Natafuta pikipiki ya mkataba kwa mtu aliopo maeneo ya Dar es salaam

MG255

Member
Mar 3, 2018
13
3
Habari zenu ndugu zangu, mimi ni kijana nilie maliza elimu yangu kwa level ya bachelor mwaka 2017, toka kipindi hicho nimejaribu kufanya vitu tofautofauti ikiwemo vyakujiajiri binafsi na vyengine vyakujitolea katika makampuni ila bado sijaona unafuu wa maisha.

Nimeamua kufikilia zaidi namna ya kuweza kuyaendesha maisha yangu hasa katika kujitafutia riziki hasa ukizingatia ugumu uliopo kwenye kupata ajira kwa kipindi hiki si serikalini, mashirika au hata kwenye makampuni imekuwa changamoto mmno.

Hivyo basi kuna biashara naifanya kwa sasa nashukuru Mungu muitikio wake kwa watu niliowakusudia sio mbaya ila changamoto yangu ni kushindwa kuwafikia wote kwa wakati hasa ukizingatia muda wanao hitaji bidhaa yangu ni kama unafanana na hawapo sehem moja hivyo inapelekea wengine nishindwe kuwafikia kwa wakati nakuushusha ufanisi wangu katika utendaji wa biashara yangu.

Kwahio ninaomba kama kuna mtu anayo pikipiki na anao moyo wakusaidi nakuona vijana wakijikwamua kwa shughuli zao naomba aniunge mkomo kwenye hili ili niweze kupata hio pikipiki itakayonisaidia kufanya shughuli hii. Nipo Kinondoni Morocco ukihitaji tuonane kwa mazungumzo zaidi nipo tayari. Asanteni.
 
Mkuu kwa nn usniajiri maana piki piki nnayo
 
Hilo swala la pikipiki ya mkataba mpya linawezekana ila shida ni swala la uwaminifu, na hilo swala ni kujuana , kwa huku itakuwa ngumu maana hatufahamiani.
 
Back
Top Bottom