ambao haujawai limwa chochote.

Pili garama mbali mbali kwa kila hatua na any other information ambayo unadhani itanisaidia!

Natanguliza shukrani.
 
Ndugu Hongera Tena kwa kuwa na kiasi hicho cha shamba kwani kama ukifanikiwa kupanda shamba lote unauhakika wa kuwa na miti sio chini ya elfu 3 ambacho ni kiasi kikubwa sana kwa kuanzia.

Nakushauri upande mikorosho iliyo bebeshwa kwani unaweza kupanda idadi kubwa kwenye shamba dogo pia inauvumilivu mkubwa wa magonjwa na inatoa mazao mapema.

Kwa kuandaa shamba ukisha safisha nivema kama mengi ni majani itakuwa vema kama ukiyachoma moto huwa inasaidia kuangamiza magojwa mbalimbali yaliyokuwa kwenye mimea hiyo ya mwanzo.

Umbali kati ya shimo na shimo unaweza kuweka kati ya mita 5-6 na umbali kati ya mstari unaweza kuweka mita 6-7,
kwa vipimo hivyo unaweza kuwa na mashimo 100-120 kwa heka moja.

Na uchimbaji wa mashimo unaweza kuchimba sentimeta 50 kwenda chini na upana wa sentimeta 50, ni vema udongo wa juu nusu ya shimo yani sentimeta 25 ukautenga na ule wa chini wa sentimeta 25,Huu udongo wa juu utautumia kuchanganya na mbolea ya samadi wakati wa kupanda mmea.

Inashauriwa kupanda mmea wakati wa mvua na kabla ya kupanda changanya ule udongo na mbolea na kuacha kwa wiki mbili ili kuwezesha samadi kuchanganyika vizuri na udongo ndipo upande mmea.

Wakati wa kupanda unashauriwa kuweka ule udongo uliochanganya na samadi ujae robo ya shimo ndipo upande mmea wako na na wakati wa kufukia fukia nusu ya shimo kwa utaratibu huo utakuwa umefukia shimo lako na mmea kwa robotatu hiyo itasaidia kuacha eneo la maji kutuama wakati wa mvua au wakati wa kumwagilia na pia mmea kupumua vizuri.

Hii nimekupa picha kidogo juu ya maandalizi hayo ila nakushauri nenda Kituo cha naliendele Nimeweka post zake kadhaa hapa na anuani zake pale utapata maelekezo mengi juu ya magojwa na tiba zake kwakuwa mradi wako unaonekana ni mkubwa huna budi kufika pale.

Contact
Zonal Director (South),
Naliendele Agricultural Research Institute (NARI),
10 Newala Road, P. O. Box 509, Mtwara.
Tel.: +255 732 934 035
Fax.: +255 732 934 103
e-mail: utafiti@iwayafrica.com

LUMUMBA
 
Nakushukuru sana Lumumba! MUNGU atupe uzima safari ianze.

HABARI,
"fungafunga,

Amen, usirudi nyuma hata kama ukikutana na shauri nyingine mamuzi yako ni yako ni heri kufeli kwa maamuzi yako kwa kuwa utajifunza ila sio ya mwingine songa mbele, Samahani sikukuuliza shamba lako liko wapi.

LUMUMBA
 
Nilikuwa kwenye seminar iliyoandaliwa na Manispaa ya Lindi kwa kushirikiana na Kituo cha Naliendele na Bodi ya Korosho tarehe 6 Januari, 2018 pale Lindi na tulielekezwa kwamba kitaalam ekari moja inatakiwa ichukue miche 25-27 ambapo ni space ya mita 12 urefu na 12 upana. Nimeshangaa kusoma mahali hapa kwamba ekari moja unaweza kuotesha miche 1200.
 
lakin ndugu lumumba baadhi ya watalamu wa nani shauri ni pande miche 35 kwa heka ni sahii kweli

HABARI,
"Mndengereko One,

Sawa hata kama ukitaka kupanda miche 25 kwa heka unaweza sawa waulize kwa vipimo gani na mbegu gani Au kama ni vipimo vya kuchanganya mazao,Mimi nilipost hapa kwamba unapopanda kwa ukaribu miche ya kubebesha huwa haiwi mipana sana kwa haraka inaweza kuchukua miaka 10-20 kuanza kubanana na inapoanza kubanana unaanza kupunguza hapo unakuwa umeshavuna zaidi ya miaka 10 huo mti kabla ya kuukata hata matumizi ya aridhi yanakuwa ni sahihi.

Tusibweteke sana kwamba tunaaridhi kubwa ndio tukaitumia hovyo tumia aridhi chache kwa kutoa mazao mengi.
Ila pia kama wamekushauri ulime kwa miche 35 hiyo inawezekana kama unataka kuchanganya kulima mazao mengine kwenye eneo hilo(intercropping)Ila kama sio hiyo idadi ya miche ni midogo sana utatumia vibaya aridhi yako pia nakushauri utembelee mashamba ya mfano hasa ya mikorosho ya kubebeshwa ukapate somo wewe mwenye tusije tukakuchanganya kwa maana kila mtu anautaalamu na maamuzi yake.
USHAURI.

