Natafuta vijana wa kupalilia shamba la nanasi na msimamizi wa shamba

Kishaju

Senior Member
Feb 23, 2008
106
62
Ndugu zangu naomba mnisaidie kama mnawajua vijana wachapa kazi wanaoweza kufanya kazi ya palizi kwenye shamba langu la nanasi ambalo lipo Bagamoyo, Fukayosi. Nahitaji kufanya palizi kabla ya mvua kuanza mwezi wa tatu.

Eka ambazo nimepanda hadi sasa ni 12 na tatizo kubwa linalonikabili kwa sasa ni nguvu kazi. Vijana wengi ambao wananifanyia kazi wana tatizo la ulevi (sio beer za TBL ni mataptap), uzembe, wizi na udanganyifu . Wakipata pesa mpaka waimalize yote ndo warudi kazini na ukiwapa "advance" kabla ya kazi ndo inakula kwangu.

Bila shaka wale mnaojishghulisha na kilimo mnaweza kuwa mmeshakutana na vijana wanaojituma na kufanya kazi kwa usahihi.

Pili natafuta mtu mwenye uzoefu na usimamizi wa mashamba (hasa ya nanasi) ambaye nitamuajiri kama Bibi au Bwana Shamba (Farm Manager). Kazi yake kubwa itakuwa ni kusimamia palizi kuhakikisha kwamba kazi ya kulitunza shamba inafanyika vizuri na kuwapangia kazi za kufanya vibarua. Hii inaweza kuwa ajira ya kudumu kwani mpango wangu ni kuwa ni ufikisha eka 30 za nanasi ifikapo 2014 pia na kufuga mifugo mbalimbali hapo shamba (mbuzi, ng'ombe, kuku, bata nk). Kwa hivi sasa niko kwenye ujenzi wa nyumba ya Farm Manager na pia kisima cha maji kitakachokuwa na uwezo wa kutunza lita 100,000.

Kama unawajua vijana wa kazi basi naomba uni-PM kwa mawasiliano zaidi tafadhali.


Nitashukuru sana kwa msaada wenu.
 
Kishaju!

Wakati mwingine jaribu kuleta POST mapema!

Ndiyo kazi zangu.
Panda mapema
Palilia mapema

Ndiyo kauli ya Baba wa Taifa enzi ya Uhai wake.
Mpk hapo sikulaumu hata kidogo kwa sababu kosa si kosa kurudia kosa ndiyo KOSA!

Na tumwombe MUNGU atujalie next season!
 
business plan yako inasemaje kwenye hali kama hii? You may need to go back to the drawing board.
 
kama ulivyosema hao ulionao ni wazembe , walevi, NI AIBU KWA TAIFA HILI KWAMBA WATU WANALIA AJIRA HAKUNA UKWELI HAKUNA MWAAJIRIWA , kuna umuhimu wa kutafakari hili , mimi nimeweka tangazo hapo siku ya 4 hakuna majibu , mabwana /bibi shamba wote wako mijini au ofisini , mimi niko kiromo bagamoyo ninaekari 175 ngombe 80 na wanyama kibao hawa nafuga kama hobby tuu
sijuwi uanze kuzaa jamii mpya huko shamba na iishi maisha ya shamba na ndiyo uweze kupata watoto wako wengi ili wafanye kazi za shamba ???
 
kama ulivyosema hao ulionao ni wazembe , walevi, NI AIBU KWA TAIFA HILI KWAMBA WATU WANALIA AJIRA HAKUNA UKWELI HAKUNA MWAAJIRIWA , kuna umuhimu wa kutafakari hili , mimi nimeweka tangazo hapo siku ya 4 hakuna majibu , mabwana /bibi shamba wote wako mijini au ofisini , mimi niko kiromo bagamoyo ninaekari 175 ngombe 80 na wanyama kibao hawa nafuga kama hobby tuu
sijuwi uanze kuzaa jamii mpya huko shamba na iishi maisha ya shamba na ndiyo uweze kupata watoto wako wengi ili wafanye kazi za shamba ???

Ni vigumu sana kupata mfanyakazi wa kazi yoyote Tanzania kutoka mikoa ya Pwani, Tanga, Lindi na Mtwara hawafanyi kazi kwa ufanisi hata kama utamlipa mshahara mkubwa sana. Ni watu waongo, walaghai, wanataka pesa bila kutekeleza wajibu.
 
Aisee mi nipo tayari kua Farm Manager kama mshahara mzuri ni PM nifanye hyo kazi na nitakutafutia vijana wa ukweli wanaojua kazi za shamba kama 50 hvi kwa kuanzia weka mshaara kwanza unawalipaje? Kumbuka huu ni msimu wa mananasi.
 
Mkuu mpigie simu bwana Msunye Mnyankala 0653262810, anapatikana Fukayosi na hizo ndio shughuli zake...(NB: siwezi kumdhamini au kumsemea ufanisi na uaminifu wake, jiridhishe mwenyewe.)
 
Ungeacha namba za simu nili nimpe kijana mmoja ambaye ana uzoefu wa kazi hizo nafikiri ingekuwa bora zaidi.
Ahsante.
 
inawezekana mshahara wako ni mdogo sana na ndio maana umeajiri mateja...mikoani huko watu kibao hawana kazi
 
Mkuu mpigie simu bwana Msunye Mnyankala 0653262810, anapatikana Fukayosi na hizo ndio shughuli zake...(NB: siwezi kumdhamini au kumsemea ufanisi na uaminifu wake, jiridhishe mwenyewe.)

Mkuu nashukuru nitajaribu kuwasiliana naye basi..
 
Nguvu kazi Tanzania ni kaaazi kweli kweli, vijana wanalalamika hakuna kazi si mjini wala vijijini. Lakini ukiwapa kazi hawataki kufanya! Ninabiashara ya kuuza chips na ukipata kijana akifanya mauzo ya 20,000 tu kasepa! Huku maeneo ya Mbezi luisi watu wameacha kabisa ufugaji wa kuku na ngombe wa maziwa sababu ya uhaba wa wafanyakazi...kwa kweli ua nashindwa kuelewa watanzania tunataka nini!!!
 
Kuhusu mifugo niko vizuri sana, weka mshahara nione kama utanitosha kuhamia na kuishi bagamoyo.
 
kwenye mada yangu NATAFUTA MTU WA KULIMA MBOGA MBOGA ninampatia mtu hisa ya aslimia 60 lakini hakuna hata mmoja aliyethubutu kuijibu au kuchangia mada lakini wewe umetangaza ajira watu wanauliza ni kiasi gani utawalipa kwa vile anachojali ni huo mshahara tuu wewe ukivuna ukiliwa hajali mwisho wa mawezi anakinga mkono baada ya miezi tisa ukimwita na kumwonesha gharama za matumizi na ukamuuliza jee mimi muajiri nimepata faida gani hatakuwa najibu , hapo ujuwe wabongo wapo kulishwa na sio kujituma
 
Nakumbuka last two years nilitapeliwaga shamba maeneo hayo ya fukayosi.
Yaani niliuziwa shamba ambalo tayari lina mtu, nkakata tamaa kabisa na mambo ya kilimo.
Kuna jamaa mmoja anaitwaga BABA UBA angekusaidia kwa hilo, ngoja nitafute namba yake nitakurushia mkuu.
 
Nakumbuka last two years nilitapeliwaga shamba maeneo hayo ya fukayosi.
Yaani niliuziwa shamba ambalo tayari lina mtu, nkakata tamaa kabisa na mambo ya kilimo.
Kuna jamaa mmoja anaitwaga BABA UBA angekusaidia kwa hilo, ngoja nitafute namba yake nitakurushia mkuu.

Sawa mkuu...mashamba ni lazima upitie kwenye serikali ya kijiji bwana...

Nasubiria unarushie hiyo namba...
 
Kwa ufanisi mzuri wa shamba lako achana na vibarua, watakusumbua na kukutoa nyongo bure, unachotakiwa kufanya ajiri vijana kama watatu hivi wenye hulka ya kupenda kazi yao, watafanya kazi wakiwa na hakika ya kipato kwa mwezi kinakingika kiganjani, na watalitunza shama lako kama lao. Na wenyewe unaweza watafutia motisha ya eka moja au nusu vile wapande vya kwao ili wajisikie nyumbani na hata kuhamia na familia zao. Nakuambia hapo utawawekea mtego mzuri. Na unapowatembelea unawaachia mara kadhaa kilo moja moja ya nyama au kuwapelekea debe la sembe na dagaa utashangaa. Watalitunza shamba lako hadi ushangae huku ukitumia gharama ndogo kuliko kuwa na kundi la vibaka zaidi ya ishirini kwa msimu na wasifanye kazi yako kwa hakika.

Kumbuka mpango huo utakusaidia hao wafanyakazi kuwa walinzi wa proparty yako, vinginevyo usijeshtukia ukienda weekend fulani kukuta shamba lako limevunwa na wanaojua kuwahi mavuno ya awali, huku umeshanunua mazao uliyolima mwenyewe pale Tandale, Buguruni au Kariakoo, na mara nyingine pale upenyo wa uhindini soko la kisutu .
 
Kwani jamani watz gani wanapenda kazi za shamba.Tangu kilimo kiwe uti wa mgongo babu zetu walikufa na hawakuona manufaa ya kilimo. Leo kijana gani akakae shamba ili hali maisha bora yako mjini? Maisha ya shamba hayajaboreshwa hakuna maji hakuna umeme zana duni za kazi na Jura kidogo.Kwa nini wasinywe matapu tapu?
 
Back
Top Bottom