Natafuta muwezeshaji/muwekezaji katika sekta ya kilimo biashara

Mungu akufanikishie hitaji la moyo wako

Watanzania tulio wengi ni waoga wa kuwekeza mitaji

Watanzania tulio wengi sio waminifu kwenye Mali

Hizi changamoto zinatufanya tuonekane hatupendani kumbe changamoto hizo hazitatuliki
 
Habarini za mchana ndugu zangu na poleni kwa majukumu mazito ya ujenzi wa taifa.

Mimi ni kijana wa kiume na Mtanzania mwenye umri wa miaka 28. Nina Elimu ya chuo kikuu katika ngazi ya shahada ya kilimo na katika hali ya ndoa mimi bado sijaoa na wala sina mtoto kwasasa.

Hivi sasa ninapatikana katika mkoa wa Katavi, Wilaya ya mlele, kata ya usevya na mtaa wa kasunzulu. Ila makazi yangu ya kudumu ni Wilaya ya Sengerema mkoani Mwanza.

Ndugu zangu, nipo hapa kutafuta mtu yeyote ambaye ana mtaji (Rasilimali fedha) ili tuanzishe mradi wa kilimo biashara katika mkoa huu wa katavi maana ni miongoni mwa mikoa ambayo bado ina fursa kubwa za uwekezaji katika kilimo biashara.

Miongoni mwa fursa hizo ni kama ifuatavyo:-

1) Uwepo wa ardhi ya kutosha na yenye rutuba (matumizi/mahitaji ya mbolea za viwandani katika uzalishaji yapo chini sana).

2) Gharama za kukodi/kununua mashamba zipo chini sana.

3) Uwepo wa mito na schemes za umwagiliaji (mfano, KILIDA irrigation scheme na KASHISHI irrigation scheme) unatoa fursa kubwa kwa uanzishwaji wa miradi ya kilimo cha umwagiliaji.

4) Kwa upande wa kilimo biashara bei za mazao huku ziko chini sana hivyo kutoa fursa ya kununua mazao ya huku kwa bei ndogo na kusafirisha kwenye masoko ya walaji wakubwa mikoa mingine ili kutengeneza faida maradufu.

5) Gharama za kuishi katika mkoa huu zipo chini pia.

6) Urahisi wa upatikanaji wa nguvukazi (vibarua) ukilinganisha na mikoa mingine maana asilimia kubwa ya vijana wa huku wana mapenzi (passion) na kilimo.

Hivyo basi, Jukumu kubwa la muwezeshaji litakua ni kuwekeza fedha zake katika miradi pendekezwa na kujipatia faida zitakazo zalishwa na miradi pendekezwa huku mimi nikiwekeza mtaji wangu (Rasilimali muda na ujuzi) katika usimamizi wa shughuli zote za miradi pendekezwa.

Kitendo cha kutokua na mke na mtoto kwasasa kitanipa fursa kubwa ya kuelekeza focus yangu yote katika kazi na vilevile kuwa na uwezo wa kuzunguka mikoa mbalimbali katika shughuli za uendeshaji wa miradi na biashara kwa ujumla.

Penye nia pana njia, mgaagaa na upwa hali wali mkavu na mtembea bure si sawa na mkaa bure pasipo kujishughulisha.

Nakaribisha maswali, maoni na mapendekezo yeyote kutoka kwenu wakuu.

Mtu yeyote atakaye guswa na mwenye nia ya dhati ya kuisaidia serikali katika kupanua "Wigo" wa uwezeshaji vijana katika kujiajiri namkaribisha hapa au PM kwaajili ya mazungumzo ya kina.

~Nawasilisha~
Mungu akusaidie. Ila kilimo sio rahisi kiasi hicho. Darasani ni rahisi, ila kilimo chenyewe ni balaa.
 
Amina mkuu.
Binafsi naamini hakuna shughuli yeyote isiyo na changamoto hapa duniani. Nikiwa kama mtaalamu wa kilimo ninaingia kwenye mapambano nikiwa na success rate (asilimia za kufanikiwa) kubwa maana huko shambani najua nianzie wapi, nilime nini, nilime wapi na nilime kwa wakati gani.
Utafanikiwa tu. Tena huhitaji mtu akusaidie milioni mbili ili uanze shughuli za kilimo. Hebu fanya jitihada zozote zile hata za kuomba vibarua visivyoendana na profession yako ili upate walau pesa kidogo za kuanzia. Kuna mwimbaji alisema mtaji wa maskini ni nguvu zake mwenyewe. Hata pesa unazotumia kununua bundle kusoma nyuzi JF, ukizichanga vizuri zitakusogeza kwenye mtaji.
 
Habarini za mchana ndugu zangu na poleni kwa majukumu mazito ya ujenzi wa taifa.

Mimi ni kijana wa kiume na Mtanzania mwenye umri wa miaka 28. Nina Elimu ya chuo kikuu katika ngazi ya shahada ya kilimo na katika hali ya ndoa mimi bado sijaoa na wala sina mtoto kwasasa.

Hivi sasa ninapatikana katika mkoa wa Katavi, Wilaya ya mlele, kata ya usevya na mtaa wa kasunzulu. Ila makazi yangu ya kudumu ni Wilaya ya Sengerema mkoani Mwanza.

Ndugu zangu, nipo hapa kutafuta mtu yeyote ambaye ana mtaji (Rasilimali fedha) ili tuanzishe mradi wa kilimo biashara katika mkoa huu wa katavi maana ni miongoni mwa mikoa ambayo bado ina fursa kubwa za uwekezaji katika kilimo biashara.

