Natafuta mwarabu wa kumuuzia eneo kwa ajili ya sheli

Naona mbaguzi huyu hataki kumuuzia mmatumbi mwenzetu, mnunuzi wake lazima awe Mwarabu tu! Sijui Wamatumbi wamemkosea nini!
 
Hivi sielewi km akili zako zinakamata tbc au clouds! Kuuza eneo hadi mwarabu, au una biashara nyingine, weka wazi.
 
Ukisikia Inferiolity Complex ndio hii! Kwa hiyo hata akitokea Mbantu mwenzio mwenye mkwanja unaohitaji wewe utakataa hadi ajitokeze muarabu??? Pole Sana.

ya elekea amefanya u beki tatu sana kwa warabu mpaka ametoka kwa hiyo anawakubali sana
 
Iko mimi nunua bana veve, veve uza gapi? mimi Kanjubai kuba 4M taka kuja hapa na namba yako ya akaunti nikupe cheki veve sawa eeeh iko zuri veve
 
nina eneo kubwa la eka 2, liko mbezi luis pembezoni mwa barabara ya kwenda mpiji, natafuta mwarabu anaetaka eneo kwa ajili ya sheli nimuuzie haraka iwezekanavyo, kama kuna mtu anamjua mwarabu anae hitaji eneo basi tuwasiliane, donge nono lipo

Check na Rostam Aziz
 
msilembee madongo sana pengine mwamba yuko kislang zaidi, kuna zama flani "mwarabu" na "mshefa" ilikuwa inatumika kwa slang kumaanisha "tajiri" inawezekana mleta mada amekuja kislang, if that is not the case, mleta mada inabidi aonane na daktari wa akili kabla hajakuwa beyond repair.
 
Wakati sisi tunajiandaa kuwatimua,wewe unawakaribisha waarabu wahindi!jiulize wewe waweza kwenda kwao kuweka shell?
 
sio lazima mwarabu lakini mara nyingi warabu ndo watu wa sheli,


Husomeki! halafu inaelekea hujui biashara! sema unauza eneo fulani na kama una details zake ambatanisha ikiwezekana na bei tuambie, sio natafuta mwarabu nimuuzie eneo, kwani waarabu peke yao ndo wenye uwezo wa kununua? na hapo kwenye sheli nadhani unamaanisha ni petrol station, duu we wa wapi wewe? acha kasumba angalia usije nunuliwa na wewe!
 
nina eneo kubwa la eka 2, liko mbezi luis pembezoni mwa barabara ya kwenda mpiji, natafuta mwarabu anaetaka eneo kwa ajili ya sheli nimuuzie haraka iwezekanavyo, kama kuna mtu anamjua mwarabu anae hitaji eneo basi tuwasiliane, donge nono lipo


usilazimishe matumizi ya eneo kwa mteja kwani lazima aweke hiyo ''sheli''?
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom