Nataka kuacha kazi, niendeshe Ubber. Ushauri.

Nakuona mkoloni mweusi jinsi unavyowakamua wenzako.
Niambie hivi nyie mnafanya kazi gani mpaka mlipwe 25%.
Mwanangu nunua bajaji paki kijiweni kwasiku utapata mpaka 80 ukikaa vijiwe vizuri. Ubber ni matapeli .
Ndio maana siku zote matajiri watabaki kuwa wachache mno, uber imetajirisha vijana:
1. Anakopeshwa gari bila sent tano kijana anajikunja ndani ya miaka 2 tu gari lake
kupitia Uber CRDB pekee wamekopesha magari 260 bado bank zingine bado mtu mmoja mmoja.
2. Niambie ni wapi utakopeshwa gari ya 12 mln bila sent ? mtaji ni leseni yako tu
3. Ukiona mabank wanafatilia mradi na wako tayari kutoa pesa zao jua hapo kuna ulaji
4. Uber ni FURSA yako wewe" KIJANA"Mchakalikaji/mchapakazi, Discipline ya hakika,
dereva mjuzi/uzoefu ,huna anasa/ulevi wowote, mwenye ndoto na malengo,

. . . . Inaendelea . . . .
 
Wewe bado hujajielewa. Huwezi kuomba ushauri kwa details finyu namna hiyo. Mfano kumshauri mtu anayelipwa net mil 3 aache kaz akafanye ubber ni tofauti na anayepojea net btn 0-500,000 kwa mwezi (assuming mazingira ya kaz yapo okay)
 
Unataka kuruka mkojo ukanyage mavi naona kaka yangu wadamu alikuwa na gari mbili uber kazitoa ww wataka endesha haya kila la kheri
Acha kumtisha, cha msingi ungeeleza nini kimemfanya ashindwe, labda huyu ana gari lake na atakuwa anaendesha mwenyewe, huyo kaka yako, alikuwa anatumia watu kuendesha!! Kwani hakuna wanaondesha uber na kufanikiwa?
 
Usimpotezee mwenzako mda nawala simkatishi tamaa ajaribu week tu aone mwenyewe pasua kichwa hiyo biashara wala simshauri aende huko.

Sababu yakutoa gari zake kaka yangu ni kama yafuatayo:-
1. Kila weak garage
2. Uchakavu mkubwa wagari.
3. Hesabu haziletwi sawa
 
Suala la kuwa kazini na kuacha kazi na kujiajiri kote nikutafut pesa, suala hapa ni kupata uzoefu wa mzunguko wa pesa ambayo huna uhakika nayo (Biashara) mtaani.
 
Habar za Wikiendi.

Mimi ni kati ya wale tuliochoshwa na Ajira. Nimefikiria sana naona bora nianze ubber. Naomba ushauri kwa wazoefu wa ubber.
Mwanaume wa kweli kwanza hujiuliza anataka kufanya kitu gani halafu anafanya utafiti kujiridhisha mwenyewe. Kwa uzoefu wangu watu wengi wa aina yako hawajui wanachotaka kukifanya na mara nyingi hubadilika badilika. Mambo yanapo haribika hutafuta mchawi wa kumuelekezea lawama.
 
Nakuona mkoloni mweusi jinsi unavyowakamua wenzako.
Niambie hivi nyie mnafanya kazi gani mpaka mlipwe 25%.
Mwanangu nunua bajaji paki kijiweni kwasiku utapata mpaka 80 ukikaa vijiwe vizuri. Ubber ni matapeli .
Shukran sana, naelewa vema na na feel unachokifikiria, bayati mbaya mm sio wa huo upande unaoufikiria japo ni mmoja wa wadau wa uber, na kama wewe kwa asili ni mtumwa(sina maana mbaya) kwa lugha nyingine sio mjasiriamali kitabia HUTANIELEWA KAMWE, wale kwa kuzaliwa ni wajasriamli wananielewa vema.
Naomba radhi kama nitakuwa nimekukwaza.
 
Habar za Wikiendi.

Mimi ni kati ya wale tuliochoshwa na Ajira. Nimefikiria sana naona bora nianze ubber. Naomba ushauri kwa wazoefu wa ubber.
Mkuu inasemekana kuwa ubber ilikuwa inalipa sana zamani ila siyo kwasasa kwakuwa wana discount na kushusha bei mara kwa mara bila kujali mmiliki wa chombo anapata nini.
Kabla ya kuacha kazi fanya research usiwe kama kawaida ya Watanzania wengi unaanza fanya kitu ushajitosa ndipo unaanza fanya research wakati inabidi ufanye research kabla ya kujitosa
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom