Check PMHabari wadau.
Mimi ni Mtanzania niliyebahatika kupata elimu katika nchi mbalimbali za Bara la Ulaya. Baada ya kumaliza elimu yangu nimerejea nchini kujenga taifa.
Kufuatia changamoto ya ajira nimeonelea nichukua route ya kujiajiri. Baada ya kufanya utafiti wa kina, nimejiridhisha kuwa mradi wa Ufugaji wa Nguruwe kibiashara (Commercial Piggery Project) unaweza lipa katika muda mfupi.
Lengo langu sio tu kufuga Nguruwe, bali kufuga na kuongezea thamani bidhaa nitakazizozalisha ili kuuza bidhaa hizo Kwenye upper-end market.
Nafahamu wapo watanzania wenye mitaji ila hawana muda wa kufanya mradi wa aina hii. Mimi nina ardhi kubwa kando ya mto Ruvu, access ya kupata soko zuri na elimu ya kutosha ambayo ninatarajia kuitumia katika mradi huo.
Hivyo nakaribisha wenye mitaji ya hali (Relevant education) na Mali (Fedha) ktk kufanikisha mradi huu.
Mambo yote yataenda kisomi/kisheria.
Karibuni sana