Natafuta Volunteers ili tuweze kumerge pamoja kwa ajili ya kusolve various social-economical problem

hbi

JF-Expert Member
Feb 6, 2011
678
297
Habari yenu wanaJamii, Ninawazo lakukutana na watu ambao tutakubaliana nao kuweza kubrainstorm na kutafuta solutions ya matatizo mbalimbali ambayo yanaizunguka jamii yetu kwa ujumla. Nimetarget zaidi watu wanaotoka katika nyanja ya taaluma ya habari na mawasiliano (ICT). Kitakachofanyika baada ya watu hao kupatikana na kila mmoja kuridhia(kwa sababu hakuna mtu atakayekua anatulipa) tutaanza kupanga namna ya kukutana ili tuweze kuidentify baadhi ya problems ambazo tunaweza kutumia knowledge tuliyonayo kuprovide solutions. After that as a team kila mmoja anachangia kulingana na nyanja yake. Mfano solution ni kudevelop mobile app, kuna watu kwa ajili ya kufanya designing, mwenye kucode atacode, pia mtu kwa ajili ya documentation atafanya kazi yake nakadhalika nakadhalika. Vivo hivyo kwa solutions zozote zitakazokua zinapatikana.
Najua changamoto zitakua nyingi lakini kama nia tunayo tunaweza kufanikiwa. Napokea mawazo na michango yoyote kwa watu wenye uzoefu ili tuweze kuboresha wazo hili kwa pamoja. Kama upo tayari unaweza kuniPM ikiwa ni pamoja na mawasiliano yako ili tuweze kuwasiliana zaidi. Kwa kuanza na prefer zaidi watu waishio Dar es Salaam, ili iwe rahisi. Sehem za kukutana na kufanyia kazi jambo hili zipo, wengi wetu mtakua mmeshawai kusikia kuna sehem inaitwa KINU na nyingine ni pale COSTECH(TanzICT). Karibuni sana wadau, mawazo yenu yanahitajika sana.
 
maisha ya bongo ni ya kukimbizana nayo mkuu kodi inakusubiri, watoto wanataka kwenda shule, nyumbani wale, umeme, maji gari inahitaji mafuta halafu uniambie nifanye kazinya kujitolea niache kutafuta hela think twice mkuu this is not califonia where there is google, and facebook this is dar es salaam aake up mkuu
 
maisha ya bongo ni ya kukimbizana nayo mkuu kodi inakusubiri, watoto wanataka kwenda shule, nyumbani wale, umeme, maji gari inahitaji mafuta halafu uniambie nifanye kazinya kujitolea niache kutafuta hela think twice mkuu this is not califonia where there is google, and facebook this is dar es salaam aake up mkuu

Ndugu yangu unachokizungumza ni sahihi kabisa, lakini sidhani kama ni sababu yakushindwa kufanya shughuli za kujitolea, na pia haikatazwi mtu kua na shughuli yake inayomuwezesha kukidhi mahitaji yake na kama anaweza kua na muda wa ziada unatosha kabisa kufanya hicho kitu. Asante kwa mawazo yako
 
Imetulia sana hii acha hawa wenye akili zilizo lala waendelee kusubiri kufanyiwa mabo na wazungu toka California nipigie simu brother :+255 716 217621 we can talk more .........Jumanne Mtambalike (GreenTech360)
 
  • Thanks
Reactions: hbi
Wazo zuri sana kijana. Natumaini watapatikana vijana wengi kwenye hii kitu kwani tukitaka kweli nchi yetu kuendelea inabidi tujitoe kweli. Hila mliopo Dar mkianza tunaomba kupata maelezo ya mahali na muda mtakapo kuwa mkikutana hata waliopo nje ya Dar wanaweza kujpanga na kuja mara moja hapo.
 
hapa yataka moyo kujitolea kwa kweli, wazo zuri sana kwa maendelo ya jamii yetu ya kitanzania
 
Imetulia sana hii acha hawa wenye akili zilizo lala waendelee kusubiri kufanyiwa mabo na wazungu toka California nipigie simu brother :+255 716 217621 we can talk more .........Jumanne Mtambalike (GreenTech360)
Okey brother Jumanne takupigia simu, naona watu wamekua wagumu sana kujitolea, wakipatikana watu baadhi tunaweza tukaanza kukutana tuone tunafanyaje, pia wewe unaweza ukatupa mwanga zaidi maana una uzoefu kwenye kusimamia masuala ya namna hii...
 
Back
Top Bottom