FaizaFoxy
Platinum Member
- Apr 13, 2011
- 92,870
- 109,164
Nguruwe ni nyama tamu sana kwa kweli, kuhsu madhara, kitu chochote ukikitumia kupita kiasi kina madhara, hata nyama ya ng'ombe ina madhara... tusivuke mipaka, inapoishia haki yako, ni mwanzo wa haki ya mtu mwingine
Wanyama najisi na wasio najisi
(Kumb 14:3-21)
1Mwenyezi-Mungu aliwaambia Mose na Aroni, 2“Wawaambie Waisraeli hivi: 3Kati ya wanyama wote duniani, mmeruhusiwa kula mnyama yeyote mwenye kwato zilizogawanyika sehemu mbili na ambaye hucheua. 4Lakini msile mnyama yeyote ambaye hucheua lakini kwato zake hazikugawanyika sehemu mbili, au ambaye kwato zake zimegawanyika lakini hacheui. Msile ngamia, kwani hucheua lakini kwato zake hazikugawanyika sehemu mbili. Kwenu huyo ni najisi. 5Pelele msimle; yeye hucheua lakini kwato zake hazikugawanyika; kwenu huyo ni najisi. 6Sungura msimle; yeye hucheua lakini kwato zake hazikugawanyika; kwenu huyo ni najisi. 7Nguruwe msimle; ana kwato zilizogawanyika lakini hacheui; kwenu huyo ni najisi. 8Kwa sababu wanyama hao ni najisi msile nyama yao wala msiguse mizoga yao.