Natafuta watu/mtu makini wa kusoma naye Chartered Institute of Marketing CIM-PGD | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Natafuta watu/mtu makini wa kusoma naye Chartered Institute of Marketing CIM-PGD

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by JF Marketer, Jan 16, 2012.

 1. JF Marketer

  JF Marketer Member

  #1
  Jan 16, 2012
  Joined: Jan 3, 2009
  Messages: 70
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Ninataka kuchukua kozi ya masoko inayotambulika ulimwenguni katika ngazi ya Uzamili kwa njia ya masafa. Nimepata Kituo kinachoendesha masoma haya kutoka Kenya.

  Kwa ujumbe huu, ninawaalika watu/mtu makini anayemaanisha kweli na kujituma kwa dhati kujiendeleza kitaaluma ajiunge nami ili tushirikiane katika kusaka elimu hii. Elimu ya masafa si mkate wa siagi. Inahitaji adabu na utiifu mkuu katika matumizi ya muda. Hii lazima itoke ndani ya nafsi ya mhusika maana hakuna wa kukushurutisha.

  Mimi niko Dar na muda wangu wa kusoma ni kuanzia saa 11 Jioni. Pia naweza kusoma katika siku za mwisho wa wiki. Kama upo tayari kujiunga nami basi tuwasiliane:

  View attachment Post-Graduate Fee's breakdown-1.pdf

  Barua pepe: upegra@gmail.com
   
 2. JF Marketer

  JF Marketer Member

  #2
  Jan 17, 2012
  Joined: Jan 3, 2009
  Messages: 70
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Wana JF,
  Vipi, mbona hakuna jibu?!
  Inamaanisha watu hawasomi Jukwaa la Elimu au ni kwamba tunapenda sana Siasa na Udaku!
   
 3. kussy

  kussy JF-Expert Member

  #3
  Jan 17, 2012
  Joined: Jun 15, 2010
  Messages: 346
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  Ndugu tumeiona sio wote tuko kny MARKETING ungekuwa unafanya CFA ningekutafuta!
   
 4. kingadvisor

  kingadvisor Senior Member

  #4
  Jan 17, 2012
  Joined: Dec 21, 2011
  Messages: 109
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Watanzania wengi hatupendi hayo masomo ya kusomea online.Na hilo tangazo la kutoka kuwa kuna online course Kenya inayotmbuliwa pia linaogofya.Baadhi ya Watanzania i wamelizwa na wakenya kuna watanzania wana maoni kuwa ukiuliza wanaigeria wa Afrika mashariki ni akina nani watakwambia wakenya.Anyway wakenya wana kazi ya kuwadhibitishia baadhi ya watanzania kuwa wao si wanigeria kwenye deals ziwe za kibiashara n.k
   
 5. feis buku

  feis buku JF-Expert Member

  #5
  Jan 17, 2012
  Joined: Aug 29, 2011
  Messages: 2,371
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Tuko/niko bize MMU
   
 6. JF Marketer

  JF Marketer Member

  #6
  Jan 17, 2012
  Joined: Jan 3, 2009
  Messages: 70
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  kingadvisor,

  Ni utapeli upo lakini katika hii kozi iliyo chini ya Chartered Institute of Marketing-United Kingdom (CIM-UK) kufanyiwa utapeli lazima kwanza na wewe uwe punguani! Unapojisajiri unalipa ada ya uanachama moja kwa moja CIM-UK. Unachokilipa Kenya ni ada ya masomo kwa njia ya masafa.

  Na hiki chuo cha Kenya kimesajiliwa na CIM-UK kama accredited training center. Unaweza kulithibitisha hili kwa kusoma Prospectus zao kwenye mtandao Search results
   
 7. JF Marketer

  JF Marketer Member

  #7
  Jan 18, 2012
  Joined: Jan 3, 2009
  Messages: 70
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Anyone please..........
   
 8. Husninyo

  Husninyo JF-Expert Member

  #8
  Jan 18, 2012
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 23,814
  Likes Received: 583
  Trophy Points: 280
  sijaelewa, ni lazma usome na mtu?
   
 9. JF Marketer

  JF Marketer Member

  #9
  Jan 20, 2012
  Joined: Jan 3, 2009
  Messages: 70
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Siyo lazima. Ila natambua udhaifu wangu unaotokana na kupenda kusoma kwa mijadala. Siwezi kujadili na nafsi mmoja.
   
 10. JF Marketer

  JF Marketer Member

  #10
  Jan 25, 2012
  Joined: Jan 3, 2009
  Messages: 70
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Bado nakuhitaji na kukusubiri wewe msomi na Mtaalamu wa Masoko mtarajiwa
   
Loading...