Natafuta Serious Partner wa Kuanzisha Mradi Mkubwa Wa Nguruwe Tanzania

Waanzilishi wa dini ulimwenguni (KANISA KATOLIKI) ni wabobevu katika haya masuala kuna vitabu vipatavyo tisa (9) vya Mungu ambavyo nimevipata viliondolewa katika Bible navipitia sasa hakika kuna mambo ya kushangaza na nina habari vipo vingine maelfu ambavyo haviko published mtandaoni vinapatikana katika Library ya mambo ya historia ya ukristo mjini Roma.
Hawa watu wanajua kinaganubaga kwanini wameruhusu hadi unywaji wa pombe kwa kiasi kwa kuzingatia Misingi ya ukristo,nakupa mfano wakristo wote kasoro madhehebu machache tunakunywa " Mvinyo" Divai kama inshara ya damu ya Yesu ila tunakunywa kwa kiasi.
Umeanza kwa kuniambia "Uraibu" ni neno la kiarabu sipingi kwa kuwa kiswahili kina maneno mengi ya lugha mbalimbali ikiwemo kireno tuna neno "Gereza" ni kireno na mengine mengi.
UMEULIZA SWALI ZURI SANA KUWA POMBE NAYOIHALALISHA HAINA URAIBU? jibu inawo uraibu ndio maana tunatakiwa tuinywe kwa kiasi, Sukari ina uraibu ambayo (Unaitumia kila siku), Kuendesha gari kuna uraibu, Kusoma sana kuna uraibu, JAMBO LOLOTE LINA URAIBU.
Sasa basi kwa kumalizia haka kamjadala nilikuuliza Swali lakini haukunijibu ukafunika tafdhali naomba unijibu.
Wewe haujawahi kuzini, je wewe haujawahi kuiba, je wewe haujawahi kula samaki wasio na magamba (kambare na ndugu zake), je wewe haujawahi kula wanyama wasio na kwato ambazo hazijagawanyika au wasio cheuwa?
Kama hivyo vitu hujawahi kuvifanya "HAKI YA MUNGU NAKUWA MUISLAMU NAKUPA MAWASILIANO YANGU UNIPELEKE KWA SHEIKH NIKASILIMU NA UNIREKODI KAMANDA NABADILI DINI"
Ila kama umewahi kufanya Unakula Samaki wasio na magamba na wanyama wengine waliokatazwa ila nguruwe humtaki basi wewe ni "MNAFIKI" na wanafki ni walioongoka

Mkuu, mimi naona unatafuta njia ya kubadilisha mjadala tu, kwani mjadala mkuu ni uharamu na madhara ya kula nyama ya nguruwe basi.

Nashangaa umeugeuza huu mjadala kuwa mahakama ya kuhukumu makosa,.sasa kama nilitenda au sijatenda au wewe kufanya au kutofanya hayo makosa hiyo inabatilisha vipi uharamu wa kula nyama ya nguruwe ??--- ukweli utabaki palepale kwamba Mungu katukataza kula nyama ya nguruwe kwa sababu inayo madhara mabaya kwetu ("acute diverse effects"). na moja ya madhara ni kuambukizwa "USHOGA" homo-sexuality kwa wanaume.
 
nimefuga nguruwe kwa miaka kadhaa maeneo ya songea peramiho sehemu ambayo pumba bei zake ni za wastani..... lakn imekuwa ngumu kuiona faida .ukiwa unajitaidi kufuga ndani ya mda mfupi maana ake inabdi usitegemee pumba tu.
ili nguruwe akue kwa kasi lazma uwe na mashudu, pig mixture na virutubisho vingine plus ivyo vyote maana ake unaongeza production cost. kwa experience yangu unaweza uza nguruwe wa kilo 80 kwa ndani ya mwaka. hapo huyo nguruwe asisumbuliwe na magonjwa yoyote yaani uwe makini na tiba hasa za minyooo. ukiteteleka kidogo nikaz sana kuendelea na kasi ile ile ya ukuaji.

hawa nguruwe wapo wa aina tofauti kuna walio na nyama nyingi na wengine mafuta mengi, wanyama nyingi mara nyingi hawa nenepi zana wanakuwa na unene wa wastani. huku kwetu nguruwe aina fulani hv ambao wanakuwa na rangi nyeusi na nyeupe nmara nyingi kichwani nyeusi na mgongoni nyeupe na mgongoni kwenda miguuni weusi hawa wana wananyama nyingi lakin wana kuwa taratibu,
nguruwe hupenda zaidi pumba za mahindi kuliko za mpunga (za mpunga ni ngumu katika mmeng'enyo ) sasa kuna vitu inabidi ukaechini uwe pnge vzuri zaidi nichakula ambacho ni beei zake upnda mara kwa mara hasa maindi yanapo patikana kwa shida. pumba hutumika karibia na wanyama wote wa fugwao.
kwa ushauri wangu ni vizuri ukapata chakula mbadala cha kuliko kutegemea pumba hasa maeneo ya mjini
 
Waanzilishi wa dini ulimwenguni (KANISA KATOLIKI) ni wabobevu katika haya masuala kuna vitabu vipatavyo tisa (9) vya Mungu ambavyo nimevipata viliondolewa katika Bible navipitia sasa hakika kuna mambo ya kushangaza na nina habari vipo vingine maelfu ambavyo haviko published mtandaoni vinapatikana katika Library ya mambo ya historia ya ukristo mjini Roma.
Hawa watu wanajua kinagaubaga kwanini wameruhusu hadi unywaji wa pombe kwa kiasi kwa kuzingatia Misingi ya ukristo,nakupa mfano wakristo wote kasoro madhehebu machache tunakunywa " Mvinyo" Divai kama inshara ya damu ya Yesu ila tunakunywa kwa kiasi.
Umeanza kwa kuniambia "Uraibu" ni neno la kiarabu sipingi kwa kuwa kiswahili kina maneno mengi ya lugha mbalimbali ikiwemo kireno tuna neno "Gereza" ni kireno na mengine mengi.
UMEULIZA SWALI ZURI SANA KUWA POMBE NAYOIHALALISHA HAINA URAIBU? jibu inawo uraibu ndio maana tunatakiwa tuinywe kwa kiasi, Sukari ina uraibu ambayo (Unaitumia kila siku), Kuendesha gari kuna uraibu, Kusoma sana kuna uraibu, JAMBO LOLOTE LINA URAIBU.
Sasa basi kwa kumalizia haka kamjadala nilikuuliza Swali lakini haukunijibu ukafunika tafdhali naomba unijibu.
Wewe haujawahi kuzini, je wewe haujawahi kuiba, je wewe haujawahi kula samaki wasio na magamba (kambare na ndugu zake), je wewe haujawahi kula wanyama wasio na kwato ambazo hazijagawanyika au wasio cheuwa?
Kama hivyo vitu hujawahi kuvifanya "HAKI YA MUNGU NAKUWA MUISLAMU NAKUPA MAWASILIANO YANGU UNIPELEKE KWA SHEIKH NIKASILIMU NA UNIREKODI KAMANDA NABADILI DINI"
Ila kama umewahi kufanya Unakula Samaki wasio na magamba na wanyama wengine waliokatazwa ila nguruwe humtaki basi wewe ni "MNAFIKI" na wanafki ni walioongoka
Unaelewa maana ya "Uraibu"??--- hili ni neno halisi la kiarabu lenye maana ya kiingereza "addiction"--- sasa, hiyo pombe uliyojihalalishia haina uraibu?!!.
Mkuu, mimi naona unatafuta njia ya kubadilisha mjadala tu, kwani mjadala mkuu ni uharamu na madhara ya kula nyama ya nguruwe basi.

Nashangaa umeugeuza huu mjadala kuwa mahakama ya kuhukumu makosa,.sasa kama nilitenda au sijatenda au wewe kufanya au kutofanya hayo makosa hiyo inabatilisha vipi uharamu wa kula nyama ya nguruwe ??--- ukweli utabaki palepale kwamba Mungu katukataza kula nyama ya nguruwe kwa sababu inayo madhara mabaya kwetu ("acute diverse effects"). na moja ya madhara ni kuambukizwa "USHOGA" homo-sexuality kwa wanaume.
Hebu toen ujinga wenu hapa, anzishen thread yenu mjadili haya
 
Hebu toen ujinga wenu hapa, anzishen thread yenu mjadili haya
Ahsante Kwa kuliona hili. Huyu jamaa Kwa kweli ameamua ku-introdcuce noises humu. Naunga mkono hoja yako, nashauri akafungue thread mpya kuhusu hoja zake.
 
hahqhaa am sorry my dear nimekupa dislike..Mie Nguruwe naiona ni zaidi ya Kharamu...siwez...uwii..bora niuze hata bangi aisee.ila sio nguruwe.kwanA hapa nimesisimkaaa😐😐!

Mkuu mimi nikiwa vizuri mfukoni na sina visafari nawekaga bili ya mwezi mahali .

Mimi siwezi acha kula nguruwe.
 
Kufuatia maoni ya wadau waliosoma uzi huu imenipasa nitoe japo a concept note.

Kiufupi lengo kuu la mradi ni Kuanzisha ufugaji wa Nguruwe kibiashara - Commercial Piggery Project (as opposed to traditional/subsistence Piggery Project). Features za commercial Piggery project include

1. Profitable Business
2. Energy-saving technology
3. Ecologically clean production
4. Humane attitude to pigs

Nimechagua kufuga Nguruwe badala ya wanyama wengine Kwa sababu zifuatazo

1. Nguruwe ana relatively low feed conversion ratio (FCR) ambayo ni nzuri mana inaelezea ufanisi Mkubwa alionao wa kuzalisha nyama toka Kwenye chakula ana chokula. Yaani anatumia chakula kidogo kuzalisha Kilo moja ya nyama.

2. Nguruwe wanakua haraka (Wana high growth rate). Nguruwe aliyetunzwa vzr anaweza kuwa na kilo Kati ya 100 -110 ndani ya miezi 6.

3. Wanabeba mimba Kwa muda mfupi Sana i.e. three months, three weeks and three days= in total 114 days. Na wanaweza kuzaa Kwa wastani watoto 10-14 Kwa mzao. Hii inategemea ubora wa mbegu, chakula na afya yao. Nguruwe pia anaweza kuzaa mara 2 Kwa mwaka.

4. Nyama yake ni White meat, hivyo ni nzuri Kwa afya na wateja wengi wanaipenda.

5. Kwa Tanzania wafugaji wa kibiashara ni wachache na kimsingi wameshindwa kumeet market demand. Hivyo Kuna soko kubwa Sana nchini ambalo Kwa sasa linalazimika kuagiza nyama hiyo nje ya nchi mana hatujaweza bado zalisha Bidhaa wanzozihitaji.

6. Wazalishaji karibu wote wamejikita katika kuuza raw pork meat/live animals (nguruwe mzima mzima). Hivyo kuna uhaba Mkubwa Sana Sana wa Bidhaa za Nguruwe zilizoongezewa thamani kama specialized and packed pork cuts, Bacon, Smoked pork meat, pork sausages etc.

Kwa kutambua haya. Ndio nikawiwa kutafuta wenzangu wanaopenda kuungana nami ili tuchangamkie fursa hii.

Gharama za ufugaji wa Nguruwe.

Kwa ujimla gharama zina tofautiana Sana kulingana na namna unavyoendesha ufugaji wako. Gharama kubwa ktk ufugaji wa Nguruwe, ukiachia Ujenzi wa Banda la kisasa, zipo kwenye chakula. Japo kuna wataalamu wanaotoa gharama za makadirio, ukweli ni kwamba si rahisi kuwa realistic Kwenye makadirio hayo.

Chakula:

1) Nguruwe ana nyonya Kwa muda wa week 4 (siku 28). Baada ya hapo anapaswa kutengwa na mama yake na kuwekwa Kwenye Banda la kukulia ili kumpa mama yake muda wa kuzalisha joto ili apandwe tena. Nguruwe no Omnivore (hula nyama na majani, nafaka/mbegu) hivyo inapaswa umlishe chakula chenye mchanganyo na virutubisho vyote na ikifaa iwe katika form ya Pellets.

Baada ya kunyonya hula chakula cha uzito mbalimbali kulingana na uzito wao mfano.

2) Nguruwe mwenye 10-17kg anapaswa kula 0.8 kg Kwa siku

3) Nguruwe mwenye 18-29Kg anapaswa Kula 1kg Kwa siku

4) Nguruwe mwenye 30-40kg anapaswa Kula 1.5kg Kwa siku.

5) Nguruwe mwenye 40-60 kg anapaswa Kula 2kg Kwa siku.

6) Nguruwe mwenye 61-80kg anapaswa Kula 2.5kg Kwa siku.

7) Nguruwe mwenye 81-100kg anapaswa Kula 3kg Kwa siku.

8) Nguwure zaidi ya 100kg na mwenye mimba anapaswa Kula 6 kg.

Inashauriwa Nguruwe auzwe chini ya 120kg maana baada ya bado anakuwa na high feed conversion ratio. Anatumia chakula kingi kutengeneza kilo moja ya nyama hivyo ni hasara Kwa mfugaji.

Naweza kudadavua zaidi Kwa interested and serious partners baadaye.

Bei ya Mbegu (Breeding Stock)

Bei ya Nguruwe wa mbegu pia inategemea unahitaji mbegu aina gani, wa ukubwa gani na unamtoa wapi. Kuna aliyetaka niuzia wa mwezi mmoja Kwa 100,000 na wa miezi sita kwa 600,000 Dar Es Salaam. Hivyo bei zina range hapo.

Soko la Nguruwe.

Soko ni kubwa Sana kuanzia soko la wateja wa kawaida hadi mahotelini. Wakati kilo 1 ya raw meat inauzwa Kwa TZS 8000 Kwa bei ya rejareja, Kwenye mahoteli ambako wananunua Bidhaa zilizoongezewa dhamani, kilo moja ya Bidhaa hiyo huuzwa hadi TZS 30,000.

Kwenye ufugaji ninaotaka kuufanya Mimi target yangu ni Soko la mahotelini.

Nini kipo tayari Hadi sasa

Ninaye mtaalam wa kuongezea thamani yaani kufanya smoking, kufanya hizo pork cuts, kutengeneza bacon n.k.

Nina shamba zaidi ya heka 3 lipo mita 600 kando ya mto Ruvu, Mlandizi na umeme haupo mbali. Hivyo suala la Maji na umeme Kwenye shamba Hilo ni rahisi.

Nina kijana wa kazi mmoja na Mimi mwenyewe ntakuwa naishi hapo hapo Shambani muda mwingi.

Nina wataalamu wa magonjwa ya Nguruwe wawili ambao wameshaonesha interest ya kushirikiana nami katika hii project.

Vinavyokosekana Hadi sasa.

Mtaji Kwa maana ya Fedha za kujenga Banda la kisasa la kuaccomodate breeding stock ya Nguruwe angalau 50 na Banda la kutunzia watoto, kujenga processing unit/house, kuweka uzio eneo la banda, kununua chakula na breeding stock 50 pigs, kutengenezea cold room/chiller, smoker, kununua machine za cutting, vacuum na vifungashio, kujisajiri TFDA na TBS.

Kama Kuna maswali zaidi nitaendelea Kujibu.

Kaka binafsi nakusifu kwa uthubutu na utayari,
Umeelezea vizuri na kwa kifupi,
Nakutakia kila la kheri Bila shaka utapata mdau sahihi wa kukamilisha hili.
 
Mkuu mimi nikiwa vizuri mfukoni na sina visafari nawekaga bili ya mwezi mahali .

Mimi siwezi acha kula nguruwe.

Hahahaha so. daily unakula kitimoto..dah..mm ananitia kinyaa..mm jaman niitie mbuzi ht km 20kms nakujà😁😁..napenda balaa mbuzi jaman..khaa!
 
Hahahaha so. daily unakula kitimoto..dah..mm ananitia kinyaa..mm jaman niitie mbuzi ht km 20kms nakujà😁😁..napenda balaa mbuzi jaman..khaa!

Mbuzi choma kilo za kutosha na kaaugali kadogo.

Mkuu usijilamu mambo mengi ni zao la umezaliwa wapi ,umekulia dini au dhehebu gani na pia aina ya wazazi .

Huenda nam ningezaliwa mfano familia ya kisabato ningekuwa kama wewe.

All in all ukiwa na hela kula unachopenda.
 
Hii sentensi ya mwisho umemaliza..!natak nije niende Mwanza ...nikale samaki had wanikome...Mungu anipe pumz tu..
 
Habari wadau. Leo tutakuwa na kikao cha Kwanza cha uanzishwaji wa hii project. Kikao kitaanza saa 11:00 jioni eneo la Tank Bovu Mbezi Beach, DSM. Ukihitaji details zaidi, please contact me privately. Nyote mnakaribishwa.
 
gaha
Hongera ndugu kwa mawazo mazuri ya kijasiriamali!
Una malengo makubwa na mazuri. Sisi ni wazoefu wa miaka mingi katika ufugaji.Inafaa kuanza kidogo kwa malengo makubwa(Start Small Dream big).
Waweza tufuata kwenye page yetu ya instagram;nna imani kuna mengi utajifunza katika ndoto yako:
 
Mkuu, mimi naona unatafuta njia ya kubadilisha mjadala tu, kwani mjadala mkuu ni uharamu na madhara ya kula nyama ya nguruwe basi.

Nashangaa umeugeuza huu mjadala kuwa mahakama ya kuhukumu makosa,.sasa kama nilitenda au sijatenda au wewe kufanya au kutofanya hayo makosa hiyo inabatilisha vipi uharamu wa kula nyama ya nguruwe ??--- ukweli utabaki palepale kwamba Mungu katukataza kula nyama ya nguruwe kwa sababu inayo madhara mabaya kwetu ("acute diverse effects"). na moja ya madhara ni kuambukizwa "USHOGA" homo-sexuality kwa wanaume.

Mmmh!! Unaweza kuweka ushahidi wa kimaandishi kutoka vyanzo thabiti nasi tukarejea? Tafadhali
 
Back
Top Bottom