Lidaku unautani na hiyo ishu?Ndugu LIDAKU upo serious kweli na hiyo biashara?
Kuna yeyote anaefahamu jinsi mafuta ya ubuyu yanavyotengenezwa??
Malila pitia hapa.
Mkuu Lidaku unauza kwa jumla ama kwa rejareja? Kama ni kwa jumla ni PM nikuunganishe na wateja faster.
Hizo ni bidhaa zinazouzika usiwe na shaka.
Kuna yeyote anaefahamu jinsi mafuta ya ubuyu yanavyotengenezwa??
Malila pitia hapa.
Jaman wadau mm ni kijana nimeamua kujiajiri ktk biashara ya kuuza mafuta ya ubuyu na asali,
kwa yeyote anayejua soko la hii kitu lilipo msaada tafadhari!
Hali ya ajira na maisha ni ngumu jamani tushirikiane kupambana nayo
Sijabahatika kuona yanavyokamuliwa, ila kwa kuwa yanatokana na mbegu, bila shaka yatakuwa yanakamuliwa kama alizeti. Mkuu Narubongo aliwahi zungumzia hili jambo kama sijakosea. ngoja nimsake kwa Pm ili aje na majibu.
Kuna yeyote anaefahamu jinsi mafuta ya ubuyu yanavyotengenezwa??
Malila pitia hapa.
Ubuyu mbegu zake ni nut kama ilivyo mchikichi nk. So jinsi ya ukamuaji ni kwa; kwanza ubuyu (tunda) lenyewe kuvunjwa, kutolewa ubuyu (unga) wake, kuutenga na mbegu na unga unakwenda kwenye process nyingine za kuchekechwa ili kutoa nyuzinyuzi n.k. Mbegu za uzalishaji mafuta hutoka zikiwa safi na huinguzwa kwenye mashine ya kukamulia na kuchuja vipande vidogovidogo(particles) na baadae hufungashwa (packed). Mafuta ya ubuyu kitaalamu hayatakiwi kufanyiwa refining zaidi ya kuchuja uchafu tu.