PatriceLumumba
JF-Expert Member
- Mar 9, 2016
- 426
- 578
Asante sana kwa elimu hiyo broo
HABARI,
"CHUMA NA GREECE,
Asante pia kwa kuelewa,Karibu kama una swali usisite kuniuliza.
LUMUMBA
Asante sana kwa elimu hiyo broo
HABARI,
"fungafunga,
Hongera Mkuu kwa kuweka mkazo kwenye kilimo cha korosho nimeona post yako nitarudi baadae na maelezo ambayo yatakuwa na msaada kwako kwa kuanzia,
LUMUMBA
Nakushukuru sana Lumumba! MUNGU atupe uzima safari ianze.
Shukran mkuu LumumbaHABARI,
Kwanza niwapongeze wadau wote mnaofatilia Kilimo cha korosho.
"Thesis, kimpupu, "Mshuza2,, SUKAH, Gu Jike , ankai, Shark , Mndengereko One ,Na wengine
Nime Post video 4 zinazoonyesha jinsi ya kubebesha miche ya mikorosho (grafting).Ukiangalia kwa vitendo inatosha,Kama una swali niulize.
LUMUMBA
lakin ndugu lumumba baadhi ya watalamu wa nani shauri ni pande miche 35 kwa heka ni sahii kweli
Nilikuwa kwenye seminar iliyoandaliwa na Manispaa ya Lindi kwa kushirikiana na Kituo cha Naliendele na Bodi ya Korosho tarehe 6 Januari, 2018 pale Lindi na tulielekezwa kwamba kitaalam ekari moja inatakiwa ichukue miche 25-27 ambapo ni space ya mita 12 urefu na 12 upana. Nimeshangaa kusoma mahali hapa kwamba ekari moja unaweza kuotesha miche 1200.
Hiyo ninayoongelea sio ya kubebesha ni hii ya Naliendele ya miaka 3 ambayo itaanza kugawiwa sasa hivi kwa ajili ya kuotesha. Je, hiyo pia ninaweza kuotesha idadi hiyo na baadae nije kupunguza?HABARI,
"Revolution,
Samahani nadhani itakuwa ni typing error kwa heka moja miche 120 kwa ile ya kubebesha na muda unavyozidi kwenda zaidi ya miaka 10 inavyozidi kubanana ndio unapunguza na unakuwa umefaidika na mavuno hayo maelekezo sawa unaweza kuyafata ila mita 12 kama utafanya kilimo cha mchanganyiko ni sawa ila kwa heka moja miche 25?? Sawa mimi nimefatilia sana mafundisho hayo hasa kwa nchi za Asia ambao wana utaalamu mkubwa kwa muda mrefu.
Mimi najua mikorosho mingi ya kubebeshwa huwa haiwi mipana sana mkorosho wa mita 3 kwa upana wa matawi ni mkubwa sana kwa hii ya kubebeshwa sasa mita 12 hilo eneo lililonaki unalitumia kwa kazi gani haa anyway kila mtu anamaamuzi yake ila india wanapanda mpaka idadi hiyo yangu kwa heka moja.
LUMUMBA
Nilikuwa kwenye seminar iliyoandaliwa na Manispaa ya Lindi kwa kushirikiana na Kituo cha Naliendele na Bodi ya Korosho tarehe 6 Januari, 2018 pale Lindi na tulielekezwa kwamba kitaalam ekari moja inatakiwa ichukue miche 25-27 ambapo ni space ya mita 12 urefu na 12 upana. Nimeshangaa kusoma mahali hapa kwamba ekari moja unaweza kuotesha miche 1200.
Hiyo ninayoongelea sio ya kubebesha ni hii ya Naliendele ya miaka 3 ambayo itaanza kugawiwa sasa hivi kwa ajili ya kuotesha. Je hiyo pia ninaweza kuotesha idadi hiyo na baadae nije kupunguza?
Mbolea ni lazima kwa miche? Na kama ni lazima na Lindi hamna ya samadi wala kuku ninaweza kutumia NPK ama DAP kwenye kuchanganya udongo?
Pia nimeona wakulima wengi wazawa wa Lindi hawatumii mbolea na mikorosho inaota