Natafuta oda za kuku wakienyeji kutoka singida kupeleka kwenye mahotel

vumiliag

JF-Expert Member
Sep 1, 2018
375
700
Habari za muda huu,
Natafuta mtu mwenye hoteli au mgahawa ambaye ntakua nampelekea kuku wa kienyeji kutoka singida vijijini kwa wingi

Mfano, naweza kua nampelekea kuku 50 Kwa wiki au kuku 100 kwa wiki..bei ya jumla ntafanya kwa 17,000 kushuka chini kulingana na saizi ya kuku

Napatikana kimara mwisho, 0692669235
 
bei ya jumla haizid 12000 nenda katafute masoko dom yapo mengi sana
Habari za muda huu natafuta mtu mwenye hotel au mgahawa ambaye ntakua nampelekea kuku wa kienyeji pure kutoka singida vijijini kwa wingi mfano naweza kua nampelekea kuku 50 Kwa week au kuku 100 kwa week ....Bei ya jumla ntafanya kwa 17000 kushuka chini kulingana na size ya kuku

Maongezi yapo

Napatikana kimara mwisho 0692669235
 
Chief mimi natafuta mbegu tu ya kuku wa huko, nikiagiza unaweza niletea hata matetea 2 na jogoo 1
 
Mwenye uhitaji wa kuku wa kienyeji Ni supply hotelin kwake
 
12000 sio rahisi maana sikuiz hata vijijini ukifata Bei ni 13000 Sasa iyo 12000 labda kuku wakizungu
Mkuu huyo unayeuza 17,000 ana kilo ngapi ? Vyuma vimekaza pote mkuu hata kama huko kijijini wanaona 12,000 kukuuzia wewe ni kubwa hivyo hivyo kitaa watu wanalia.., kwahio kwa uzoefu wako huyo kuku wako anaweza akaliwa na watu wangapi na wasilalamike kwamba wamekula njiwa ?
 
12000 sio rahisi maana sikuiz hata vijijini ukifata Bei ni 13000 Sasa iyo 12000 labda kuku wakizungu
Yeah hiyo 12 wanauzwa wale chotara, ila pia wafanyabiashara ni wakandamizaji hiyo bei kwao inawezekana, ukiweza wanunue na tafuta kaeneo uwe unawaandaa mwenyewe unauza na chakula au chips au hata wabichi ukiwa na freezer ddm wageni ni wengi utauza ukizoeleka
 
Mkuu nachofanya mm kuku wanapokusanywa vijijini naangalia ukubwa wa kuku ili wateja wasilalamike mfano uyo wa 17000anafika Hadi kilo 3 yategemea na ukubwa wa kuku ikiwa Bei chini ya hapo na ukubwa wa kuku unapungua pia lakini mtu akihitaji wa biashara Kama namletea inamaana ntamletea wakubwa Ili wateja wake wasilalamike
 
Yeah hiyo 12 wanauzwa wale chotara, ila pia wafanyabiashara ni wakandamizaji hiyo bei kwao inawezekana, ukiweza wanunue na tafuta kaeneo uwe unawaandaa mwenyewe unauza na chakula au chips au hata wabichi ukiwa na freezer ddm wageni ni wengi utauza ukizoeleka
Itabidi nlifanyie kazi hili wazo mkuu Ni zuri Sana japo kua Mimi nawanunua singida nawauzia dar
 
12000 sio rahisi maana sikuiz hata vijijini ukifata Bei ni 13000 Sasa iyo 12000 labda kuku wakizungu
Siyo kweli. Dodoma tunakula Kuku wa kuchoma wa kienyeji hadi tsh13,000! Kwa hiyo bei ya kununua lazima iwe 10k au chini ya hapo
 
Karibuni kwa oda za kuku maongezi yapo
tapatalk_1565443356467.jpeg
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom