Nataka kuacha kazi nisimamie biashara yangu lakini naogopa-naomba ushauri | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nataka kuacha kazi nisimamie biashara yangu lakini naogopa-naomba ushauri

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by FADHILIEJ, May 13, 2011.

 1. FADHILIEJ

  FADHILIEJ Senior Member

  #1
  May 13, 2011
  Joined: Nov 5, 2010
  Messages: 134
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  Wana JF nimekuwa muajiriwa kwenye NGO Moja kwa takriban miaka kumi.
  Imefika wakati nataka kuacha ili nipate muda wa kutosha kusimamia biashara yangu japo ni ndogo.
  Kinachonisumbua ni hofu ya kuacha kazi.naombeni nishaurini nitumie mbinu gani?
   
 2. Raia Fulani

  Raia Fulani JF-Expert Member

  #2
  May 13, 2011
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 10,220
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Tatizo unang'atwa na hofu. Angalia kama mapato ya biashara yako in terms of net profit kwa mwezi ni zaidi net salary yako. kwa mwezi. Cha pili angalia opportunity cost. Uko huru zaidi upande gani. Pia angalia uendelevu wa biashara yako kwa miaka 5 ijayo kama itakuwepo. Angalia una ujuzi gani na hiyo biashara pamoja na washindani wako ktk soko. Last but not least angalia uthubutu wako katika kujiajiri-entrepreneural ability. Hii ni rasilimali muhimu sana. Baada ya hapo kata shauri
   
 3. BASIASI

  BASIASI JF-Expert Member

  #3
  May 13, 2011
  Joined: Sep 20, 2010
  Messages: 3,102
  Likes Received: 341
  Trophy Points: 180
  miaka kumi unafanyaa nini yotee kwanza umechelewa na bado una nafasi mkuu kamua kivyako
  tuko nyuma yako
   
 4. Gurta

  Gurta JF-Expert Member

  #4
  May 13, 2011
  Joined: Sep 17, 2010
  Messages: 2,246
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  Haupo tayari, endelea na kibarua chako hapo NGO mkuu usitafute presha bure. In short you are not a 'business-type' guy, you are a 'salary-type' guy
   
 5. VIKWAZO

  VIKWAZO JF-Expert Member

  #5
  May 13, 2011
  Joined: Apr 9, 2011
  Messages: 1,910
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  pamoja na ushauri wa mkuu hapo chini kama biashara yako ina wateja wa uhakika kwa kipindi cha miaka mitano ijayo na na kama inaweza kupanuka kama ikinderezwa bora kusimamia biashara.
  lakini pia ni ukuweka detail za kutosha hapa, utopata ushauri wa maana au kukusaidia


   
 6. Babkey

  Babkey JF-Expert Member

  #6
  May 13, 2011
  Joined: Dec 10, 2010
  Messages: 4,256
  Likes Received: 2,079
  Trophy Points: 280
  Wasiwasi ni akili mpendwa.
  Ni vema ukaangalia faida unazopata kibaruani kwako na biashara pia. Uhakika ni muhimu juu ya mwendelezo wa biashara yenyewe isije kuwa ni ya msimu tu.
  Endelea kutumia kazi kama dhamana kama haikubani sana katika shughuli zako binafsi. Ukipata faida kotekote huoni kuwa inalipa zaidi?
   
 7. Wakumwitu

  Wakumwitu JF-Expert Member

  #7
  May 13, 2011
  Joined: Jan 22, 2011
  Messages: 373
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Kuna Professor wangu mmoja amenifundisha enterpreneurship and Innovation alituambia darasani hivi. Alifanya kazi makampuni makubwa mf IBM nk. akwa anasema niligundua siwezi kuwa President akaacha, akaend akampuni nyingine vilevile akaacha kwa sababu hiyohiyo. Alipokuwa na umri wa miaka 37 akaamua kuacha kazi zote akaanza shughulizake binafsi. Na toka wakati huo hajawahi kuludi nyuma. NA sasa biashara zake zina mtaji wa Dola Ml.3 za kimarekani. almost 4.5 billion kwa hela za madafu.

  Sasa basi angalia Business Plan yako for the next 3 to 5 years. Tengeneza Income Statement Projection for that period.. na kwa kuwa umekuwa nayo tayari haitakusumbua kujua Annual Revenue generation na expenses zake. Pili angalia Balance Sheet yako inasemaji in terms of equity( chako ni kiasi gani na Benki ama business patner wako) Alafu mwisho Cash flow kwa kipindi chote cha miaka utayoamua.

  Hii itakusaidia kujua ni faida kiasi gani unapata kwa mwaka, hata kwa mwezi. Then hapo utakuwa na uhakika wa kujua kuwa biashara itaendelea ama lah.. Kinachoshinda wengi ni kutosimama kwa misingi ya biashara aliyoweka mwenyewe.

  UKiweza kuwa na business plan nzuri na ukaisimamia basi hutokuwa na hofu ya kuacha hiyo kazi unayofanya

  Option nyingine unaweza endelea na kazi yako lakini ukai monitor kwa results produced kwa uliowaajiiri but business plan ni muhimu mkuu.

  All the best
   
 8. Manumbu

  Manumbu JF-Expert Member

  #8
  May 13, 2011
  Joined: Oct 28, 2009
  Messages: 1,751
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  niliwahi kusoma katuni kwenye newsweek zamani kidogo. kanuni ya kwanza ya kujitegemea kwenye soko huria ni kuruka toka kwenye ndege angani ukiwa na parachuti. lazima uiache ndege (sehemu salama) kwanza. halafu ukishaanza kudondoka ndo unafungua hilo parachuti lililoko mgongoni kwako. kwanza huna uhakika kama litafunguka. lakini pia huna uhakika litakapofunguka litakupeleka mpaka wapi. kwa hiyo hofu ya yote hayo lazima uwe nayo kabla ya kuacha kazi ujitegemee. na katika kuweka mambo sawa ndo maana unashauriwa kutazama mambo mengi kwa marefu na mapana. ila kikubwa sana cha kutambua ni kuwa huwezi kuwa tajiri kwa kuajiriwa...haipo. ukitaka kuwa tajiri lazima ujiajiri!
   
 9. FADHILIEJ

  FADHILIEJ Senior Member

  #9
  May 14, 2011
  Joined: Nov 5, 2010
  Messages: 134
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  Nashukuru kwa mawazo yote mazuri,
  nimepaata idea mpya kwamba labda nichukue likizo isiyo na malipo kwa miezi mitatu plus annual leave nisome ramani na kuondoa hofu,kikieleweka basi niachie ngazi,

  mnasemaje?
   
 10. K

  Kaseko Senior Member

  #10
  May 14, 2011
  Joined: Feb 15, 2011
  Messages: 160
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  fanya vyote mpaka hapo ajira itakapokoma, sababu biznes yako imetokana na ajira, ukiacha ajira bizness ina bankrupt sure nakueleza. Continue doing reseach on that.
   
 11. M

  Mama Joe JF-Expert Member

  #11
  May 14, 2011
  Joined: Mar 30, 2009
  Messages: 1,507
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  Hii ndiyo naona ni sawa maana inaonekana hujawi kutokuwa muajiriwa kabisa, pia angalia uwezekanao wa kutotumia mshahara wako kabisa kwa miezi sita ukitegemea hiyo biahsara tu, I mean iwe inajizungusha yenyewe na kuweza kukupa mahitaji yako na faida kiasi, ili ukiacha usiwe na hofu. hat ahiyvo muda huo ni mfupi na inaweza kukupa picha nzuri au mbaya kwa iyo angalia other factors ambazo zimechangia kwa kipindi utakapokuwa unafanya evaluation mfano kupanda na kushuka shilingi etc.
   
 12. babalao

  babalao Forum Spammer

  #12
  May 14, 2011
  Joined: Mar 11, 2006
  Messages: 431
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Angalia kipato kama biashara yako inaingiza faida kiasi sawa na mshahara wako unaweza kuacha na kujiunga na biashara yako kama unaweza kuishi bila kuchukua mshahara wako zaidi ya miezi 6 unaweza kuacha kazi vinginevyo endelea na kazi ukiacha utajuta.
   
 13. Mgombezi

  Mgombezi JF-Expert Member

  #13
  May 14, 2011
  Joined: Mar 23, 2009
  Messages: 630
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  "Uoga wako ndio umaskini wako!!" - Kanyagio (JF Senior Expert Member)
   
 14. L

  LAT JF-Expert Member

  #14
  May 14, 2011
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 4,523
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 0
  mwisho wa siku lazima urudi kujiaajiri ....hata pensheni huisha kama hujajiandaa...... tafakari chukua hatua mapema

  be strong and decide
   
 15. A

  Akiri JF-Expert Member

  #15
  May 15, 2011
  Joined: Sep 21, 2010
  Messages: 1,447
  Likes Received: 62
  Trophy Points: 145
  mkuu umenena. Huyu jamaa bado kwenye kujiajiri. Nadhani endelea na kazi yako na tafuta muda wa kujifunza zaidi kuhusu hiyo biashara mpaka hapo utakaporidhika kwamba hiyo biashara inaripa. Binafsi nilijitoa muhanga nikaacha kibaru na kujikita kwenye kikampuni changu.sasa si haba nimetoka kwenye sole proprietor naelekea kuwa limited
   
 16. L

  LAT JF-Expert Member

  #16
  May 15, 2011
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 4,523
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 0
  mkuu ... kwenye ujasiriamali usithubutu kujaribisha au kufanya vitu mguu nje mwingine ndani .... fanya maamuzi ... after all kwenye ujasiriamali siyo siku zote mambo ni mazuri ..kuna up and downs ...
   
 17. A

  Arkad Member

  #17
  May 16, 2011
  Joined: Jan 16, 2011
  Messages: 25
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Biashara ni kitu kinachoweza kujiendesha chenyewe ndani ya mwaka mzima bila uwepo wako. Sasa nionavyo mimi hapo utakuwa umebadirisha ajira sio kusimamia biashara.
  Usiache kazi.
   
 18. F

  FUSO JF-Expert Member

  #18
  May 16, 2011
  Joined: Nov 19, 2010
  Messages: 11,822
  Likes Received: 2,302
  Trophy Points: 280
  Tumia hesabu ifuatayo:

  Chukua mshahara wako kwa mwezi gawanya kwa 30 then utapata kiasi gani kwa siku, then ringanisha na pato lako la siku kwenye biashara yako.

  Kama tofauti yake ni 5% plus or minus then upo safi, hakuna haja ya kuogopa.

  Angalia product yako kama ina demand kubwa kwenye current na future market, if YES then mwaga manyanga kazini - chukua nusu NSSF yako baada ya miezi sita wekeza kwenye biashara.

  Baada ya miaka 5 utakuwa mbali sana- Kama mkeo anafanya kazi we mwache aendelee huko usimwachishe.

  Tatizo wengi ni woga wa kuacha kazi.
   
 19. F

  FUSO JF-Expert Member

  #19
  May 16, 2011
  Joined: Nov 19, 2010
  Messages: 11,822
  Likes Received: 2,302
  Trophy Points: 280
  duh hapo kwenye blue ndiyo kikwazo, wengi wetu business plan zetu ni vichwani kwetu. mambo ya kuandika andika as if unaenda kuomba mkopo benki duh.
   
 20. Mihayo

  Mihayo JF-Expert Member

  #20
  May 16, 2011
  Joined: Apr 12, 2010
  Messages: 270
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Mkuu niliacha kazi 7 years a go kusimamia biashara yangu na sikuwa na willing ya my wife and my mother, but I decided it. Ni ngumu kwa kiasi fulani kwani 3 months down the line mambo yaliharika sana baada ya kuugua na vijana niliowaajiri kunichakachua. Sikukata tamaa nilipigana kiume na ninavyo andika niko napambana na my wife ameamua kujoin the boat from last year. Hivyo karibu sana mzee uwanjani pambana na utafanikiwa. Kwa taarifa tu nilipoamua kuacha my gross salary it was aroung 6.7m
   
Loading...