Nataka kuanzisha shamba la korosho 32 acres

Prodigal Son

Prodigal Son

JF-Expert Member
Joined
Dec 9, 2009
Messages
982
Points
225
Prodigal Son

Prodigal Son

JF-Expert Member
Joined Dec 9, 2009
982 225
Changamoto nyingine kubwa kwa shamba jipya ni nyani! Hawa wanyama wanaweza kukutia hasara hadi ukashangaa maana huwa wanafukua miche ya mikorosho na kuing'oa. Labda Kama kuna utaalam wa kuwathibiti tofauti na kuweka mtu wa kulinda tusaidiane ujuzi tafadhali
Mkuu, Mimi Nyani wameniharibia shamba la korosho ekari 30 Ikwiriri, mpaka leo tunahangaika nao
 
taikuny

taikuny

JF-Expert Member
Joined
Jan 2, 2016
Messages
1,186
Points
2,000
taikuny

taikuny

JF-Expert Member
Joined Jan 2, 2016
1,186 2,000
Mkuu, Mimi Nyani wameniharibia shamba la korosho ekari 30 Ikwiriri, mpaka leo tunahangaika nao
Akuna mdudu mwenye akili za ki pumbavu Kama nyani anafukua iyo Miche Wala Hali Ila to anadhan umeficha kitu chin me walini sumbua Sana lindi
 
Mandison

Mandison

Senior Member
Joined
Mar 10, 2017
Messages
161
Points
225
Mandison

Mandison

Senior Member
Joined Mar 10, 2017
161 225
Akuna mdudu mwenye akili za ki pumbavu Kama nyani anafukua iyo Miche Wala Hali Ila to anadhan umeficha kitu chin me walini sumbua Sana lindi
Nimekutana na hiyo changamoto Liwale. Wamefukua eka 12 nikarushia, wakafukua Tena kama 8
 
taikuny

taikuny

JF-Expert Member
Joined
Jan 2, 2016
Messages
1,186
Points
2,000
taikuny

taikuny

JF-Expert Member
Joined Jan 2, 2016
1,186 2,000
Nimekutana na hiyo changamoto Liwale. Wamefukua eka 12 nikarushia, wakafukua Tena kama 8
Hahaha Yan awa wadudu shida Sana ASA umuone anavyofukua utacheka maana anato mche alafu anaanza kufukua shimo. Utasema anatafuta madin baadea anaanza kuuchambua mche mizizi yote then anahamia mche mwingine
 
Mandison

Mandison

Senior Member
Joined
Mar 10, 2017
Messages
161
Points
225
Mandison

Mandison

Senior Member
Joined Mar 10, 2017
161 225
Hahaha Yan awa wadudu shida Sana ASA umuone anavyofukua utacheka maana anato mche alafu anaanza kufukua shimo. Utasema anatafuta madin baadea anaanza kuuchambua mche mizizi yote then anahamia mche mwingine
Washenzi sana Hawa. Inabidi kumtega mmoja halafu unamwamba mtini na kumtundika ili wenzie wamuone
 
Y

yonga

JF-Expert Member
Joined
Mar 17, 2012
Messages
1,500
Points
2,000
Y

yonga

JF-Expert Member
Joined Mar 17, 2012
1,500 2,000
HABARI,
"fungafunga,

Ndugu Hongera Tena kwa kuwa na kiasi hicho cha shamba kwani kama ukifanikiwa kupanda shamba lote unauhakika wa kuwa na miti sio chini ya elfu 3 ambacho ni kiasi kikubwa sana kwa kuanzia.
Nakushauri upande mikorosho iliyo bebeshwa kwani unaweza kupanda idadi kubwa kwenye shamba dogo pia inauvumilivu mkubwa wa magonjwa na inatoa mazao mapema.

Kwa kuandaa shamba ukisha safisha nivema kama mengi ni majani itakuwa vema kama ukiyachoma moto huwa inasaidia kuangamiza magojwa mbalimbali yaliyokuwa kwenye mimea hiyo ya mwanzo.

Umbali kati ya shimo na shimo unaweza kuweka kati ya mita 5-6 na umbali kati ya mstari unaweza kuweka mita 6-7,
kwa vipimo hivyo unaweza kuwa na mashimo 100-120 kwa heka moja.

Na uchimbaji wa mashimo unaweza kuchimba sentimeta 50 kwenda chini na upana wa sentimeta 50,Ni vema udongo wa juu nusu ya shimo yani sentimeta 25 ukautenga na ule wa chini wa sentimeta 25,Huu udongo wa juu utautumia kuchanganya na mbolea ya samadi wakati wa kupanda mmea.

Inashauriwa kupanda mmea wakati wa mvua na kabla ya kupanda changanya ule udongo na mbolea na kuacha kwa wiki mbili ili kuwezesha samadi kuchanganyika vizuri na udongo ndipo upande mmea.

