Natafuta Mwalimu mzuri wa Udereve Theory mwenye notes-Kuna Fursa

Masokotz

JF-Expert Member
Nov 26, 2018
3,434
5,404
Habari,

Kama mada inavojieleza niko Mbioni kufungua chuo cha Udereva kwa ajili ya Mteja wangu mmoja na ninahitaji Mwalimu Mzuri wa udereva ambaye anatakiwa akidhi vigezo vifuatavyo:
  1. Awe na notes za electroniki za full course
  2. Awe anajua kutumia PC na Projector
  3. Awe tayari kujifunza zaidi
  4. Awe tayari kusafiri
I wapo unafikiri wewe ni mwalimu mwenye Vigezo tafadhali tuma wasifu(CV yako) pamoja na NOTES ulizonazo na mahali ulipo pamoja na kiwango cha malipo unachohitaji au kutarajia kwa siku/mwezi.ZIngatia kwamba taarifa/mahitaji yote hapo juu ni lazima. taarifa zitumwe kwenda masokotz@yahoo.com Kabla ya tarehe 5 March. Hakikisha unayo leseni ya udereva

Asanteni na karibuni sana
 
wewe shida yako sio mwalimu mzuri, wala sio nini, shida yako kuu ni upate Notes nzuri utokomee
Vyvyote vile utakavyofikiri. Kama ukituma note na zikiwa ni nzuri basi uwezekano wa kuwa mwalimu mzuri unaogezeka. Hata hivyo hizo ni fikra zako tu.
 
Hapo kwenye kutuma materials za kufundishia sijaelewa nadhani mngefanya siku ya interview ndio kila mmoja anaonyesha ana nondo kiasi gani
 
Mkuu,Materials mtu kama anazo anazo tu.Kama anataka kutuma atatuma tu.Kama hataki kutuma ni yeye.Ila kwa sisi tunataka mtu atume na itakuwa ni kigezo mojawapo katika kuamua nani atafutwe na nani aachwe?

Any way kama mtu akituma haimfanyi apungukiwe na kitu ila kama anaona kutuma ni tatizo atatafakari mwenyewe.Sisi tutaangalia vigezo na masharti yetu tu.Hayo mengine ni maamuzi ya muombaji.
 
Nafikri ungempa email atume details zinazohiajika ingependeza zaidi ila nitaangalia namna nimtafute
mkuu msifanye mambo kuwa magumu, siyo kila Mwalimu anaweza kuwa na access ya E-mail, wekeni alternatives pia! Kwani nyie hamna ofisi ama sanduku la Posta?
 
Mkuu,Materials mtu kama anazo anazo tu.Kama anataka kutuma atatuma tu.Kama hataki kutuma ni yeye.Ila kwa sisi tunataka mtu atume na itakuwa ni kigezo mojawapo katika kuamua nani atafutwe na nani aachwe?

Any way kama mtu akituma haimfanyi apungukiwe na kitu ila kama anaona kutuma ni tatizo atatafakari mwenyewe.Sisi tutaangalia vigezo na masharti yetu tu.Hayo mengine ni maamuzi ya muombaji.
hmmm, naona kama Notes imekuwa kipaumbele sana,
 
Mnakusanya NOTES hamtaki waalimu simple and clear.

kwanini atume kama ni mimi nakuja na projector na laptop nakuonesha tunakubaliana au nasepa nazo
 
Kama unafikir hivyo utangoja sana.Its up to you kama unafikir notes zako ni bora kuliko zote.
 
hmmm, naona kama Notes imekuwa kipaumbele sana,
Ni jinsi tu unavoangalia.Chuo kina sababu ya kutaka mwalimu mwenye notes kwa sababu za kimkakati.Kama shida ni notes Udereva sio engineering.Notes zipo ila tuna sababu y akutaka mwalimu mwenye notes na anayejua kutumia projector kufundisha.
 
Huyu anatafuta notes kwa ajili ya registration ya chuo chake wala hatafuti mwalimu
Mkuu unaweza fikiri hivo ila utshangaa sana kugundua kwamba kama shida ni notes najua pa kuzipata.Ila nahitaji mwalimu mzuri,anayejiamini,mwenye notes na anayejua kutumia projector kufundisha
 
Kama hivyo ndivyo je mtu akituma notes inaku guarantee kwamba ni mwl mzuri na anajiamini na anajua kufundisha? Nadhani njia nzuri ingekuwa kama alivyosema mdau hapo juu,mwl aje personally na material (notes) afanye demo hapo ndo utajua anakufaa au la,sidhani kama kuna mtu makini ataweza kutuma hizo notes.
 
Mkuu,hutaelewa,watu wametuma na wako makini.Tangazo liko very clear.
 
umenisoma vizuri
 
4 Reactions
Reply
Back
Top Bottom