Natafuta sehemu au mtu wa kufanya naye kazi ya ufundi wa magari

charenger

Senior Member
Mar 16, 2023
181
258
Habari wakuu?

Mimi nimejifunza ufundi magari na kazi nishaweza changamoto yangu ni kuwa kwa sasa Sina sehemu ya kufanyia kazi mana kunasehemu nilikuwa nimejishikiza ila kwa sasa hii sehemu ishafungwa kutokana na fundi mkuu kushindwa kulipa Kodi kwahio naomba Kama kuna fundi mechanics anahitaji msaidizi anitafute nipo tayari kufanya kazi popote.

Umri wangu miaka 22 nipo Dar, magari ambayo najua kutengeneza ni
  1. Toyota
  2. Nisan
  3. Mistubish
  4. Ford ranger
Lakini Kama kuna fundi anakazi tofauti nagari ninazo jua anahitaji msaidizi pia anitafute tuu Mana ni mwepesi kujifunza kwa haraka.

PM ipo wazi mwenye uhitaji tuwasiliane.
 
Kama utaweza kwenda Moshi nikupe namba ya mtu uwasiliane nae anahitaji mafundi.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom