Naomba msaada kuhusu biashara ya kuuza na Kubadilisha gesi

Ungekua mbeya ningekua wakala wako mkuu. Ila kwa dar onana na superdealer na sio madealer utapata maelekezo. Kifupi uwe na chumba tin leseni ya biashara fire extinguisher na mzani. Na pesa isiyopungua mil1
 
Ungekua mbeya ningekua wakala wako mkuu. Ila kwa dar onana na superdealer na sio madealer utapata maelekezo. Kifupi uwe na chumba tin leseni ya biashara fire extinguisher na mzani. Na pesa isiyopungua mil1
1M inatosha?
 
Idea nzur tafuta location nzur mtaji ulionao unatosha kabsa kufanya hyo biashara...Oryx,lake,mihan na manjis(mpya).. Tenga 6million kwa mtaji kuanzia !
 
Wadau naomba msaada wenu nina mtaji kama wa milioni kumi 10k tsh,nimepata mawazo ya kuanzisha biasahara ya kuuza Gesi ya kupikia,lakini sijui nianze wapi sijui kama hii biashara ina tija kwaufupi sijui chochote kuhusu hii biashara

Sababu ya kutaka kuanza hii biashara naona kuwa mkaa umekuwa bei juu sana wakazi wengi wa Daresalam wanatumia Gesi kwa matumizi ya kupikia,akili yangu inanambia kama hii biasahara inaweza kunioa katika hali ngumu ya kimaisha...

Naomba msada wenu,asanteni
Kwanza nakupa hongera kwa kufikia uamuzi wako, biashara ya gesi inafaida kubwa sana pale unapopata sehemu inayotoka kwa haraka sana.Kwan faida yake huongezeka kutokana na ujazo wa mtungi utakaouza.Mimi ni mmojawapo wa mfanyabiashara wa gesi,kikubwa ili usipate usumbufu inakubidi uwe na leseni ya biashara,Tin number na fire certificate.
Ufuatao chini ni mkokotoo wa bei ya kununulia na kuuzia kwa brand ya Mihan gas
Bei ya kununulia(GAS ONLY)
6kg=17500
15kg=42000
38kg=85000

Bei utakayouzia wateja(GAS ONLY)

6kg=19000
15kg=48000
38kg=100000

Bei ya mitungi mitupu(Cylinders)

6kg=23000
15kg=42000
38kg=85000

Updates:Bei itashuka zaidi kuanzia week ijayo
 
Unaweza kua na mitungi 20 mikubwa Inanunua mpya 85000mtungi na Gas utawabadilishia watu kuwajazia kwa 46000 we utajaziwa kwa 40000 kwahiyo mtungi mkubwa una faida 6000 kama unauza mitungi 10 kwa siku utakua na faida elfu 60 ndogo mpya ni elfu 45000 kununua gesi ni 16500 we uttauza 19500 au mengine kama kuuza complite unauza kulingana na sehemu ulipo
 
Habarini za muda wanauchumi,

Rejea kichwa cha habari hapo juu,

Naomba msaada nina mpango wakufungua hii biashara na kuna vitu bado nataka kuvijua, na kwa imani watu wengi watajifunza kitu kupitia huu uzi na na kutoa msukumo. Wenye uzoefu wa kutosha juu ya hili tunaomba michango yenu mtusaidie mtupe mwanga, tuanze na michanganuo kati ORYX, ORANGE na MIHANI bei elekezi za jumla, pia gasi ipi inanunulika sana yani yenye high demand na kwanini inapendwa sana.

Pia nasikia bei za jumla zinatofautiana katika kila mkoa, ila mnaweza kunisaidia kunipa bei elekezi za jumla, mkiweka katika mpangilio huu.

BEI ELEKEZI ZA JUMLA
Oryx_complete
6kg...........?
15kg........?
Oryx_Refill
6kg..........?
15kg.......?

Orange_complete
6kg..........?
15kg........?
Orange_Refill
6kg.........?
15kg......?

Mihani_complete
6kg........?
15kg......?
Mihani_refill
6kg.......?
15kg.....?

Halafu na bei za jumla katika hivi vifaa:
-Regulator
-Burner
-figure
-Hosepipe
 
Biashara hii nzuri ukifanya maeneo ambayo bei ya mkaa ipo juu sana.

Kama mwanza gunia la mkaa elf 55,000

Mtungi wa gas 53,000
Gas demand inaongezeka siku hadi siku ili kupunguza matumizi ya mkaa kwa lengo utunzaji wa mazingira... Mijadala mingi ya utunzaji wa mazingira inachochea utumiaji wa gas kwahiyo inafanya soko la gas kuwa zuri
 
Back
Top Bottom