Natafuta Television au YouTube Chaneli inayoweza kuandaa makala za uchunguzi kama Jicho Pevu za Mohamed Ali wa KTN

Dr. Zaganza

JF-Expert Member
Jul 15, 2014
1,193
1,659
Habari wakuu,

Nimekuwa mpenzi wa kujisomea habari za magazeti na kuandika makala kwa zaidi ya miaka 25 sasa. Nimefanya tafiti ndogo, nimeona jamii imeshift toka kwenye magazeti na kwa sasa wanadeal zaidi na digital works kama e-newspaper, YouTube chanels n.k. Hivyo nimeandaa matukio 10 yalowahi tikisa Tanzania tangu mwaka 1951 mpaka mwaka 2010.

Hivyo natafuta Kituo cha Televisoin au chaneli watakaoweza kubadili kuwa digital na ziwe na msisimko kama au kupita ule wa kipindi cha Jicho pevu cha KTN cha Mohamed Ali kabla hajawa mbunge.

Simu 0713-039875
 
Wakuu tutengeneze ajira kwa vijana: Matukio mengi kama G55, Justine kasusura, Sarah simbaulanga n.k , kizazi kipya wanahitaji kuyaona kidigitali na sidhani kama yanamuathiri mtu
 
Wakuu tutengeneze ajira kwa vijana: Matukio mengi kama G55, Justine kasusura, Sarah simbaulanga n.k , kizazi kipya wanahitaji kuyaona kidigitali na sidhani kama yanamuathiri mtu
Ongeza na Stan Katabalo, Jombi et cetera🤣🤣🤣
 
Tengeneza makala zinazoonesha Mabeberu wanavyowatumia wanasiasa wa upinzani kuhujumu uchumi, makala zinazioonesha wakwepa Kodi, makala zinazoonesha wizi wa madini na wanyama pori, makala zinazoonesha biashara za mihadarati n.k Hapo, tutakuunga mkono. Kuwa Mzalendo kwa nchi yako.
 
Makala hizi hazitahusu siasa. Bali kukumbusha kizazi kipya matukio ya zamani yaani kama jumba la makumbusho kuna picha hadi za utumwa na wazungu wanakuja kuzitembelea bila kusema tumewatukana
 
Makala hizi hazitahusu siasa. Bali kukumbusha kizazi kipya matukio ya zamani yaani kama jumba la makumbusho kuna picha hadi za utumwa na wazungu wanakuja kuzitembelea bila kusema tumewatukana
Simulizi zitaanza soon
 
Back
Top Bottom