Natafuta nafasi ya kujitolea katika sekta ya ujenzi

Granite

JF-Expert Member
Jul 6, 2016
268
624
Wakuu wa JF!

Mimi ni kijana wa kiume nina umri wa miaka 24 nimemaliza Ordinary Diploma ya Civil Engineering (Stashahada) mwaka 2015 na nilipata nafasi ya kuendelea na masomo ya shahada kuanzia mwaka 2015 hivi sasa niko mwaka wa pili wa masomo ya Bachelor in Civil Engineering mwaka wa 2. Ninatafuta sehemu ya kufanya kazi ya kujitolea lengo kubwa likiwa ni kupata uzoefu wa taaluma ninayoisomea kwa hivi sasa

Ninapenda kujitolea kwa kampuni zenye miradi mkoa wa dar es salaam ili nisi athiri shughuli zangu za kitaaluma.
Nina uzoefu wa shughuli za ujenzi ambazo niliwahi kuzifanya katika kipindi cha mafunzo ya vitendo ambapo nilishiriki Ujenzi wa Daraja la Mto Kanoni(Kagera) nilikuwa chini ya usimamizi wa Tanroad kama Fundi msanifu msaidizi (Assistant Technician), Ujenzi wa Jengo la kibiashara katika jiji la mwanza ( Sub-structure level and super structure level of 6 floor building)
Uzoefu nilionao ni Building works na Road construction works
Nina ujuzi wa kutumia program za computer kama Microsoft office Pack(Excel and word kwa ufasaha)

Na nipo katika hatua ya kujifunza kutumia program za uhandis kama vile Autocad na Archcad

Natanguliza shukurani
 
peleka maombi kwa kampuni ya UNITEC construction company wapo hapo dar
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom