Natafuta soko la mafuta ya ubuyu na asali popote pale ndani na nje ya Tz

DullyJr

JF-Expert Member
Apr 10, 2011
11,398
2,000
Jaman wadau mm ni kijana nimeamua kujiajiri ktk biashara ya kuuza mafuta ya ubuyu na asali,
kwa yeyote anayejua soko la hii kitu lilipo msaada tafadhari!
Hali ya ajira na maisha ni ngumu jamani tushirikiane kupambana nayo
 
Crispin Nyoni

JF-Expert Member
Dec 11, 2012
413
195
Mimi nayahitaji mafuta ya ubuyu ila nijulishe matumizi yake.Nimesikia ni dawa.Je inatibu nini?Utujulishe nifungue soko
 
eucalyptos

JF-Expert Member
Jan 23, 2010
391
250
Mkuu Lidaku unauza kwa jumla ama kwa rejareja? Kama ni kwa jumla ni PM nikuunganishe na wateja faster.
Hizo ni bidhaa zinazouzika usiwe na shaka.
 
Crispin Nyoni

JF-Expert Member
Dec 11, 2012
413
195
Sasa huyu Lidaku tangu ameposti hii kitu hii hajarudi tena kutujibu.Labda hayuko siriasi na hiyo biashara.
 
Jun 26, 2009
67
95
Naona jamaa alibip sasa ngoja mie nipige. Mie ninayo nauza 40,000 kwa lita 1. My number is 0713 067 577 karibuni sana i see
 
Husninyo

JF-Expert Member
Oct 24, 2010
23,789
2,000
Kuna yeyote anaefahamu jinsi mafuta ya ubuyu yanavyotengenezwa??
Malila pitia hapa.
 
Last edited by a moderator:

MORIA

JF-Expert Member
Jul 1, 2011
699
500
Kuna yeyote anaefahamu jinsi mafuta ya ubuyu yanavyotengenezwa??
Malila pitia hapa.

Baada ya tunda la ubuyu kukobolewa na mashine unapatikana unga nao ni dawa, ndipo zile mbegu za ubuyu hukamuliwa na kupatikana mafuta ya ubuyu...fika railways gerezani kota nyumba namba 5, kuna duka la haya mafuta pamoja na asali mbichi, nimeishawahi yanunua hapo..
 
Last edited by a moderator:

theROOM

JF-Expert Member
Nov 4, 2010
946
250
Mkuu Lidaku unauza kwa jumla ama kwa rejareja? Kama ni kwa jumla ni PM nikuunganishe na wateja faster.
Hizo ni bidhaa zinazouzika usiwe na shaka.

Mkuu hapa ninayo mafuta hayo kwa bei ya jumla na rejareja. Kwa wanaohitaji wani-PM faster..
 
Malila

JF-Expert Member
Dec 22, 2007
4,705
2,000
Kuna yeyote anaefahamu jinsi mafuta ya ubuyu yanavyotengenezwa??
Malila pitia hapa.

Sijabahatika kuona yanavyokamuliwa, ila kwa kuwa yanatokana na mbegu, bila shaka yatakuwa yanakamuliwa kama alizeti. Mkuu Narubongo aliwahi zungumzia hili jambo kama sijakosea. ngoja nimsake kwa Pm ili aje na majibu.
 
Malila

JF-Expert Member
Dec 22, 2007
4,705
2,000
Jaman wadau mm ni kijana nimeamua kujiajiri ktk biashara ya kuuza mafuta ya ubuyu na asali,
kwa yeyote anayejua soko la hii kitu lilipo msaada tafadhari!
Hali ya ajira na maisha ni ngumu jamani tushirikiane kupambana nayo

Siku nyingine inabidi ujaze nyama tangazo lako. Hujasema unaweza kuingiza sokoni kiasi gani, hujasema bei yako na location ulipo au ilipo mali, je hiyo asali ni ya nyuki gani, wadogo au wakubwa na je ni mbichi na je tayari umesha-park. Kizazi cha sasa kinataka kila kitu kiwe peupe.
 
bagamoyo

JF-Expert Member
Jan 14, 2010
15,228
2,000
Thailand wao wanauza ukwaju kama ulivyo toka mtini na kuuhifadhi ktk ma-box ya viwango vya kimataifa kwa uuzaji wa rejareja bara la Ulaya na Marekani.

Hata wewe mdau ungeweza kufungasha ubuyu-ghafi ktk vifuko vya plastiki na kuhifadhi ktk maboski yenye viwango vya kimataifa kwa ajili ya uuzaji wa rejareja ktk maduka na masupamaketi badala ya kwenda mbali kupata mafuta ya ubuyu.
 
Husninyo

JF-Expert Member
Oct 24, 2010
23,789
2,000
Sijabahatika kuona yanavyokamuliwa, ila kwa kuwa yanatokana na mbegu, bila shaka yatakuwa yanakamuliwa kama alizeti. Mkuu Narubongo aliwahi zungumzia hili jambo kama sijakosea. ngoja nimsake kwa Pm ili aje na majibu.

any feedback? au ulimkosa?
 
eucalyptos

JF-Expert Member
Jan 23, 2010
391
250
Kuna yeyote anaefahamu jinsi mafuta ya ubuyu yanavyotengenezwa??
Malila pitia hapa.

Ubuyu mbegu zake ni nut kama ilivyo mchikichi nk. So jinsi ya ukamuaji ni kwa; kwanza ubuyu (tunda) lenyewe kuvunjwa, kutolewa ubuyu (unga) wake, kuutenga na mbegu na unga unakwenda kwenye process nyingine za kuchekechwa ili kutoa nyuzinyuzi n.k. Mbegu za uzalishaji mafuta hutoka zikiwa safi na huinguzwa kwenye mashine ya kukamulia na kuchuja vipande vidogovidogo(particles) na baadae hufungashwa (packed). Mafuta ya ubuyu kitaalamu hayatakiwi kufanyiwa refining zaidi ya kuchuja uchafu tu.
 
thanx, nahitaji kilo ngapi za ubuyu kupata mafuta lita moja?
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom