Nyani Ngabu
Platinum Member
- May 15, 2006
- 92,216
- 113,519
Hivi kwa sisi tulio na watoto wadogo na tunafanya kazi watoto wetu tuwe tunawapeleka wapi kama tusipokuwa na Msaidizi?
Hivi wewe unaelewa tofauti ya "msichana (bila aibu eti msichana, kwa nini asiwe mvulana?) wa kusaidia kazi za nyumbani" kama kichwa cha mada kinavyosema na mwangalizi wa watoto? Msichana wa kusaidia kazi za nyumbani = maid, mwangalizi wa watoto = babysitter. Unataka kuniambia hakuna tofauti hapo?
Kuna watu ambao hawana watoto au ambao watoto wao wameshakuwa wakubwa lakini bado wana wasaidizi wa kazi za nyumbani. Hawa ndio haswa ninaowazungumzia mimi. Kuajiri mtu wa kukuangalizia mtoto ni jambo linaloeleweka kwa watu wengi na karibu lipo ktk kile pembe ya dunia hii. Lakini hili la mfanyakazi wa ndani akufuliaye nguo na kukupikia kabla hujarudi kutoka kazini huku huna watoto wadogo limezidi bana. Mimi kamwe sijawahi kuajiri mtu na sitakuja kuajiri mtu wa kunifanyia kazi ndani ya nyumba yangu. Napika, nafua, nasafisha mwenyewe. Mtu wa kuniangalizia mtoto nikiwa kazini hilo wala silipingi.