Nataka kuacha kula ugali wa shikamoo nishaurini wandugu

Xiang Hao

Senior Member
Nov 19, 2016
126
97
Habari ndugu zangu wa JF,

Mimi ni kijana nimezaliwa miaka 22 iliyopita kwasasa nina mpango wa kuanza kujitegemea sina kitanda wala godoro malipo yangu kwa mwezi ni 70 elfu pekee.

Kutokana na hali halisi nataka kuanza kuyakabili maisha yangu sina shaka wala wasiwasi katika kuanza safari hii ya kusaka tonge langu binafsi.

Naomba muongozo kwenu ninataka kuanza kuhifadhi pesa kwaajili ya safari hii ya maisha naomba mnipe maarifa kwa wale wenye uzoefu wa kuanza kujitegemea bila ajira maalum

Shukrani kwa wote watakao changia kwa hekima.

NAWASILISHA
 
nishaanza kupiga pasi ndefu mkuu simu yangu bando kwa mwezi mara moja pia na funga kila jumatatu na alhamisi
Hapana kua baili haimaanishi kujitesa mzee, angalia usije ukajilitea matatizo mengine yakapelekea kushindwa timiza malengo btw nakushauri uanze biashara ndogo ndogo kulingana na mtaji wako then mambo yakiitika ww jiongeze, pesa ipo kama utathubutu niamini mimi
 
nimekupata kaka ahsante kwa ushauri wako nitaleta mrejesho hali itakavyokuwa katika vita hii
 
mkuu nimeshawatema wote sina hata mpango nao maana usawa huu sio poa
Tatizo zikiongezeka utaanza kurudi. Jitahidi sana sana kujiwekea malengo endelevu. Mfano: kufikia mwezi wa 12 unataka uwe umeweka kiasi gani cha pesa hiyo pesa igawe kwa mwezi utapata jawabu. Utakapofikia miaka 25 unataka uwe na nini gharama za hiyo kitu nk. Anza kuweka mikakati midogo midogo na mikubwa bila kuvunja sheria za nchi. Angalia pia aina ya watu unaokuwa nao je wana hali ambazo unatamani kuwa kama wao au ndo wale kila ukipata mia wanataka mia 5. Jibu unalo mwenyewe.
 
ahsante sana mkuu nimeyapata maneno yako nayaweka akili mungu akuzidishie maarifa shukrani sana
 
Fungua account bank.kila mwezi deposit elfu 40.alafu elfu thalathin ndo utumie.kwa mwaka utapata 480,000.huu ni mtaji Wa kufungua kabiashara
 
Back
Top Bottom