Natafuta shule nzuri kitaaluma kwa kidato cha tano

askarikambi

JF-Expert Member
Dec 22, 2013
246
263
Habari bandugu,

First born wangu amemaliza kidato cha nne na amepata div. II ya point 20. Ni mvulana na anataka comb. ya EGM.

Najua anaweza kupata shule ya Serikali, lakini natafuta ya private ili kama akipangiwa shule "yenye kutia mashaka kitaaluma" basi nimpeleke private kama nilivyofanya kwenye o'level.

Maombi yangu kwenu, naomba mnisaidie kunitajia shule nzuri kitaaluma za a'level za boys katika mikoa ya Dar, Pwani, Morogoro, Tanga, Kilimanjaro na Arusha ambazo ada yake haizidi sh. 3.5 mil.

Natanguliza shukrani na kila la kheri kwa siku ya wapendanao.
 
feza boyz
Hapo nimeenda, wanataka Mil. 9 na elfu 50 kwa form five na 8.5 mil atakapoingia f. Six.
Uwezo wangu ni mil 3.5 hata ikizidi kidogo sio mbaya. Si unajua vyuma vimekaza, hata mdogo wake anayekula Mil 3.7 nimemwambia ikiongezwa tu unahama shule. Ndio najikuna hadi hapo.
 
Kuna shule mkoa wa pwani inaitwa Ali Hassan Mwinyi au ifupi Ahames Ni nzuri na matokeo yao Ni mazuri.Form unachukulia hapa kawe karibu na golf course ya Jeshi.
 
Tunaomba mtuelekeze pia shule nzuri zenye ada nafuu kwa wasichana Form Five wapendwa. Huyo anayetafuta ya wavulana ajaribu pia Eagles Boys Bagamoyo.
 
Back
Top Bottom