Natafuta ngo yakushirikiana nayo kutekeleza mradi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Natafuta ngo yakushirikiana nayo kutekeleza mradi

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by nyendo, Feb 18, 2012.

 1. n

  nyendo Member

  #1
  Feb 18, 2012
  Joined: May 31, 2011
  Messages: 20
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wakuu habari za miangaiko mimi ni kijana mwenye shahada ya mazingira ( Bachelor of Science in Environmental Management) baada ya kusaga sana viatu kutafuta ajira nikajikuta nakuwa na wazo la kujiari na kuajiri wengine pia. Asante kwa mitandao ya siku hizi! nilipoweka idea yangu na profile yangu kwenye mtandao wa Imagine Nations nikabahatika kumpata Mentor ambaye amefurahia sana idea yangu na yeye yupo USA ni consultant ambaye anawalink na kusaidia kupata pesa toka Usaid. Sasa tumefikia hatua ambayo nahitajika kuja Template za mradi huo na yeye kuziwakilisha ili fund iweze kutoka. Hii nilikuwa kama natest zari sikuwa na NGO wala CBO na huyu bwana anataka vitu hivi na mambo mengine. Kwa vile anayomiradi mingine Uganda anataka pia kuja hapa kwangu ili kuniona. Maelezo ni mengi kwa aliyetayari tusaidiane kutekeleza naomba tuwasiliane ili nimpe details zaidi. Just to hint mradi ambao tunatakiwa kuimplement ni wa kilimo cha mboga na matunda kwa kujenga mabwawa ya maji na kufanya drip irrigation na baada ya hapo vikundi vitakavyoundwa na kulima kwa kutumia mabwawa hayo vitaunda cooperative ili kukausha matunda na mboga kwa ajili ya soko la nje na ndani na hapa tutatumia solar dryer na electric dryer. Idea ni kutotegemea rainfed holticultura.
  Nipo Karagwe kagera.
  please kwa aliye tayari anaweza kuni PM hapa mwijagejr@gmail.com au 0764312429.
  Asanten
   
 2. CHASHA FARMING

  CHASHA FARMING Verified User

  #2
  Feb 18, 2012
  Joined: Jun 4, 2011
  Messages: 6,133
  Likes Received: 2,117
  Trophy Points: 280
  Mku hongera sana kwa hili, ila mimi ningekushauri jambo moja, kutumia NGOs ya watu wengine si jambo jema kabisa kwa sababu NGOs ya watu wengine ina VISION YAO INA MISION YAO WENYEWE NA INA OBJECTIVE ZAO,

  Mkuu kama unaona kuregsta NGO ni mlolongo jaribu kuregsta kama Kampuni, utakuwa umenielewa,
  Kuna zile kampuni ambazo ni LTD kabisa lakini hazina cha share wala nini so unaweza kuiregsta kama LTD COMPANY ambayo haina cha kugawana share kuna maelezo yake kwenye website ya brela,

  Mimi nisha fanya kazi na NGOs kama mbili hivi ambazo zimesajiriwa kama LTD company
   
 3. Entrepreneur

  Entrepreneur JF-Expert Member

  #3
  Feb 20, 2012
  Joined: Jun 26, 2011
  Messages: 1,092
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Ushauri wa Komandoo, hapo juu ni mzuri na ukiufuata nadhani utakusaidia. Lakini mimi binafsi nina observation chache ambazo zinatakiwa kufanyiwa kazi. Kwanza ni vyema ukamuuliza huyo mentor hiyo NGO iwe vipi?, I mean iwe ime-exist kwa muda gani? -kwani kuna Donors wanahitaji track record of three years. Ukishajua hilo ni rahisi kupata mbia kwani wengi wanaweza kukukwaza kwa tamaa ya hela za haraka haraka.

  Sasa turudi kwenye ushauri wa Komandoo, na ndio msingi wa hapo kwenye red
  Ni kweli, unaweza ukasajil NGO kama kampuni, lakini mpaka upate hiyo status kuna procedure za kufuata. kwanza utatakiwa usajili kampuni isiyo na mtaji. Hii kitaalamu wanaita Company Limited by Guarantee, hii haina share capital kama nilivyosema hapo awali. Ka hiyo registration fee inategemea na idadi ya subscribers kwenye MEMARTS. For example; For the registration of this kind of company where the number of members as stated in the Articles of Association, does not exceed 25, registration fee ni Tsh.50,000/=.Halafu utatakiwa ulipie filing fee Tsh.45000 na stamp duty Tsh. 16200.

  Kazi hii ni rahisi na inachukua muda mfupi kwa mtu anayezitambua vyema corridor za BRELA. Ukishamalizana na BRELA kwa gharama hizo, basi itabidi uende kwa Registrar of NGO ili uombe Certificate of Compliance (hii hutolewa bure). Certificate hiyo ndiyo itakayoipatia status ya NGO hiyo kampuni yako.

  Hata mimi nakushauri upitie njia hii, ili uwe na sauti katika hiyo project yako. Lakini kama kuna kigezo cha muda wa uhai wa hiyo NGO, basi rudi hapa hapa, ili tujue tunasaidiana vipi.
  Kila la heri
   
 4. n

  nyendo Member

  #4
  Feb 20, 2012
  Joined: May 31, 2011
  Messages: 20
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Asante sana kwa ushauri kaka zangu ushauri hapo juu ni wa busara na kitaalam zaidi hasa kwa kuzingatia mambo ya ownership ila kaka kwenye mradi huu hakuna limitation ya muda kwani huyu bwana ndo ametoa idea ya ushirikiano baada yakumwambia kuwa sina papers.
  It sound easy lakini kaka mara nyingine hata kuja cafe pesa inakuwa tabu sana je hayo mambo fee ntayaweza? nakumbuka nipo huku mipakani i mean kagera.
  So wanajamvi hivi ndio hali halisi hopeful mtazidi nishauri kwa kuzingatia hayo.
   
Loading...