Miongoni mwa fursa hizo ni kama ifuatavyo:-

1) Uwepo wa ardhi ya kutosha na yenye rutuba (matumizi/mahitaji ya mbolea za viwandani katika uzalishaji yapo chini sana).

2) Gharama za kukodi/kununua mashamba zipo chini sana.

3) Uwepo wa mito na schemes za umwagiliaji (mfano, KILIDA irrigation scheme na KASHISHI irrigation scheme) unatoa fursa kubwa kwa uanzishwaji wa miradi ya kilimo cha umwagiliaji.

4) Kwa upande wa kilimo biashara bei za mazao huku ziko chini sana hivyo kutoa fursa ya kununua mazao ya huku kwa bei ndogo na kusafirisha kwenye masoko ya walaji wakubwa mikoa mingine ili kutengeneza faida maradufu.

5) Gharama za kuishi katika mkoa huu zipo chini pia.

6) Urahisi wa upatikanaji wa nguvukazi (vibarua) ukilinganisha na mikoa mingine maana asilimia kubwa ya vijana wa huku wana mapenzi (passion) na kilimo.

Hivyo basi, Jukumu kubwa la muwezeshaji litakua ni kuwekeza fedha zake katika miradi pendekezwa na kujipatia faida zitakazo zalishwa na miradi pendekezwa huku mimi nikiwekeza mtaji wangu (Rasilimali muda na ujuzi) katika usimamizi wa shughuli zote za miradi pendekezwa.

Kitendo cha kutokua na mke na mtoto kwasasa kitanipa fursa kubwa ya kuelekeza focus yangu yote katika kazi na vilevile kuwa na uwezo wa kuzunguka mikoa mbalimbali katika shughuli za uendeshaji wa miradi na biashara kwa ujumla.

Penye nia pana njia, mgaagaa na upwa hali wali mkavu na mtembea bure si sawa na mkaa bure pasipo kujishughulisha.

Nakaribisha maswali, maoni na mapendekezo yeyote kutoka kwenu wakuu.

Mtu yeyote atakaye guswa na mwenye nia ya dhati ya kuisaidia serikali katika kupanua "Wigo" wa uwezeshaji vijana katika kujiajiri namkaribisha hapa au PM kwaajili ya mazungumzo ya kina.

~Nawasilisha~
Wazo zuri sana, unapatikana vipi sasa, nicheki tuyajenge 0712363358
 
Ni ushauri mzuri umetoa mkuu lakini changamoto ya huku niliko mimi ni kijijini sio mjini ambapo unaweza pata uhakika wa kupata kibarua kila unapohitaji.

Vibarua vingi vya kijijini ni labda usubiri msimu wa kilimo ukalime mashamba ya watu wasio wazawa wa huku maana wakulima wengi wa huku wanatumia watoto wa familia zao wenyewe kama nguvukazi ya shambani.

2M ni ndogo lakini kwa chimbuko la familia yetu hio pesa siwezi kuipata kwa mwanafamilia yeyote.
Sehemu yoyote wanauotumia wanafamilia kulima kwa jembe la mkono basi hao wakulima ni maskini na hawatatoboa.
Tushirikiane kupinga jembe la mkono na kutumia watoto ktk kilimo. Familia zetu zitaendelea kuwa maskini.
Niwapongeze wapogoro wa ifakara, wanatumia trekta kulima maashamba yao ya mpunga, nilikaa huko mwaka 2008/9.
 
Elite power una mawazo mazuri

Changamoto ni uaminifu, Mimi binafsi kuna vijana nimekutana nao hapa JF, wachache waaminifu wengi wakikaa sehemu yenye mali wanapiga janja janja.

Anaway kila la kheri Mimi nipo interested na Songea/Ruvuma
 
Nashukuru mkuu kwa kulipongeza wazo langu.
Changamoto ya uaminifu ni kubwa sana hakika kwasisi vijana na imetukosesha na inaendelea kutukosesha fursa muhimu ya kushikwa mkono na wafadhili mbalimbali.
Suala la kuandikishana mkataba wa kisheria ni muhimu sana katika zama hizi ili kulinda maslahi na uwajibikaji wa pande zote mbili.
 
Elite power una mawazo mazuri

Changamoto ni uaminifu, Mimi binafsi kuna vijana nimekutana nao hapa JF, wachache waaminifu wengi wakikaa sehemu yenye mali wanapiga janja janja.

Anaway kila la kheri Mimi nipo interested na Songea/Ruvuma
Binafsi niko tayari kufanya kazi mkoa wowote ambapo mfadhili atapendekeza.
 
Shida kubwa ya nyie vijana wa kitanzania si mtaji bali UAMINIFU. Hamna uaminifu kabisa na hamjielewi. Mnalewa pesa haraka, hamko focused, mna elements za wizi na ujanja ndani yake. Tatizo hili lisingekuwepo, ajira zingekuwa nyingi sana. Lakini pia kwa upande wako mtoa mada, JF ina wasomaji members na non members. Ingekupendeza kwa Jambo ulifanyalo ungetumia jina lako halisi au kuweka namba zako Ili hata non members uwapate.
 
Kila la heri kijana mwenzangu.
Binafsi tumetengeneza kikundi cha vijana 5 tayari tumepata wawekezaji. Mungu akipenda mwezi wa 8 tunaanz rasmi shughuli za kilimo,Sisi tutajikita mkoa wa Ruvuma.
Ninakutakia kila lililo jema
 
Naomba nije pm mkuu kwa maelezo zaidi
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom