Natafuta Team ya Basketball iliyopo wilaya ya Temeke

Codename96

Member
Sep 17, 2020
90
85
Nianze kwa kuwaomba radhi mods na watu wengine ntakaowaudhi kwa kupost hapa.

Nimewaza sana jukwaa sahihi la kupost hii thread ila nimekosa. Nikaona nipost hapa nikiamini kuna watu wa kunisaidia.

Natafuta team ya Basketball, ambayo ntafanya nayo mazoezi na hatimaye niwe mmoja wa wachezaji wao tushiriki mashindani ya RBA au mengine makubwa. Kwa kuwa mimi nipo Temeke, ntashkuru sana kama training court ya hiyo team ntakayotajiwa itakuwa Temeke.

Asanteni.
 
Nenda Kurasini hapo...au kwa kuepuka usumbufu na upate information vizuri nenda kadunde hapo viwanja vya Sigara kisha utawauliza players kuhusu timu nyingi Temeke...maana sidhani kama unaweza tu kwenda timu kama JKT ukafanya mazoezi then ucheze nao ligi.
 
Nenda Kurasini hapo...au kwa kuepuka usumbufu na upate information vizuri nenda kadunde hapo viwanja vya Sigara kisha utawauliza players kuhusu timu nyingi Temeke...maana sidhani kama unaweza tu kwenda timu kama JKT ukafanya mazoezi then ucheze nao ligi.
Asante sana. Sigara ipo sehemu gani ? Maana huwa naisikia tu, sijawahi kwenda
 
Alright! Nimekuelewa. Kwahiyo kumbe kabla hujafika Tameko, kuna basketball court baada ya kuvuka shule ya Kibasila ?
Kama unatokea chuo Cha VETA kwenda Temeke shuka kituo kinaitwa Maduka mawili, ulizia ilipo sigara club ni hatua chache kutokea apo kituoni.
 
Ni beginner ila nina idea ya Basketball, kwa sababu nimetizama sana RBA na NBA kidogo sana. Urefu wangu ni 5.9 feet.
Safi sana, urefu mzuri kikubwa jitihada, mim nilianza kufundishwa na Mwalimu nikiwa na miaka 27. ilinichukua miezi sita kuanza kuaminika baada ya apo sikumbuki Kama nikiwa mzima niliwahi kukosa kucheza mechi yoyote mbaka naacha kucheza 2013.
 
Nenda Maduka Mawili Sigara TCC kuna Chang'ombe Boys,nenda Mgulani Jeshini,nenda Temeke Mikoroshini kuna Kituo cha Vijana Don Bosco kuna timu ya Basketball pale.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom