Nahitaji nyumba ya kuishi niwe kama msimamizi

drmaxmhozya

Member
Aug 7, 2020
51
48
Mimi naishi nyumbani ila ni kijana ambaye nahitaji pia ndoto zangu zikamilike kila mmoja yupo duniani kwa ajili na ameumbwa kwa mfano wake siyo kwamba Sina Kodi ya kulipa hapana namatumaini kuna watu wana nyumba zao wengi tu ila wamekosa watu gani waaminifu ambao wanaweza kulinda nyumba zao kwa uaminifu wote kwa kuzingatia usafi wa mazingira nasema hivyo kuna watu wanaishi ulaya nyumba zao zipo huku Tanzania.

Basi mimi nahitaji hiyo fursa Kama kuna mwenye nyumba kakosa muangalizi basi Mimi nipo tayari kuilinda nyumba hiyo kwa uaminifu wote kabisa nichukue nafasi hii Kama kuna mwenye nyumba kakosa muangalizi nyumba ipo tu basi tusaidiane ndo itakuwa mwanzo wa udugu wetu mungu katuumba wanadamu tupendane na msaidie mwenzio anapohitaji asanteni sana namatumaini jamii forum inawatu sahihi Sana wenye weledi na upendo

Mimi ni muhitaji nisaidieni nipo Dar es Salaam

Mawasiliano yangu ni 0657709912
 
Wewe najua ni mtu mzima nazani watu wamenielewa wenye utu Kama Mimi ni chawa Asante Sana ubarikiwe Sana ila angalia kinywa chako hiko mungu hapendi maneno machafu
 
Sawa Asante Sana ndugu yangu Mimi nipo tayari kuja ili hata shughuli zangu nizihamishie huko Kama uko tayari kunisaidia kwa hilo wewe ndo binadamu unayeelewa thamani ya utu na mtu
 
Ushauri wangu ni huu

Hata upigike vipi usikubali kurudisha mpira kwa kipa pambana.

Kuishi bure sehemu ya mtu kwa kuhisi kwamba unapunguza ugumu wa maisha haitakusaidia kitu sanasana itakulemaza, na maisha yako yote yatajijenga katika utegemezi.

Kama kipato ni kidogo angalia sehemu rahisi unayoweza kulipia chumba kisha jipange pambana hakika utatiboa.

Nna wasiwasi unachokitaka saivi, una uzoefu nacho, na inawezekana umeshakaa nyumba kadhaa za watu kwa mtindo wa kulinda, kama hichi ninachohisi nikweli basi jua ya kwamba mazoea ya kuishi maisha hayo yamekwisha ingia kwenye damu, jitahidi kwa namna yeyote uachane na haya maisha.

Nakupa mfano mdogo
Kuna ndugu zangu walipewa hifadhi kwa baba zao wakubwa tangu ujanani, na kwa bahati nzuri au mbaya hao baba wakubwa hawakuwahi kuwafukuza wakajitegemee, waliwaacha wakae miaka yote mpaka leo hii bado wanaishi kwa baba zao wakubwa kwa zaidi ya miaka 30.

Madhara yake ni haya
Hawajui gharama za kupanga hivyo wamebweteka hata hari ya kutafuta maisha inapungua kwasababu majukumu yao yanabaki kutafuta ela ya kula tu.

TAFAKARI CHUKUA HATUA
 
Sijawahi Mimi naishi kwetu na kila mmoja anamipango yake na malengo ndo mana awali nilisema siyo kwamba Sina pesa ya kodi sijawahi kuwa mlinzi wa nyumba na siwezi bweteka najitambua Sana brother anayebweteka hana malengo Mimi na uchungu wa maisha ukinifikiria kwa ndani sana ndo utanielewa yani kwa kina Sana

Kuhusu kurudisha mpira kwa kipa katika maisha hiyo kawaida ni bora urudishe mpira kwa kipa kuliko mpira ule kupotea kipa ataanzisha upya ukipotea je

Kosa siyo kuanguka kosa ni kuanguka na kushindwa kuinuka
 
Kama kazi unayo na hela ga kodi unayo acha mseleleko wewe mtoto wa kiume kapange yaani unataka uanze kudandia kwente nyumba za watu alafu wakija kukutimua unaondoka na nguo tu acha mawazo hayo kama kodi unayo unavyosema kalipe kodi
 
Kama kazi unayo na hela ga kodi unayo acha mseleleko wewe mtoto wa kiume kapange yaani unataka uanze kudandia kwente nyumba za watu alafu wakija kukutimua unaondoka na nguo tu acha mawazo hayo kama kodi unayo unavyosema kalipe kodi
Uko sawa lakin hujanielewa vizuri kwa kina Sana namanisha nini inatakiwa unidadavue nini nahitaji Mimi ni muhitaji siyo kwamba napenda mseleleko kumbuka watu waliotoka waliinuana hilo jua kumvuta shati mtu haijalishi anakianzio gani unaweza mvuta shati mtu kwa kumuongezea ili apambane zaidi mimi cyo wa kwanza na siyo nikikosa nyumba itashindikana kuendeleza maisha ni sawasawa na msaniii anatafuta management au mtu mwenye uwezo aweze msimamia ili kazi zake zifike anapopataka kwanini wasijiendeshe wao?

Na mfumo huu bado unaendelea sana kwahiyo kushikana mikono bado tu kupo sema wewe ndo hujanielewa targets zangu ila aliyenielewa na kuguswa atajua kweli dogo anamanisha kitu watu wanatafuta masponser mbele huko Sasa Mimi natafutia nyumbani hapahapa ni moja ya kupambana pia nazani umenielewa vizuri brother
 
Uko sawa lakin hujanielewa vizuri kwa kina Sana namanisha nini inatakiwa unidadavue nini nahitaji Mimi ni muhitaji siyo kwamba napenda mseleleko kumbuka watu waliotoka waliinuana hilo jua kumvuta shati mtu haijalishi anakianzio gani unaweza mvuta shati mtu kwa kumuongezea ili apambane zaidi mimi cyo...
Kuishi kwenye nyumba ya watu bure haya nayo ni malengo kweli?
 
Kuishi kwenye nyumba ya watu bure haya nayo ni malengo kweli?
Huwezi kunielewa Kama umeshindwa kunielewa endelea kutonielewa maisha ni safari ndefu Sana mjomba leo uko hapa kesho pale kuna changamoto nyingi Sana katika maisha na unaweza tengeneza urafiki mwema kwa mtu hata asiwe ndugu yako malengo ya mtu no matter where he lives or how much does he pay for rent unaweza kuwa na pesa ukapanga nyumba ya milioni moja kwa mwezi ukakosa malengo yote nimeandika ndani basi hujataka kunielewa what do I mean
 
Post #12 imebeba matokeo ya hicho unachotaka kufanya.

Tukiacha yote, kumbuka jambo lako siyo dogo, yaani mtu kukukabidhi nyumba, inaonekana kuna sababu kweli ya msingi ya wewe kuhitaji nyumba ila ungeweka sababu hasa kwanini unahitaji nyumba kuwa kama muangalizi badala ya wewe kwenda kupanga maswali yangepungua na uaminifu ungekuwepo.

Humu kuna watu wana uzoefu na washapitia majanga ya kila aina hivyo try to be specific mtu anaweza kuelewa.

Maelezo uliyoyaandika yote na katika reply za comments zote hujawa muwazi kuweka lengo lako haswa.

Kwanini unahitaji nyumba kama muangalizi, Je

1. Ni kwaajili ya kujipanga ?
2. Ni kwaajili ya kupata connection?
3. Ni kwaajili ya kujenga ukaribu kwa lengo la kusaidiwa mambo fulani katika maisha yako?

Weka wazi nia yako dhahiri itakuwa rahisi kufikirika.

Unaweza pewa nyumba ukauza vitu na ukasepa, siyo rahisi kumuamini mtu karne hii.
 
Binafsi nimekuelewa sana.

Sio ulaya tu, watu wengi pia wamehamia Dodoma. Ni matumaini yangu utakuwa na nia njema, utakuwa tayari kutoa stakabadhi zote za uthibitisho wako na ikibidi kusaini mkataba wa mababidhiano ...

Nakutakia kila la kheri
 
Back
Top Bottom