Natafuta sehemu Tanzania nitakapopata nyama choma au supu ya Mamba au Kenge

Wakuu

Hivi nchi nzima na kubwa namna hii hakuna mkoa au sehemu ninapoweza kupata nyama choma ya mamba au nyama choma ya kenge?

Hao wanyama ni watamu sana hata kuku haoni ndani kwa utamu wake kwanza ni nyama laini halafu ni white meat.

Mkuu nenda Bandundu, DRC utaipata hiyo supu!
 
Kipindi cha nyuma alikuwepo mzee mmoja sumbawanga akiitwa sultani alikuwa muwindaji mzuri wa mamba na muuzaji wa nyama ya mambo pia jaribu kuulizia kwasababu alikuwa anafuga mamba pia, mm mwenyewe nimewahi kutumia nyama hiyo ni tamu asikwambia mtu
Wakuu

Hivi nchi nzima na kubwa namna hii hakuna mkoa au sehemu ninapoweza kupata nyama choma ya mamba au nyama choma ya kenge?

Hao wanyama ni watamu sana hata kuku haoni ndani kwa utamu wake kwanza ni nyama laini halafu ni white meat.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hayo mambo utayapata huko visiwani zenji isee nilikuwa huko last year kunamahali kulikuwa na kidibwi kenge akarogwa kuingia humo niliona njemba tatu zina mkimbiza vibaya mno nikabaki mdomo wazi nn hawa watu wanafanya!

Yaani funga na kufumbua yule kenge ameshadakwa jamaa waka mchuna ngozi na kumpika supu mm naona isee wakanunua na mikate yao ya boflo inaitwa wanasema hakuna nyama tamu km hii mm nilishidwa kula kwanza nawaogopa hao wadudu.
Lakini sijui walimchinjaje? Maana kumshika ni suala moja, lakini kumchinja ili awe halali kwa mlo wa wakazi wa huko ni shughuli nzito!
 
Back
Top Bottom