Fisadi.Jones
Senior Member
- Aug 15, 2008
- 110
- 7
- Thread starter
- #41
Vidude gani tena nawe Fisadi?
Niliviulizia hapa mkuu...
Nshukurusa sana kwa wazee wa kukokotoa, mnatoa mwanga sana. Inabidi TRA wawalipe, maana lazima wana-budget ya kutoa elimu ila sijui inaendaga wapi.
Matumaini yangu yakujikomboa na hii adha yanarudi, ila naomba wakuu mnikosoe. Na pengine hii inaweza kuwasaidia wengine kama mimi.
Nimeona kuna hivi vigari vidogovidogo (Nissan March, Toyota Duet, etc) vya mwaka 2001, vya cc 1,000, nimeona vinauzwa FOB $600 mpaka $800. Hivi vinapunguza kodi sana kwa kuondoa dumping fee na excise duty. Tukichukulia CIF ni $2000, pengine mtu anaweza kutoka maana nikikokotoa fasta napata 3,345,300/= bila kumhonga mtu.
Je, maana yake nikipata pa kukopa hiyo 500,000 nikaongezea kwa vi M3 vyangu naweza nikapata moja ya hivi vidude?
Kwa mfano:
http://www.tradecarview.com/used_car/japan car/nissan/march/820691/
http://www.tradecarview.com/used_car/japan car/toyota/duet/900408/
Sijali kina nini, mi ilimradi kitembee tu na kiweze ku-overtake daladala basi ... tehe tehe.
Naomba mawazo wakuu.
Nimeshaelewa elewa kidogo jinsi mnavyofanya ukokotozi, ila nauliza ulize usije kukuta kuna catch mahali, nije kushikwa pabaya.