Natafuta Shule ya awali ya mtoto wa miaka miwili na nusu!

tete'a'tete

JF-Expert Member
Feb 10, 2010
472
62
Wana Jf na imani mu buheri wa afya!

Nina binti yangu ana miaka miwili na nusu ananisumbua sana kuhusu shule. Natafuta shule ya awali Nursery school English medium ambayo ni nzuri na yenye kuwafundisha hawa watoto maadili! ninaishi Sinza hapa Dar yeyote mwenye kujua shule yeyote anisaidie! kwani nataka aanze mwezi ujao wa saba.

Natanguliza shukrani zangu za dhati...
 
Jaribu St Columbus ipo Makongo Juu haina madoido ila mtoto anafundishwa vyema
 
Jaribu New Era Nursery School Upanga

education weaved in morals
 
Shule iliyopo Maeneo ya Bunju itakufaa?

Mkuu tuangalie na issue ya transport charges! na kumchosha mtoto vilevile kwani umri bado ni mdogo sana binamu! miaka miwili na nusu! by the way mtoto anatakiwa aanze nursery akiwa na umri gani wakuu??
 
Hivi mtoto anatakiwa aanze nursery akiwa na umri gani?

Wangu ana timiza miaka 3 this June, lakini naona kama bado mdogo sana.

Hebu tusaidieni wazoefu katika haya mambo!!
 
Wangu ana timiza miaka 3 this June, lakini naona kama bado mdogo sana.

Inategemea na mazingira unayoishi. Mimi wangu aliaanza shule (nusery) akiwa na mwaka mmoja na miezi tisa. Shule ilikuwa inapokea watoto kuanzia mwaka mmoja na miezi sita!

Kwangu mimi cha muhimu ilikuwa ni mtoto apate fursa ya kujichanganya na watoto wengine kwa sababu nyumbani alikuwa anakaa ndani muda mrefu na hata nafasi ya kucheza kwa uhuru ilikuwa finyu sana na hivyo kuzuia maendeleo yake. Kama ujuavyo watoto wa umri huo kila kitu anataka kujaribu na kila anachogusa anaambiwa 'acha', so niliona vema kumpeleka shule katika umri huo mdogo.

Lakini ni muhimu kuzingatia umbali na mazingira ya shule husika (nenda kwenye shule husika, tizama mazingira yao, sehemu za kucheza, kulala, choo nk).

Ningekushauri kuchagua shule iliyopo karibu kabisa na unapoishi ili mtoto asitumie muda mrefu barabarani.
 
Inategemea na mazingira unayoishi. Mimi wangu aliaanza shule (nusery) akiwa na mwaka mmoja na miezi tisa. Shule ilikuwa inapokea watoto kuanzia mwaka mmoja na miezi sita!

Kwangu mimi cha muhimu ilikuwa ni mtoto apate fursa ya kujichanganya na watoto wengine kwa sababu nyumbani alikuwa anakaa ndani muda mrefu na hata nafasi ya kucheza kwa uhuru ilikuwa finyu sana na hivyo kuzua maendeleop yake. Kama ujuavyo watoto wa umri huo kila kitu anataka kujaribu na kila anachogusa anaambiwa 'acha', so niliona vema kumpeleka shule katika umri huo mdogo.

Lakini ni muhimu kuzingatia umbali na mazingira ya shule husika (nenda kwenye shule husika, tizama mazingira yao, sehemu za kucheza, kulala, choo nk).

Ningekushauri kuchagua shule iliyopo karibu kabisa na unapoishi ili mtoto asitumie muda mrefu barabarani.

Asante kwa ushauri!!
 
Kunashule pale Upanga seaview karibu na ile clinic ya moyo ya Dr, Lwakatare mitaa ya kina Mzee Malecela ni nzuri jina la hiyo chule sina uhakina Ni Patricia ama mwenye hiyo shule anaitwa hivyo kuna rafiki yangu alimpeleka mwanae hapo kwakweli nimefurahishwa na maendeleo ya huyo mtoto noow ametimiza miaka 3 alimwanzisha mapema now anajua kila kitu
 
Asante mkuu nitaenda kuiangalia!
 
Kutafuta shule za awali imekuwa changamoto kwa wazazi sana kutokana na shule zenyewe kuwa mbali halafu gharama kubwa. Nway hope Ndugu t'a't atapata shule nzuri kwa mwanae na wale wengine wote wenye hitaji kama yeye
 
Jirani Mbona hujasema fee isizidi kiasi gani?Hicho ni kipimo haswa. Lakini ukipata shule yenye kufundisha maadili mema na elimu bora ndio cha muhimu.Majina wakati mwingine yanaongeza gharama za bure. Ni kweli hiyo Patricia karibu na kwa Dr.Rwakatare ni excellent. Lakini nadhani St. Joseph kama unataka combination ya hivyo vitu 3 basi ni bora zaidi na cha kufurahisha waalimu, wamesomea kufundisha watoto wa Nursery. Sio mtoto anakuja anaimba ABCD..... ukimuonyesha Z iko wapi haijui au anakuimbia 1,2...1000 ukimuandikia 55 haijui,au mtoto anasoma lakini ukiangalia mpangilio wa chumba chake,vitu vyake,table manner etc zero(Kumbe waalimu ni University leavers waliokosa kazi). Nenda St.Joseph ujionee fee nadhani kama 600K/year jumlisha transport 45K/month lakini una uhuru wa kumpeleka mwenyewe-ukikasahau kwa kukaa kwenye JF utakuta kameliwa na sisimizi nje pale-ahaaaaaaaaaaaha.
 
Mkuu asante nimewasiliana nao wanasema ni 775,000 kwa term kwa hiyo term tatu ni 2,325,000 ada yao...

Nina mtoto anasoma hapo beby class, ada ni 310,000 kwa muhula mmoja, na wana mihula mitatu.

775,000 inaweza kuwa wakati wa kuanza kwani kunakuwa na michango mingi zaidi ya ada kama vile kuchangia majengo, uniforms etc. Mwanangu first time nilimlipia 550,000 kwakati ada ilikuwa ni 210,000 kwa muhula.

Upungufu wa shule hii ni kuchanganya watoto wadogo na wakubwa kwenye parade na pia mabasi ya shule, halafu eneo lao ni finyu sana.
 
Sio mtoto anakuja anaimba ABCD..... ukimuonyesha Z iko wapi haijui au anakuimbia 1,2...1000 ukimuandikia 55 haijui,au mtoto anasoma lakini ukiangalia mpangilio wa chumba chake,vitu vyake,table manner etc zero
Ni kweli, serious problem na hii ipo sana kuna shule ni watoto kuimba tu na nyimbo zenyewe hkuna mpya ni zile zile ambazo mtoto anazisikia kila siku.
 
Back
Top Bottom