Natafuta Rafiki, Mchumba

Idimi

JF-Expert Member
Mar 18, 2007
14,888
10,368
Natafuta rafiki wa kike (girlfriend) wa kubadilishana naye fikra na uzoefu wa mambo mbalimbali.

Wasifu Wangu

  • Mfupi kiasi, 5'5 ft, Maji ya kunde
  • Umri,miaka 28
  • Ni mkristo
  • Nina kazi
  • Napendelea kucheza mpira wa miguu, kucheza pool table, kuogelea, kuendesha baiskeli, kufanya kazi kwa bidii, kusafiri, kusikiliza na/au kuandaa/kutengeneza muziki. Napenda pia mara chache chache kwenda baharini kupunga upepo.
  • Ni mcheshi
  • Napenda kujifunza mambo mapya
  • Nashaurika katika mambo yenye mantiki.
  • Makazi: Dar es Salaam

Ningependelea kupata rafiki mwenye sifa hizi

  • Awe na umri usiozidi miaka 30
  • Mrefu wa wastani
  • Awe mweupe kiasi, (sio weupe wa mkorogo)
  • Mnene wa wastani ama mwembamba
  • Elimu, angalau kidato cha sita
  • Awe mcheshi na mwepesi kujifunza
  • Sibagui rangi ya mtu (kwa maana ya Uhindi, Uarabu, Uzungu, Uafrika ama Uchotara)

Mwenye sifa mwafaka anitumie PM kwa kujiamini kabisa, nitajibu bila kusita.
Nashukuru!

Mkuu Idimi
 
Kwi kwi kwiiii!
Nilijua akina bonge watalalamika tu,
hahahahhhh!
Ni kweli mkuu, ila sina nia mbaya kamwe!
 
Mzee naona unaweka mitego hapo mwanangu ila usihofu utawanasa tuu. Kama ni rafiki wa kushauriana naye pia wakubwa zaidi ya 30yrs wanaweza kukupa constructive ideas bila shaka. Au sio ushauri wa kawaida? Nakutakia kila la kheri mwana.
 
NATAFUTA RAFIKI WAKIUME AWE ANATOKEA MWANZA AWE NA UMRI WA MIAKA 30 ANA ADIA YA BIASHARA KTK MKOA WA MWANZA TWASILIANE erasto02@yahoo.com
 
Inaweza kuwa bahati yako mkuu Idimi, nakutakia kila la heri.

Nashukuru sana mkuu, tuombe uzima, huenda nikafanikiwa!
Inawezekana Jf hapajafikiwa na watu ninaowataka, sijapata Pm mpaka sasa.
Naendelea kuvuta subira!
 
NATAFUTA RAFIKI WAKIUME AWE ANATOKEA MWANZA AWE NA UMRI WA MIAKA 30 ANA ADIA YA BIASHARA KTK MKOA WA MWANZA TWASILIANE erasto02@yahoo.com

"Awe anatokea Mwanza"
Kwa kigezo hiki tu, basi mie nishafeli tayari.
Hapa Jf wapo wanaotokea Mwanza, utawapata tu.
Ila hilo jina ktk email nalitilia shaka, "Erasto"?
Nakutakia kila la kheri!
 
Last edited:
Natafuta rafiki wa kike (girlfriend) wa kubadilishana naye fikra na uzoefu wa mambo mbalimbali.
* Napenda kujifunza mambo mapya
* Awe mcheshi na mwepesi kujifunza

Mkuu Idimi,
ni katika kutafuta ufafanuzi, 'awe mwepesi wa kujifunza'? au awe na 'experience'? ili uweze kujifunza?

kila la heri kaitka kutafutab 'girl friend'
subira yavuta heri
 
Mkuu Idimi,
ni katika kutafuta ufafanuzi, 'awe mwepesi wa kujifunza'? au awe na 'experience'? ili uweze kujifunza?

kila la heri kaitka kutafutab 'girl friend'
subira yavuta heri

Mkuu Kasana,
Najua mhusika atakuwa na ujuzi fulani wa jambo fulani ambalo huenda jambo hilo silijui,na hatakuwa na ujuzi wa jambo jingine ambalo mie nina ujuzi nalo, kwani hakuna mtu "Asiye na kitu" kamwe! Hali kadhalika hakuna aliye na kila kitu. Ndipo hapo inakuja pointi ya yeye kuwa "Mwepesi" kupokea yangu niliyonayo, kama mimi nilivyojiweka tayari kupokea toka kwake yale ambayo sinayo.

Tuombeane kheri mkuu!
Bila shaka nitampata
 
Sasa Bw.Idimi mimi sijaelewa kwani ni kujifunza tu au kuna issue nyingine kwani nimeona umeweka mpaka suala loa urefu nk.na kama ni suala la kujifunza unaweza kujifunza kwa mtu yeyote yule hata kwa mtoto mdogo any way endelea kuvuta subira tapatikana tu, kila la kheri
 
Wala usikonde Felister, kuna vigezo vingine ni "negotiable", kwa hiyo kuna watu wengine wanaweza kujitokeza na kuwa na asilimia nyingi ya vigezo ninavyotaka lakini wakakosa baadhi yake, kwa hiyo tunaweza ku "iron out" bila shida.
Nadhani nitampata mhusika, naendelea kuvuta subira.
 
Mkuu Kasana,
Najua mhusika atakuwa na ujuzi fulani wa jambo fulani ambalo huenda jambo hilo silijui,na hatakuwa na ujuzi wa jambo jingine ambalo mie nina ujuzi nalo, kwani hakuna mtu "Asiye na kitu" kamwe! Hali kadhalika hakuna aliye na kila kitu. Ndipo hapo inakuja pointi ya yeye kuwa "Mwepesi" kupokea yangu niliyonayo, kama mimi nilivyojiweka tayari kupokea toka kwake yale ambayo sinayo.

Tuombeane kheri mkuu!
Bila shaka nitampata

vipi ukipata aliyebobea kila eneo utamkubali? usije kushangaa wewe ni kupokea tuuuuu.utapata tu,weee tulia
 
vipi ukipata aliyebobea kila eneo utamkubali? usije kushangaa wewe ni kupokea tuuuuu.utapata tu,weee tulia

Duh! Hii kali.
Haiyumkini kumpata aliye kamili kila idara, ingawa huenda ikatokea. Anyway, nitamkubali tu.
Still searching.
 
samahani IDIMI wewe ni mvulana unatafuta rafiki wa kike au? maana kuna mtu anataka kueusha ndoano ila anashindwa kukusoma vizuri,

Duh huu kweli ni mtego mzuri, vuta subira ndugu yangu anaweza akatokea mtu akakuonea huruma, ukiona kimya basi punguza badhi ya vigezo kama umri na vinginevyo
 
Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom