Natafuta soko la matofali

twaleeb

JF-Expert Member
Oct 13, 2016
231
83
Wadau naomba ushauri kwenu nataka kufungua kiwanda cha kufyatua matofali naomba mnijuze kuhusu jinsi ya kupata soko sababu mashine zote nimeshanunua tayari ss natafuta soko ntalipataje naombeni ushauri wenu
 
Mashine haziozi.... Ongeza nguvu ya mkwanja, fyatua tofali zako mwenyewe, anza kujenga nyumba za kuishi na za kibiashara( kama office ndogondogo but siziwe local esp mijini, markerts / commerial complex ndogondogo ili uchukue kodi hasa shem zisizo na masoko ama maeneo ya biashara, vilabu, stores ( maghala) ya bidhaa, na nyumba za kupangisha madonni sio walala hoi...!!) kwa kifupi jikite kwenye real estate, in long run utakua mbali sana kulinganisha na biashara ya tofali...!! Ndio utajiri wa dunia uko huku
 
Tx kwa ushauri ila ningependa sana kuuza hayo matofali huku nifanye na hio idea ulionipa
 
Wadau naomba ushauri kwenu nataka kufungua kiwanda cha kufyatua matofali naomba mnijuze kuhusu jinsi ya kupata soko sababu mashine zote nimeshanunua tayari ss natafuta soko ntalipataje naombeni ushauri wenu
usisikilize maneno ya watu...mm nipo kwenye sekta hii ya ujenzi...watu bado wana jenga kama zamani...sema biashara hii ya ujenzi huwa na yenyewe ina misimu yake...usisikilize maneno ya watu...nini ufanye...fanya hivi tafuta eneo ambalo shuhuri za ujenzi ndo zimeanza bado hakuja jengeka vya kutosha..kama kibaha ndani ndani..kiluvya tondoroni..makurunge..kidimu kibamba kwa uchache tu au eneo lolote unalo liona wewe halija jengeka sana.. weka ofisi yako...wapi watu wengi wanafeli..sehemu kubwa watu katika sekta hii wanafeli hawataki kutoa commision kwa watu wanao waletea wateja...ukiwa mbahiri rafiki yangu utaona matofari ya wenzio yana pitishwa mbele ya ofisi yako..nini ufanye tafuta mafundi wako kama 20..wambie wakikuletea mteja wa matofari kwenye kila tofari litakalo nunuliwa na mteja huyo utatoa shilingi 50 au 100...itategemea na wewe untka upate faida ya shilingi ngapi kwa kila tofari baada ya kutoa gharama zako..kingine hakikisha una canter yako au ya kukodi lkn maalumu kwa ajiri ya kubebea hizo tofari za wateja..tofari utakazo peleka hadi site kwa mteja zina bei yake na zile mteja atakazo amua kupeleka nwenyewe ziwe na bei yake..tafuta vijana wa kufyatua tofari uwe una walipa kwa kutwa au wa kudumu ni juu yako..pia uwe na duka la cement hapo hapo wateja wengi wanapenda kuchukua vitu kwa pamoja..yangu n hayo tu
 
Tx kwa ushauri ila ningependa sana kuuza hayo matofali huku nifanye na hio idea ulionipa

Tafuta contractors, tumia ushawishi wako wote, ingia nao mkataba kama material supplier kwenye site zao za ujenzi...!! Hawa wengi wana miradi mingi ya ujenzi asikwambie mtu hali ngumu, kila siku tunawaona wanapandisha mijengo mijini, wadogo kwa wakubwa...!! Hakikisha tofali zako zina ubora wa kujiridhisha kwa macho pia bila hata kupima...!!
 
Ndugu naomba namba yko ya cmu tuwasiliane
usisikilize maneno ya watu...mm nipo kwenye sekta hii ya ujenzi...watu bado wana jenga kama zamani...sema biashara hii ya ujenzi huwa na yenyewe ina misimu yake...usisikilize maneno ya watu...nini ufanye...fanya hivi tafuta eneo ambalo shuhuri za ujenzi ndo zimeanza bado hakuja jengeka vya kutosha..kama kibaha ndani ndani..kiluvya tondoroni..makurunge..kidimu kibamba kwa uchache tu au eneo lolote unalo liona wewe halija jengeka sana.. weka ofisi yako...wapi watu wengi wanafeli..sehemu kubwa watu katika sekta hii wanafeli hawataki kutoa commision kwa watu wanao waletea wateja...ukiwa mbahiri rafiki yangu utaona matofari ya wenzio yana pitishwa mbele ya ofisi yako..nini ufanye tafuta mafundi wako kama 20..wambie wakikuletea mteja wa matofari kwenye kila tofari litakalo nunuliwa na mteja huyo utatoa shilingi 50 au 100...itategemea na wewe untka upate faida ya shilingi ngapi kwa kila tofari baada ya kutoa gharama zako..kingine hakikisha una canter yako au ya kukodi lkn maalumu kwa ajiri ya kubebea hizo tofari za wateja..tofari utakazo peleka hadi site kwa mteja zina bei yake na zile mteja atakazo amua kupeleka nwenyewe ziwe na bei yake..tafuta vijana wa kufyatua tofari uwe una walipa kwa kutwa au wa kudumu ni juu yako..pia uwe na duka la cement hapo hapo wateja wengi wanapenda kuchukua vitu kwa pamoja..yangu n hayo tu
 
unatafuta soko wakati huna product .... ulitakiwa kufanya market research/study kabla ya kuamua ku-invest au kuanzisha biashara ..... sasa hivi zalisha tu upambane na masoko kwa kutumia creativity yako mwenyewe especially kwenye competive advantage na quality
 
Wewe weka kiwanda chako maeneo ambapo mji unaendelea kujengwa, wateja watakuja tu wenyewe bila shida
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom