Natafuta sehemu ya kujitolea(internship), ajira au shughuli yoyote ya kuniweka bize

Mimi naomba nimtetee mleta uzi. Unajua kuna baadhi ya ndugu au jamaa zetu anapokuona unauwezo au kipaji fulani cha kupiga kazi fulani anaangalia unamadhaifu gani au unamapungufu gani then anapretend kuwa anakusaidia umsaidie ila ukitazama kiuhalisia ni wewe unamsaidia yeye.....


Nitakupa mfano, kuna rafiki yangu, alikuwa ana bro wake anaishi US, huyu swahiba alikuwa amemaliza chuo level ya degree na alikuwa ameshapata kazi kwenye kampuni analipwa laki 8 kwa mwezi.

Changamoto aliyokuwa nayo ni alikuwa anasomesha watoto wawili wa dada zake na anasimamia bili za home kwa bi mkubwa wake kwa kiasi kidogo. Yeye hakuwa na familia bado.

Sasa alipokuwa akiwasiliana na huyu ndugu yake aliyepo mbele walikuwa wakizungumza maswala mbali mbali ya kiamaisha. Maswala ya uchumi biashara na uwekezaji. Jamaa alikuwa na ndoto ya kufanya biashara ya kuuza nafaka na mazao ya kilimo. Yule ndugu yake wa nje alipomsikia ametoa hilo wazo akamuunga mkono na kupenda kujua zaidi.

Walizungumza sana na yule ndugu wa nje akainyesha interest ya kupenda kushirikiana nae huyu mshikaji waifanye hiyo biashara kuwa kweli.

Basi jamaa alikuwa tayari ameshaanza kusajiri jina la kampuni na alishatafiti baadhi ya vitu na mahitaji ya kuanzia. So changamoto kwa mshikaji ilikuwa ni ataachaje kazi na kuendelea na biashara kabla hajasave kiasi cha akiba ya kumsapoti kwenye biahsara na maisha. Kazi alipofanya alikuwa ana miezi 9 toka kuanza......so jamaa alikuwa na mtihani.

Huyu ndugu yake wa marekani akamwambia kama vipi aache kazi halafu atakwenda kaa kwenye nyumba yake ambayo ipo wazi na atatumia gari yake ndogo ambayo ipo kwa ndugu yake mwingine. Na atamsaidia kulipia hao watoto ada na kumsapoti. Jamaa akaona hiyo ni deal nzuri haina shida mradi wafanye hilo jambo lao.

Jamaa akakabidhi sehemu yake ya kuishi alipopanga, na akauza baadhi ya vitu. Then akaenda kuishi katika nyumba ya jamaa huko nje ya mji kidogo.

Sasa jamaa anasema baada ya kufika kule ikawa sasa wanatakiwa kujadili biashara ile na namna wataanza. Anasema yule ndugu yake sasa akawa akimwambia kuwa hapa tunafanya ABC basi atawasiliania na watu zaidi ya 20 pembeni huko kupata ushauri wa ziada na mwisho wa siku anakuja na maoni ya hao watu wengine kisha ndio anayaleta mezani, sasa mshikaji hii kitu ikaanza mkwaza kwamba ima maana mimi haya niliyoyatafiti hayana uzito hadi jamaa anayacrush then akawa anahisi ni kama mtu aliyeajiriwa sasa anatakiwa kupokea maelekezo tu na sio partner ambaye anatakiwa kutoa maoni yake.

Anadaia pia huyu ndugu yake akaanza hapo hapo kumtumia amsaidie katika shughuli zake za ujenzi na kusimamia mafundi, na baadhi ya vitu vingine. Sasa hii kitu ikaanza kumla kwa ndani kwasababu ni kama jamaa alimchenjia gia hewani. Maana alichojua yeye ni kwamba itakuwa njoo tufanye biashara wewe ndio director mimi nakusikiliza wewe mradi tu usiharibu.

Sasa ikawa ni habari ya kuletewa vitu tofauti visimamiwe na shughuli tofauti ambazo jamaa hakuwa na matarajio nazo. Mwisho wa siku jamaa akaanza kujiskia kama anapata hali ya msongo wa mawazo. Hii ikamfanya kukosa amani kabisa. Na akajutia sana maamuzi yake ya haraka kuacha kazi kumsikiliza ndugu yake huyo.

Hivi sasa akaamua kurudi home kimya kimya na akamuacha jamaa akilalamika kwa ndugu wengine kuwa dogo ameamua kuondoka kimya kimya na kuna vitu ameacha vimesimama na haviendi mafundi hawajalipwa na malalamiko mengine.

Kimsingi kuna watu akikuona unataka jambo fulani anataka akutumie kwa ile shida yako ili yeye mambo yake yaende huku akikurubuni kwa maneno kuwa anakusaidia au mnasaiidiana. Kwanini usiheshimu muda na malengo ya mtu. Mtu anaacha kazi ya mshahara wa laki nane akijua mtakaa muanze kusimamisha biashara ya mamilioni unakuja unaanza mletea story za kwanza hii biashara sio lazima kuanza na mtaji mkubwa wa million 5,unaweza ukaanza na hata 50,000 halafu ukakuza taratibu huo mtaji hadi ifike huko juu. Sasa yeye amekwambia hiyo 50,000 hakuweza imudu, why usingeongea hayo mapema. Hivi utaanzisha biashara ya mazao ya kueleweka kwa mtaji chini ya milioni 5 na ufanye mambo ya msingi kufikia mafanikio mazuri?!
kweli mkuu na huu ndo uhalisia lakini hawa ma boss wetu wakija kwenye jamii wanajaribu kutuonesha kuwa wako na roho nzuri kumbe ni full exploitaion ya idea muda na nguvu za sisi ambao hatuna kitu! unapata mtu anawatetea sijuw nani kawambia mtakufa na hizo hela zenu
 
Mtu kasoma IT tena bachelor alaf unamuajir kuchoma chips huku akilala kwenye zizi la mbuzi, hivi huyu muajiri anajielewa kweli?

Kwa sisi wataalamu wa masuala ya Utawala na rasilimali watu tunaona kuna ignorance kubwa kwenye kichwa cha muajiri, kwani demotivation mara nyingi husababishwa na waajiri pale wanaoamua kukiuka kanuni na miongozo, Mtu wa Diploma mpe kazi ya level yake, wa masters mpe ya masters. Otherwise uwe unataka kutengeneza tatizo lingine.
 
Mimi ni IT na huna la kunifundisha ninapokwambia nina biashara zangu sio utopolo nilianza kuuza genge tangia nipo mwaka wa kwanza sasa hivi limeshakua duka na nimeajili kijana na nimempangishia na kumlipa mshahara kwa hiyo huna kitu cha kunieleza.

Tatizo la kukosekana kwa ajira isiwe sababu ya kudharirisha elimu zetu! siwez soma miaka kumi na sita almost afu uje unambie nize mihogo ya mia mia mimi never na kama kuna graduate wa hivo ujue anafanya ujue yupo kwenye progress mana hata mimi nishauza hadi mkaa wa kupika nikiwa first year hizo zote ni hustle kuhakikisha natimiz ndoto zangu haiwezekan utokee huko uanze kunipelekesha kisa kuna tatizo la ajira! basi ukinipelekesha nipe mahtaji yangu ya msingi
Ss uliomba kazi ya nini wkt una biashara zako?.!
 
Back
Top Bottom