Wakati wa kupanda unashauriwa kuweka ule udongo uliochanganya na samadi ujae robo ya shimo ndipo upande mmea wako na na wakati wa kufukia fukia nusu ya shimo kwa utaratibu huo utakuwa umefukia shimo lako na mmea kwa robotatu hiyo itasaidia kuacha eneo la maji kutuama wakati wa mvua au wakati wa kumwagilia na pia mmea kupumua vizuri,

Hii nimekupa picha kidogo juu ya maandalizi hayo ila nakushauri nenda Kituo cha naliendele Nimeweka post zake kadhaa hapa na anuani zake pale utapata maelekezo mengi juu ya magojwa na tiba zake kwakuwa mradi wako unaonekana ni mkubwa huna budi kufika pale.

Contact
Zonal Director (South),
Naliendele Agricultural Research Institute (NARI),
10 Newala Road, P. O. Box 509, Mtwara.
Tel.: +255 732 934 035
Fax.: +255 732 934 103
e-mail: utafiti@iwayafrica.com


LUMUMBA
Mkuu kwa nini majarida mengine wanasema miche ipandwe mita 12 kwa 12 kwa mstari kwa mstari na mche kwa mche

Kipi ni kipimo sahihi kwenye upandaji wa mikorosho?
 
Y

yonga

JF-Expert Member
Joined
Mar 17, 2012
Messages
1,500
Points
2,000
Y

yonga

JF-Expert Member
Joined Mar 17, 2012
1,500 2,000
Nilifanikiwa aise namshukuru MUNGU! Nilianza usafi kwa kufyeka msitu mwezi julai 2018 na kufikia novemba nikawa na 50 acres ambapo nilichoma moto kupiga mashimo na kupanda ekari zote 50 ilipofika january 2019. Nimepanda mikorosho kwa ushauri wa ndugu zetu wa chuo cha kilimo Naliendele na mpaka hivi sasa inaendelea vizuri sana!

Mwezi julai tena mwaka huu ntaendelea tena kumalizia kipande cha msitu kilichobaki ili 2020 januari nimalizie eneo lililobaki!

*KARIBU SHAMBANI BROTHER*
Mkuu ulipanda kwa umbali kutoka mche mpaka mche na mstari kwa mstari,msaada tafadhali
 
V

victory02

Member
Joined
Nov 18, 2015
Messages
37
Points
125
V

victory02

Member
Joined Nov 18, 2015
37 125
Habari ya leo mkuu...!
Hongera sana kwa kuwa na ardhi ya ukubwa huo.

napenda kukuongezea ujuzi wa faida kidogo juu ya matumizi bora ya ardhi kuhusu kilimo mseto, iko hivi kipindi unasubiri mikorosho yako ya kisasa(hybride) ianze kutoa matunda ili upate faida takribani miaka 3-5 jaribu kupanda mahindi kwa kipindi cha misimu miwili ya mwanzo kwa hilo eneo lako ili lisipotee bure na hii itapelekea kupata faida ya zao moja under zero cost of production.

(a) gharama za uzalishaji
-kulima ni bure kumbuka umelima kwa ajili ya korosho.
-mbegu ni mifuko 128 kila ekari ni mifuko 4 na kila mfuko ni 12,000/=(1,536,000/=)
-kupanda ekari moja maeneo mengi ni 30,000/=(960,000/=)
-palizi hapa ni ile itakayotumika kupalilia mikorosho(bure)
-sijaweka mbolea kwa sababu shamba kama ulivosema ni virgin.
Jumla ya gharama za uzalishaji/matumizi upande wa mahindi itakuwa ni Tshs 2,496,000/=

(b) mapato.
Ekari moja inatoa wastani wa gunia 8-10 chini ya uangalizi mzuri kwa mtu aliezamilia kama wewe,
Hivyo basi utapata magunia 256 kwa ekari 32.

mapato/mauzo kwa sasa ni 60,000/= kwa gunia (15,360,000/=)

utakuwa na faida ya 12,864,000/= kumbuka hii umelima msimu mmoja tu na nimesema ulime misimu miwili ya wawli maana mikorosho inakuwa bado ni michanga na itakuwa ni sehemu ya ulinzi wa shamba kwa mifugo na watu wanaokuzunguka hivyo. 12,864,000/=x misimu 2 (25,728,000/=).

Nakutakia kazi njema mkuu kwa haya maamuzi yako mazuri.
Ila mkuu hiyo bei ya mahindi ni kwa sababu msimu uliopita mvua hazikuwa nzuri hivyo watu hawakuvuna vizuri.
 
daudthefarmer

daudthefarmer

JF-Expert Member
Joined
Apr 30, 2016
Messages
5,306
Points
2,000
daudthefarmer

daudthefarmer

JF-Expert Member
Joined Apr 30, 2016
5,306 2,000
Ila mkuu hiyo bei ya mahindi ni kwa sababu msimu uliopita mvua hazikuwa nzuri hivyo watu hawakuvuna vizuri.
Uko sahihi, lakini ulichokisoma leo kiliandikwa mwaka jana so bei ilikua hiyo. pia sina imani bei itabaki hiyo hiyo unayoisema.
 

Forum statistics

Threads 1,336,211
Members 512,562
Posts 32,530,791
Top