LUMUMBA
 
Nilikuwa kwenye seminar iliyoandaliwa na Manispaa ya Lindi kwa kushirikiana na Kituo cha Naliendele na Bodi ya Korosho tarehe 6 Januari, 2018 pale Lindi na tulielekezwa kwamba kitaalam ekari moja inatakiwa ichukue miche 25-27 ambapo ni space ya mita 12 urefu na 12 upana. Nimeshangaa kusoma mahali hapa kwamba ekari moja unaweza kuotesha miche 1200.

HABARI,
"Revolution,
Samahani nadhani itakuwa ni typing error kwa heka moja miche 120 kwa ile ya kubebesha na muda unavyozidi kwenda zaidi ya miaka 10 inavyozidi kubanana ndio unapunguza na unakuwa umefaidika na mavuno hayo maelekezo sawa unaweza kuyafata ila mita 12 kama utafanya kilimo cha mchanganyiko ni sawa ila kwa heka moja miche 25?? Sawa mimi nimefatilia sana mafundisho hayo hasa kwa nchi za Asia ambao wana utaalamu mkubwa kwa muda mrefu.

Mimi najua mikorosho mingi ya kubebeshwa huwa haiwi mipana sana mkorosho wa mita 3 kwa upana wa matawi ni mkubwa sana kwa hii ya kubebeshwa sasa mita 12 hilo eneo lililonaki unalitumia kwa kazi gani haa anyway kila mtu anamaamuzi yake ila india wanapanda mpaka idadi hiyo yangu kwa heka moja.

Hiyo ninayoongelea sio ya kubebesha ni hii ya Naliendele ya miaka 3 ambayo itaanza kugawiwa sasa hivi kwa ajili ya kuotesha. Je, hiyo pia ninaweza kuotesha idadi hiyo na baadae nije kupunguza?
 
Nilikuwa kwenye seminar iliyoandaliwa na Manispaa ya Lindi kwa kushirikiana na Kituo cha Naliendele na Bodi ya Korosho tarehe 6 Januari, 2018 pale Lindi na tulielekezwa kwamba kitaalam ekari moja inatakiwa ichukue miche 25-27 ambapo ni space ya mita 12 urefu na 12 upana. Nimeshangaa kusoma mahali hapa kwamba ekari moja unaweza kuotesha miche 1200.

HABARI,
"Revolution,

Soma vizuri pale nilisema miche 120 kwa heka kama una heka 10 itakuwa 1200,Au kama sio hapo please nionyeshe niparekebishe.

LUMUMBA
 
Hiyo ninayoongelea sio ya kubebesha ni hii ya Naliendele ya miaka 3 ambayo itaanza kugawiwa sasa hivi kwa ajili ya kuotesha. Je hiyo pia ninaweza kuotesha idadi hiyo na baadae nije kupunguza?

HABARI,
"Revolution,
Ok sawa Asante hata kama sio ya kubebesha nilipost sana hapa unaweza kupanda idadi hiyo niliyosema ukaanza kuvuna ndani ya miaka 10 miti ikianza kubanana unaanza kupunguza,Haina maana ukaacha aridhi wazi kwa miaka 12 kusubiri ianze kubanana wakati muda huo ungekuwa umevuma korosho tani za kutosha huo sio ushauri mzuri na wakitaalamu labda kama unampango wa kuchanganya mazao mengine kama mahindi,mtama alizeti n.k ila kama ni korosho peke yake sio kabisha ni matumizi mabaya ya aridhi.Mkulima wa Tanzania atazalisha tani 50 kwenye heka 100 lakini mkulima wa india atazalisha tani 50 kwenye hake 35 tu tofauti ni matumizi ya aridhi vitu vingine ni vema kujiongeza.
Ni vema kufata ushauri wa mbegu,Pembejeo upanda wa mbolea ila kwenye swala la nafasi lazima ujiongeze mkuu.

LUMUMBA
 
Mbolea ni lazima kwa miche? Na kama ni lazima na Lindi hamna ya samadi wala kuku ninaweza kutumia NPK ama DAP kwenye kuchanganya udongo?

Pia nimeona wakulima wengi wazawa wa Lindi hawatumii mbolea na mikorosho inaota.
 
Mbolea ni lazima kwa miche? Na kama ni lazima na Lindi hamna ya samadi wala kuku ninaweza kutumia NPK ama DAP kwenye kuchanganya udongo?
Pia nimeona wakulima wengi wazawa wa Lindi hawatumii mbolea na mikorosho inaota

HABARI,
"Revolution,
Kweli mbole ya samadi sehemu nyingi ni adimu hata za viwandani zinafaa kutumika hizo husaidia kukuza haraka ila ki uhalisia hata ukipanda bila mbolea hii miti inaota na utavuna kama kawaida ila tofauti ya Kutumia mbolea husaidia kukua kwa haraka.

LUMUMBA
 
Nashukuru sana mkuu Lumumba, nimepitia Uzi wote nauliza swali ambalo halijaulizwa, Je unaweza kumwagilia mikorosho labda kwa kutumia Sprinkler kila siku jioni kwaajili ya kuifanya ikue haraka haraka? Au unaweza shauri umwagiliaji kwa ratiba ipi? Case study ya shamba ambalo Lipo Lindi.
 
Back
Top Bottom